Il Papa:ibada ya Zaire ni mwelekeo kama ule wa ibada ya Amazonia!

Katika utangulizi wa kitabu kilichopewa jina “Papa Francisko na Misale ya Roma kwa ajili ya majimbo ya Zaire chapisho la LEV, Papa anatafakari kuhusu utamadunisho wa liturujia ambayo lazima iguse moyo wa yule anayeishi katika Kanisa mahalia.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Ibada ya Zaire katika Misale ya Roma hadi sasa imekuwa ni moja ya ibada ya utamadunisho wa Kanisa la Amerika ya Kusini iliyoridhiwa baada  Mtaguso wa Vatican II  na mchakato huu ni wa utamadunisho wa kiliturujia huko Congo ambao ni mwaliko wa kuthamanisha zawadi mbali mbali za Roho Mtakatifu. Ndivyo Papa Francisko anasisitiza katika maandishi ya utangulizi ambao umewakilishwa mchana Jumanne tarehe Mosi Desemba 2020 mahali ambapo umakini huu ni kutaka kujua kwa kina mantiki tofauti ya misale ya Roma kwa ajili ya Majimbo ya Zaire iliyoridhiwa tangu mwaka 1988 na Baraza la Kipapa la Ibada, Sakramenti na nidhamu. Ni kitabu kilichochapishwa na kutolewa na Dula la Vitabu la Vatican kwa kuandaliwa vema na Rita Mboshu Kongo, mtawa wa Shirika la Mabinti wa Maria Mtakatifu na Profesa wa Taalimungu ya Kiroho na mafunzo ya kitawa katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urubaniana. Kitabu hicho kitakuwa  kwenye Duka la vitabu tarehe 9 Desemba.

Katika mwaka wa kwanza wa Ekaristi ulioadhimishwa na Papa katika Ibada ya kizaire, katika fursa ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Kikanisa Kidogo cha Congo jijini Roma, wamewakilisha kitabu hiki kipya ambacho kinaonesha hata Ibada ya Misa na baadhi  ya picha mbali mbali za sherehe hiyo. “Kitabu kiitwacho Papa Francisko na Misale ya Roma kwa ajili ya Majimbo ya Zaire”: Ibada inayoahidi tamaduni zingine”, Papa anaandika kuwa ni mfano wa utamadunisho wa kiliturujia ambayo inakumbusha hata Querida Amazonia ambayo ilibainishwa wazo  la namna ya kupokea katika liturujia mambo mengi muhimu ya uzoefu wa watu wa asili katika ndani ya mioyo yao na asili na kutoa chachu ya kielelezo asili cha nyimbo, ngoma, kucheza na ishara mbalimbali. Tayari katika Mtaguso wa  Vatican II ulikuwa umeomba jitihada hizo za utamadunisho wa liturujia kwa watu asilia , lakini imepitia miaka zaidi ya 50 na tumeweza kufanya maendeleo machache katika mwelekeo huo” amesema a Papa hasa katika Wosia wa Kitume wa baada ya Sinodi 2020.

Kwa maana hiyo katika muktadha wa ibada ya Zaire, anatoa ushauri kwa njia ile inayohaidi hata kwa ajili ya ushirikiano wa ibada ya Amazonia ambapo kadri mahitaji ya kiutamaduni ya eneo maalum la muktadha wa Kiafrika inavyotambuliwa, bila kubadilisha  asili ya Misale ya Kirumi, inadhibitisha kuendelea na tamaduni  ya zamani na ya ulimwengu ya Kanisa. Kutokana na hili ni matumaini ya Papa kwamba kazi hii inaweza kutusaidia kutembea katika mwelekeo huu huo. Katika utangulizi, huo Papa anasisitiza jinsi gani katika sherehe hiyo kulingana na ibada ya Zaire, inavyoleta msisimuku wa  utamaduni na hali ya kiroho iliyohuishwa na nyimbo za kidini katika kucheza  Kiafrika, sauti  za ngoma na vyombo vingine vya muziki ambavyo ni maendeleo ya kweli katika mizizi ya ujumbe wa Kikristo katika roho ya Congo. Ni sherehe ya furaha na mahali pa ukweli pa kukutana na Yesu, anabainisha, akinukuu mara kadhaa kutoka Wosia wa Evangelii gaudium.

Akizungumzia, kwa maana hiyo, juu ya umuhimu wa utamadunisho, Papa anasema kwamba baada ya kuwa na uzoef binafsi wa mkutano unaobadilisha na Kristo, kila watu wanatafuta kumwomba Mungu, aliyejifunua kupitia Yesu Kristo kwa maneno yake, na lugha yake ya kidini, kishairi, ishara na simulizi. Na ni kweli katika nguvu hii kwamba Baraza la Maaskofu wa Congo wamejitengenezea utu wake kwa kutaka kuomba Mungu, siyo kwa kupitia  wakala au kwa maneno yaliyokopeshwa kutoka kwa wengine, lakini kwa kuzingatia upendeleo wote wa kiroho, kijamii na kiutamaduni wa watu wa Congo na mabadiliko yake.

Kwa mtazamo huo wa kitabu bado ni urejesho katika  hitaji la kwenda kwa kitu ambacho kinagusa ulimwengu wa kiutamaduni wa watu kwa sababu liturujia  lazima iguse mioyo ya washiriki wa Kanisa mahalia na iwe ya kupendeza. Vile vile akiangazwa na Wosia wa Kitume wa juu ya  kutangazwa kwa Injili katika ulimwengu wa leo, unaodhaniwa kuwa ni maandishi ya mpango wa Hati ya Kipapa, Papa anakumbuka kwamba Ukristo hauna mfano hata mmoja wa kiutamaduni, lakini unabaki wenyewe kabisa, kwa uaminifu kamili kwa tangazo la utamaduni wa kiinjili na kikanisa, pia utachukua sura ya utamaduni na watu wengi ambao unakaribishwa na kuota mizizi. Kwa hivyo, katika watu tofauti wanaopata zawadi ya Mungu kulingana na tamaduni zao, Kanisa, linaelezea ukatoliki wake halisi"na unaonyesha uzuri wa uso huu wenye sura nyingi. Na Roho Mtakatifu hupamba Kanisa kwa kulionyesha mambo mapya ya Ufunuo na kulipatia sura mpya.

01 December 2020, 17:26