Mwaka 2020 wa Papa Francisko:nguvu ya sala wakati wa janga

Dharura ya kiafya ulimwenguni ya Covid-19 imesimamisha ziara za Kimataifa, kwa mwaka 2020, lakini Papa amebaki kidete na daima karibu na waamini wake, shukrani kwa nguvu ya sala.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Dominika tarehe 8 Machi 2020 ulikuwa ni mstari unatengensha kabla na baada ya tarehe hii. Ilikuwa ni siku ya sala ya Malaika wa Bwana http://www.vatican.va/content/francesco/en/angelus/2020/documents/papa-francesco_angelus_20200308.html ya Papa Francisko kwa njia ya Audio na video akiwa katika Jumba la Kitume. Karantini iliyowekwa kwa sababu ya janga la virusi vya  corona au Covid-19 vilikuwa vimeingilia kati. Papa Francisko akianza tafakari alisema “utafikiri ni jambo la ajabu kufanya sala ya Malaika wa Bwana namna hii na Papa amefungwa katika maktaba, lakini mimi ninawaona”. Baadaye bila kupangwa, Papa alichungulia dirishani kupitia Jumba la kitume ili kubariki Uwanja wa Mtakatifu Petro. Kwa kutojuayajayo, lakini uwanja huo kadiri ya siku na miezi ukabaki wazi na kimya; kwa kuweza  kuujaza zilikuwa ni sala za kipapa na matumaini ya ulimwengu. Kiukweli, inaonesha wazi kwani chini ya mvua, Papa Francisko katika usiku wa tarehe 27 Machi ikiwa ni Ijumaa ya Kwaresima alifanya http://www.vatican.va/content/francesco/en/homilies/2020/documents/papa-francesco_20200327_omelia-epidemia.html muda maalum wa maombí katika kipindi cha janga’ kwa kuwaalika binadamu wote wasiwe na hofu na kukambidhi Bwana: “tunayo matumaini alisema, katika msalaba wake tumetakaswa na kukumbatiwa ili pasiwepo lolote linalo tutenganisha na upendo wa mkombozi.

Sala kwa ajili ya dharura ya kiafya ilirudiwa hata katika katekesi zake za mwaka 2020: ya kwanza kiukweli Papa alijikita katika mzunguko mzima ambao alianza ‘tarehe sita Mei’ na kuendeleza tena tarehe 7 Oktoba.  http://www.vatican.va/content/francesco/en/audiences/2020/documents/papa-francesco_20200506_udienza-generale.html. Kwa kuongozwa na mada  ya “ uponywaji wa ulimwengu”,  Papa alitafakari kuanzia mwezi Agosti akikumbusha kwa namna ya pekee tarehe19 Machi umuhimu wa  upatikanaji wa chanjo kwa ajili ya ulimwengu wote. General Audience of 19 August 2020 - Catechesis “Healing the world”: 3. The preferential option for the poor and the virtue of charity | Francis (vatican.va). Mzunguko wa tatu wa Katekesi kuanzia Januari hadi mwishoni mwa Aprili, alijikita kutazama ‘Heri za mlimani’. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, katekesi zake kwa ujumla zitakuwa 46 mwaka huu na mara 58 za sala ya Malaika wa Bwana na Malkia wa Mbingu na mahali ambapo amepata fursa ya kutoa idadi kubwa ya miito kuhusu amani.  Inayoshinda kati ya yote ni ushauri wa tarehe 19 Julai: Angelus, 19 July 2020 | Francis (vatican.va) :  “Ninapyaisha kwa wote kusitisha mapigano ulimwenguni na mara moja, ambayo itaruhusu amani na usalama muhimu wa kutoa msaada wa kibinadamu unaohitajika”.

Tangu tarehe 9 Machi hadi tarehe 18 Mei, zaidi kutokana na kwamba nchini Italia hapakuwapo na uwezekano wa kuadhimisha misa kwa watu wa Mungu, Papa Francisko aliridhia kufanya Misa ya moja kwa moja kwa njia ya televisheni, audio na video ambazo alikuwa akiongoza kila siku saa 1.00 kamili asubuhi katika kikanisa cha Mtakatifu Marta, Vatican. Misa ya mwisho ya moja kwa moja ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ‘asubuhi ya tarehe 8 Mei’, Holy Mass for the 100th anniversary of Saint John Paul II's birth (18 May 2020) | Francis (vatican.va) siku ambayo ilikuwa inakumbusha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II. Mwaka 2020 vilevile ni mwaka wa Waraka wa tatu wa Papa Francisko ambao uliochapishwa tarehe 4 Oktoba wa  “Fratelli tutti”, ‘wote ni Ndugu’ Fratelli tutti (3 ottobre 2020) | Francesco (vatican.va) ambamo Papa anaelekeza udugu na urafiki wa kijamii kama njia msingi kwa ajili ya kujenga dunia iliyo bora. Awali tarehe 2 Februari, ulikuwa umechapishwa Wosia wa Kitume wa (“Querida Amazonia”, “Querida Amazonia”: Post-Synodal Exhortation to the People of God and to All Persons of Good Will (2 February 2020) | Francis (vatican.va) ambao ni tunda la Sinodi ya maalum kwa ajili ya Kanda ya  Amazonia, ni Sinodi iliyofanyika kunako mwezi Oktoba 2019.   Hati hiyo inawakilisha matumaini ya Papa Francisko kwa ajili ya Kanisa moja ambalo linakuwa na uso wa kiamazonia na katika nyayo mpya za uinjilishaji na utunzaji wa mazingira.

