Wito kwa mara nyingine wa Papa kuhusu maelewano ya Pwani ya Pembe;na msaada Ufilipino!

Katika siku ya IV ya Maskini duniani,Papa Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana mtazamo wake umekuwa ni kwa ajili ya wale wenye kuhitaji zaidi,hasa waathirika wa ulimwengu huu hata wa vita na majanga ya mazingira.Ametoa wito kwa mara nyingine tena kuhusu nchini Pwani ya Pembe pia kukumbusha msaada kwa ajili ya nchi ya Ufilipino waliokumbwa na vimbunga.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amekumbusha siku ya Jumapili tarehe 15 Novemba  kuwa ni maadhimisho ya Siku ya Amani nchini Pwani ya Pemba ambayo katika Muktadha kwa bahati mbaya wa mivutano kijamii na kisiasa ambayo imesababaisha waathirika wengi. Anawatia moyo wahusika wa kitaifa na kimataifa ili waweze kutafuta muafaka kwa ajili ya wema wa taifa.

“Ninaungana katika maombi ili kupata kutoka kwa Bwana zawadi ya maelewano kitaifa; ninawasihi watoto wa kike na kiume wa nchi hiyo pendwa ili kushirikiana kwa uwajibikaji katika kutafuta upatanisho na kuishi kwa amani na utulivu. Kwa namna ya pekee ninawahimiza wahusika wakuu wa kisiasa kuanzisha tena hali ya kuaminiana na mazungumzo, katika kutafuta suluhisho la haki ambayo inalinda na kuhamasisha wema wa wote”.

Vimbunga viwili nchini Ufilipino kusababisha waathirika wengi

Papa Francisko akiendelea amesema yuko karibu katika maombi kwa ajili ya watu wa Ufilipino ambao wanateseka sana kutokana na uharibifu uliotokana na mafuriko ya nguvu ambayo yamesababishwa na dhoruba kali. Ameonesha mshikamano kwa familia maskini zaidi na ambazo zimo katika hali ngumu na kuomba msaada wote, pia kwa wale wote ambao wanajikita kuwasaidia.

Ikumbukwe wiki mbili za mwisho nchini Ufilipino wamekumbwa na dhoruba kali mbili za kipindi cha mwaka. Mwanzo mwa mwezi huu, kimbunga Goni kilisababisha vifo vya watu 26 na milioni moja ya mlundikano wa ndani wa watu na hivi karibuni, kimbunga kingine kiitwacho Vamco ambacho kimesababisha vifo na uharibifu katika Kisiwa kwani takwimu zinasema ni karibia watu 42 na wengine 20 kupotea.

Nchini Ufilippino ni moja ya nchi hatari zaidi ya majanga ya mazingira

Kabla ya kimbunga cha pili kugonga maeneo ya pwani, zaidi ya watu 400,000 walihamishwa na kupelekwa sehemu iliyo salama. Hata hivyo familia milioni 3.8 ziliachwa bila umeme katika mji mkuu na katika mikoa ya mbali. Ofisi za serikali zimefungwa na madarasa mengi yamesimamishwa. Ufilipino inakumbwa karibu na vimbunga 20 na dhoruba za kitropiki kila mwaka pia ina mitetemeko ya ardhi na kuifanya kuwa moja ya nchi zilizo hatarini zaidi kwa majanga ya mazingira ulimwenguni. Caritas ya Manila tayari inapeleka msaada kwa majimbo yaliyoathiriwa zaidi.

15 November 2020, 14:44