Tafuta

Sala ya Malaika wa Bwana Sala ya Malaika wa Bwana  

Papa Francisko:Baraka kwa watoto na mtoto Yesu

Msisahau furaha.Mkristo ni mwenye furaha moyoni hata katika matatizo.Ni kuwa na furaha kwa sababu yuko karibu na Yesu.Ni yeye anayetupatia furaha.Ni ushauri wa Papa kwa waamini wote wakati wa kuhitimisha Sala yake kwa waamini na mahujaji waliounganika mjini Vatican kusali Sala ya Malaika wa Bwana,Dominika ya tatu ya Majilio tarehe 13 Desemba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko mara baada ya tafakari yeke kwa waamini wote  waliunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Dominika rarehe 13 Desemba 2020 ametoa  salamu zake kwa kuwaeleza kuwa: “Ninawasalimia ninyi nyote, waroma na mahujaji. Kwa namna ya pekee ninawasalimia makundi ambayo yamekuja kuwakilisha familia na watoto wa Roma katika fursa ya kubariki sanamu za mtoto Yesu, utaratibu ambao unaandaliwa katika vituo katoliki vya mafundisho Roma”.

Akiendelea na ufafanuzi huo amesema “Mwaka huu mpo hapa wachake kwa sababu ya janga, lakini ninatambua kuwa watoto wengi na vijana wameunganika katika vituo vyao na katika nyumba zao huku wakifuatilia kwa njia ya vyombo vya mawasiliano. Kwa kila mmoja ninamsalimia na kubariki hizo sanamu za mtoto Yesu ambazo zitawekwa kwenye Pango kama ishara ya matumaini na furaha”.

"Kwa ukimya tubariki watoto….. Mara baada ya ukimya huo Papa amesema “mtakapokuwa mnasali nyumbani mbele ya Pango mkiwa na familia zenu, basi acheni mvutiwe na upendo wa mtoto Yesu aliyezaliwa maskini katikati yetu ili kutupatia upendo wake”.

“Kwa wote ninawatakia Dominika Njema! Msisahau furaha. Mkristo ni mwenye furaha moyoni hata katika matatizo; ni kuwa na furaha kwa sababu yuko karibu na Yesu. Ni yeye anayetupatia furaha, msisahau kusali kwa ajili yangu. Mlo mwema na kwaheri ya kuonana! Amehitimisha Papa.

13 December 2020, 13:42