Siyo kwa bahati mbaya mwaka huu unatazama hata kumbu kumbu ya Waraka wa pili wa Papa Francisko wa  “Laudato si’”, ‘yaani sifa iwe kwako’, kuhusu utunzaji bora wa mazingira nyumba yetu ya pamoja na ambao umeadhimisha tarehe 18 Juni kwa kutangazwa Hati iitwayo” ‘njia za utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja’ Conferenza Stampa di presentazione del Documento dal titolo “In cammino per la cura della casa comune – A cinque anni dalla Laudato si’ ”, elaborato dal Tavolo Interdicasteriale della Santa Sede sull’ecologia integrale (vatican.va) iliyofanyiwa kazi na kuandaliwa na kikundi cha pamoja na Baraza la Kipapa kuhusu Ekolojia Fungamani na ambayo lengo lake ni kuhimiza kila mkristo kuwa na uhusiano safi na kazi ya uumbaji. Tarehe 24 Mei  baadaye ulizinduliwa “mwaka maalum wa Laudato si’”,na wakati huo huo  huo tarehe 12 Desemba Papa Francisko ametuma ‘ujumbe kwa njia ya video’  Video message of the Holy Father for the High Level Virtual Climate Ambition Summit 2020 (12 December 2020) | Francis (vatican.va) kwa washiriki wa Mkutano wa ngazi ya juu kimataifa  kwa njia ya mtandao kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi  ambapo alizungumza na Umoja wa Mataifa katika kuonesha jitihada za Vatican za upungazaji wa hewa chafunzi kufikia Zero kabla ya mwaka 2050. Na kati ya barua za kitume za mwaka  2020, inaonesha  ili ya  “Patris corde”,  yaani “Moyo wa ubaba” iliyochapishwa tarehe 8 Desemba katika fursa ya mwaka wa 150 tangu kutangazwa mchumba wa Maria, Mtakatifu Yosefu kuwa Mlinzi na msimamizi wa Kanisa Katoliki kwa utashi wa Papa Mwenyeheri Pio IX. Katika fursa ya hiyo Idara ya Toba ya Kitume imetangaza Mwaka Maalum wa Mtakatifu Yosefu ambao utahitimishwa tarehe 8 Desemba 2021.

Katika Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 27 Desemba, Papa Francisko amesema kuwa tarehe 19 Machi 2021 utazinduliwa Mwaka wa “Famiglia Amoris Laetitia”, na ambao utahitimishwa tarehe 26 Juni 2022 katika mwaka wa kumi tangu kuanzishwa Mkutano wa Familia ulimwenguni na ambao unatarajiwa kufanyika jijini Roma. Mwaka ambao unakaribia kuisha, unatazama  hata baadhi ya maadhimisho maalum yaliyoongozwa na Papa. Tarehe 26 Jauari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa aliadhimisha Misa kwa mara ya kwanza ‘Dominika ya Neno la Mungu’ ambayo ilitangazwa na Papa mnamo 2019. Tarehe 10 Aprili, katika uwanja  wa Mtakatifu Petro, ilifanyika (alla Via Crucis,) Njia ya Msalaba na  tafakari iliyoandadaliwa na wafungwa wa “Due Palazzi” wa  Padua, Italia.  Baada ya ibada hiyo Papa Francisko hakusema neno lolote, bali ukimya wa sala na ndiyo ilikuwa nguvu ya Kanisa na  aina ya neno. Ukimya huo, ulijaa imani, ulimsindikiza miezi ya badaye (in Piazza di Spagna), katika Uwanja wa Hispiania, Roma. Ilikuwa ni tarehe 8 Desemba katika Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili na ambapo Papa Francisko alijiunda kwa ukimya kwa sala chini ya sanamu ya Bikira Maria.

