Tafuta

2020.12.06 sala ya Malaika wa Bwana 2020.12.06 sala ya Malaika wa Bwana  

Papa Francisko:Hakuna janga linaloweza kuzima mwanga wa Noeli

Papa Francisko amewaalika wakristo kufungulia mioyo yao katika mwanga wa Kuzaliwa kwa Bwana na kuwafikiria wale wote wenye kuhitaji.Watengeneze ishara katika majumba yao kwa ajili ya furaha ya siku kuu lakini wasiishie hapo bali kujikita kwa kina juu matumaini.Hakuna janga,hakuna mgogoro ambao unaweza kuzima mwanga wa Kuzaliwa kwa Bwana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican Dominika tarehe 6 NìDesemba 2020, amewasalimia wote wa kuwapongeza kwa ujasiri wao licha ya hali mbaya ya hewa, akiwakumbuka waroma, mahujaji na wote wanaofuatilia kupitia vyombo vya habari. Papa Francisko amewaonesha katika uwanja wa Mtakatifu Petro uwepo wa mti mrefu sana wa mapambo ya siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Amewakumbusha wote kwamba katika siku hizi watu wengi katika majumba yao wanaandaa ishara hizi za siku kuu, kwa ajili ya furaha ya watoto, lakini pia hata wakubwa!

Ni ishara za matumaini, hasa katika wakati huu mgumu. Lakini amehimiza  kutosimama  kuangalia juu ya ishara hizo, bali ni kujikita  kwa kina juu ya maana yake yaani Yesu, upendo wa Mungu mbao kwa njia yake aliuonesha, kwenda katika wema wake usio na mipaka ambao alifanya uangaze ulimwenguni. Papa Francisko ameongeza kusema: “Hakuna janga, hakuna mgogoro ambao unaweza kuzima mwanga huo. Tumuacha aingie ndani ya mioyo yetu na tuwasaidie wale ambao wanahitaji. Kwa kufanya hivyo Mungu atazaliwa kwa upya ndani mwetu na katikati yetu”,Papa amesema. Kwa kuhitimisha amewatakia Dominika njema na wasisahau kusali kwa ajili yake.

06 December 2020, 14:29