Tarehe 12 Aprili , Siku ya Pasaka ya Ufufuko Bwana, Katika Kanisa Kuu, ambalo lilikuwa karibu ni wazi: Papa Francisko aliongoza Misa kwa uwepo wa waamini wachache sana na kutamka l’Urbi et Orbi mbele ya altare ya Maungamo. Siku hiyo ilikuwa na tukio la kimataifa  hasa kwa kuona janga la Cabo Delgado, chini Msumbuji. Kati ya miito aliyoitoa kuhusu amani  Papa Francisko alibainisha katika  Ujumbe wake kwa jiji na kwa ulimwengu  mzima ambapo kiukweli ulikuwa ni mwangwi wa ujumbe wa Mkoa ya Kaskazini mwa  Nchi hiyo, ambayo kwa miaka mitatu sasa vurugu na mgogoro inaendelea.  Na katika muda huo huo ni kama  kwamba Papa Francisko aliweka Cabo Delgado katika ramani ya ulimwengu. Vile vile, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, liliona maadhimisho ya Kristo Mfalme tarehe 22 Desemba,  maandhimisho ya kukabidhi Msalaba na Picha ya Maria, ishara mbili za Siku ya Vijana ulimwenguni, makabidhiano yalikuwa kati ya vijana wa Panama nchi iliyokaribisha vijana mwaka 2019 na kuwakabidhi vijana wa Lisbon, mji ambao utakaribisha tukio la mwaka 2023.  Kwa ajili ya fursa hiyo,kwa hati Holy Mass for the handing over of the WYD Cross (22 November 2020) | Francis (vatican.va)Papa aliaazimia kuwa maadhimisho ya Siku ya vijana  ulimwenguni kijimbo ya yaadhimishwe kutoka Dominika ya Matawi na kuwa katika Dominika ya Kristo Mfalme.

Kwa mtazamo wa mageuzi, katika mwaka ambao unakaribia kuisha, Papa Francisko ametia saini hati mbali mbali, kwa mfano  mwezi Machi aliridhia la legge CCCLI sull’ordinamento giudiziario dello Stato Città del Vaticano ‘sheria ya 151 kuhusu mahakama ya mji wa Vatican’, ambayo ilikuwa inasasisha ile iliyochapishwa mnamo 1987, na kuwapa uhuru zaidi mahakimu.  Tarehe 1 Juni  kwa barua ya Motu Proprio  “Norme sulla trasparenza, il controllo e la concorrenza dei contratti pubblici della Santa Sede e della Città del Vaticano”, ya kanuni kuhusu ‘uwazi wa uthibiti na mikataba ya umma na Vatican’. Ikafuatia tarehe 5 Desemba kuhusu, Statuto dell’Autorità di Informazione Finanziaria,‘Sheria ya Mamlaka ya habari za Fedha kuwa Mamlaka ya Usimamizi na Habari za Fedha’. Na mwisho,  tarehe 28 Desemba kwa barua ya  Motu proprio “Circa alcune competenze in materia economico-finanziaria”, yaani  “Kuhusu umahiri fulani katika masuala ya kiuchumi na kifedha”, na mali zisizohamishika za  Sekretarieti ya Serikali pamoja na Mfuko wa Mtakatifu Petro kuhamishiwa APSA.  Na wakati huo huo wameongeza nguvu ya nafasi ya uthibiti wa Ofisi ya Katibu wa  Uchumi ambayo itakuwa na kazi ya Ukatibu wa Kipapa kwa ajili ya masuala ya uchumi na fedha.

Ilikuwa na umihumu hata ile ya  tarehe 22 Oktoba wakati wa kupyaisha kwa miaka miwili kuhusu  dell’Accordo Provvisorio tra la Santa Sede e la Repubblica Popolare Cinese, ‘Mkataba wa Muda kati ya Makao ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China’ ilikuwa imetiwa saini Jijini Beijing mnamo 2018 , na unaotazama juu ya kuchaguliwa kwa Maaskofu. Mkataba huo ulifuatiwa na tukio la tarehe 24 Novemba kwa nomina di un nuovo presule, ‘kuteuliwa kwa Askofu  Tommaso Chen Tianhao, ambaye ataongoza jimbo la Qingdao.  Katika mwezi huo huo Novemba, Jumanne tarehe 10, ilichapishwa  “Rapporto sulla conoscenza istituzionale e il processo decisionale della Santa Sede riguardante l’ex Cardinale Theodore Edgar McCarrick”. Ripoti kuhusu utambuzi kikatiba na mchakato wa maamuzi ya Vatican kuhusiana na aliyekuwa Kardinali Theodore Edgar McCarric”. Aliye tambuliwa kuwa muhusika wa manyanyaso ya kijinsia kwa watoto na kujidhulu katika uklero mnamo 2019. Kardinali wa zamani ni mada kubwa iliyopo katika hati  ambayo Sekretarieti ya Serikali inashughulikia kwa niaba ya Papa. Na Papa mwenyewe aliweza kuzungumzia katika Katekesi yake ya tarehe 11 Novemba: General Audience of 11 November 2020: Catechesis on prayer - 14. The persevering prayer | Francis (vatican.va):Jana imechapishwa Ripoti ya uchungu kuhusu aliyekuwa kardinali wa zamani Theodore McCarrick, alisema, na kwamba,  Ninapyaisha ukaribu wangu kwa waathirika wa kila manyanyaso na juhudi za Kanisa ili kuondoa mizizi ya ubaya huo.” Katika kuelekea mwisho wa mwaka 2020, kumekuwapo na mabadiliko ya Baraza la makardinali, kwani tarehe 28 Novemba, ikiwa ni katika Baraza la saba la Upapa wake, Papa Francisko aliwateua makardinali wapya 13, Ordinary Public Consistory for the creation of new Cardinals (28 November 2020) | Francis (vatican.va) akawaita katika nafasi mbalimbali kutoka pembeni mwa ulimwengu na Zaidi kuna nchi mpya kama vile Brunei na  Rwanda ambazo ziliingia kwa mara ya kwanza kuwa  sehemu ya kijiografua ya Baraza la Makardinali.

Na zaidi mwaka 2020, ni mwaka ambao haukuwa na ziara za Papa kimataifa na  ambaye ameweza kutoka nje  tu ndani ya nchi ya Italia. Ilikuwa ni tarehe 23 Februari, alikwenda huko Bari Katia fursa ya Mkutano wa tafakari na tasaufi ya “Mediterranea mpaka wa amani”. Visit of the Holy Father to Bari for the meeting of reflection and spirituality, “Mediterranean: frontier of peace” (23 February 2020) | Francis (vatican.va). Hapa Papa Francisko aliomba amani na udugu kwa sababu vita ni ukichaa ambao hatuwezi kujikabidhi kamwe”. Vile vile tarehe 3 Oktoba, Papa Francisko alikuwenda Assisi, in visita  privata,  kama ziara ya faragha  na juu ya kaburi la Mtakatifu Maskini Francis alitia saini Waraka wa  “Fratelli tutti”, yaani wote ni ndugu ambao ulichapishwa siku iliyofuata. Katika miezi hii 12, inarekodiwa idadi ya Ujumbe wwa Papa kwa njia ya video ambapo miongoni mwake ni ile ya tarehe 25 Septemba na tarehe 10 Desemba. Ya kwanza Papa Francisko aliwalekeza Mkutano Mkuu wa 75 wa Umoja wa Mataifa Video Message of His Holiness Pope Francis to the Seventy-fifth Meeting of the General Assembly of the United Nations (25 September 2020) | Francis (vatican.va) na kuzundua ushauri wa nguvu kwa jumuiya ya kimataifa ili waweze kusitisha mwisho wa mbio za kisilaha, kulinda haki za wahamiaji na kufikiria tena mifumo ya kiuchumi na fedha. Alishutumu  pia vikali juu ya utoaji mimba na kuomba uwepo wa huduma bora ya kibinadamu.  Ijumbe wa pili Il secondo  kwa njia ya video uliwaelekea washiriki wa Mkutano ulioandaliwa moja kwa moja mtandao wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu, kuhusu mgogoro wa Siria na Iraq. Papa alisema “lazima kufanya kwa namna kwamba uwepo wa wakristo katika ardhi hizo unaendelea kuwapo kama ilivyokuwa daima. Ni ishara ya amani, ya maendeleo, na upatanisho”.

Na ndiyo hiyo kweli nchini Iraq ambayo  ni matazamio ya Papa Francisko kunako mwaka 2021. Ilikuwa ni tarehe 7 Desemba ambapo ilitangazwa ziara ya Papa kuelekea katika Ardhi ya Iraq kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi ijayo. Dichiarazione del Direttore della Sala Stampa della Santa Sede, Matteo Bruni (vatican.va). Ni ziara ambayo Papa Francisko anatamani sana, na ambayo aliweza kuonesha nia hiyo tangu tarehe 2 Juni 20219, wakati wa nell’udienza ai partecipanti alla Riunione delle Opere di Aiuto alle Chiese Orientali (Roaco). Mkutano na washiriki wa Mkutano wa Matendo na Msaada wa Makanisa ya Mashariki (Roaco). Ishara hiyo pioa ilioneshwa  tarehe 25 Januari 2020 wakati Papa alipokutana mjini Vatican na Barhan Salih, Rais wa Jamhuri ya Iraq il Pontefice riceve in Vaticano Barham Salih, Presidente della Repubblica d'Iraq.  Kwa sasa ni kazi kwao katika Nchi kujenga daraja kati ya mwaka ambao unakwisha na mwingine unaanza , ili uweze kuchanua matumaini mapya.

29 December 2020, 11:24