Tafuta

2020.11.28 Kusimikwa kwa makardinali 13 wapya 2020.11.28 Kusimikwa kwa makardinali 13 wapya 

Hata Papa na Makardinali,lazima kujitazama katika Neno la ukweli.Ni upanga unaokata kwa uchungu

Hata kwa Papa na Makardinali,lazima kujimulika katika Neno la ukweli.Ni upanga ambao unatukata na uchungu lakini wakati huo huo linatuponesha.Linatupa uhuru na kutupatia uongofu.Uongonfu ndiyo huo wa kutoka nje ya njia na kwenda katika njia ya Mungu.Roho Mtakatifu leo hii na daima atupatie neema hii.Ni hitimisho la tafakari ya Papa Francisko wakati wa kusimika makardinali wapya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika mahubiri ya Papa Francisko wakati wa kusimika makardinali wapya Jumamosi jioni tarehe 28 Novemba 2020 kwenye mkesha wa kipindi cha majilio, Papa Francisko ameanza na tafakari kwa kuongozwa na Injili illiyosomwa kwamba: Yesu na mitume walikuwa katika njia. Njia ni mazingira ambayo yanaoneshwa na mwinjili Marko (10,32-45). Na ni mazingira ambao daima Kanisa linatembea. Njia ya maisha, ya historia na ambayo ni historia ya wokovu katika kiwango kilichofanywa na Yesu, katika mwelekeo wa fumbo lake la Pasaka. Yerusalemu daima iko mbele yetu. Msalaba na Ufufuko vinahusiana na historia yetu na ndiyo leo yetu, lakini daima imekuwa hatima ya safari yetu.” Papa Francisko akiendelea amesema: “Neno hili la kiinjili mara nyingi limesindikiza usimikwaji wa makardinali wapya, na  siyo kiini tu ni maelekezo ya mchakato kwa ajili yetu leo hii ambao tunatembea pamoja na Kristo ambaye yuko mbele katika njia yetu. Yeye ni nguvu na maana ya maisha yetu na huduma yetu”, amesema Papa Francisko.

Yote ambayo Yesu anafanya ni kwa ajili ya wokovu wetu

Kwa njia hiyo “inahusu sisi kujipima na Neno hilo. Marko anaonesha wazi katika njia ndefu, mitume ambao walikuwa wanaogopa; je ni kwa sababu gani, kwa sababu walikuwa wanasubiri kile kilichokuwa kikiwasubiri huko Yerusalem; Yesu alikuwa amekwisha waeleza mara nyingi wazi. Bwana anajua hisia zao wale ambao walikuwa wanamfuata, na hiyo haiwezi kuacha na sintofahamu.  Yesu hakuwahi kuwaacha marafiki zake; wala hakokusa kuwajali kamwe. Hata wakati utafikiri anakwenda njia yake moja bila kugeuka; Yeye daima anafanya hivyo kwa ajili yetu. Yote hayo ambayo anafanya ni kwa ajili ya wokovu wetu. Katika kesi hiyo  kwa wale tenashala anafanya hivyo kwa kuwaandaa katika majaribu, ili waweze kuwa naye sasa na  baada yake, wakati yeye hatakuwa katikati yao tena. Ili kwamba  waweza kuwa naye katika njia yake. Alikuwa anajua kuwa moyo wa wafuasi wake umekuwa na wasi wasi, hivyo aliwaita hao kumi na mbili pembeni kwa uwazi na  kuwaambia yale ambayo yalikuwa yatokee baadaye. Lilikuwa ni tangazo la tatu la mateso, kifo na ufufuko wake. Hii ndiyo njia ya Mwana wa Mungu. Njia ya Mtumishi wa Mungu. Yesu anajifananisha  mwenyewe na njia hiyo. Mimi ni njia(Yh 16, 6) Njia hii na siyo njia nyingine. Baada ya kusema hayo ndipo palitokeza jambo jingine ambao linampa fursa Yesu ajieleze kwa Yakobo na Yohane lakini kiukweli ni kwa mitume wote, hatima  inayowasubiri. Papa ameongeza  kusema,  fikirieni baada ya kuwaeleza yale ambayo yatamtokea huko Yerusalemu, tazameni vizuri sura zao hao kumi na mbili wanavyomtazama akizungumza na kumkazia macho. Kwa maana hiyo Yakobo na Yohane wakamkaribia ili kumwomba wakae katika utukufu wake mmoja kulia na mwingine kushoto.

Yesu anatuvumilia na hakasiriki

Hii ni njia nyingine Papa anasema kwa maana siyo njia ya Yesu. Ni njia ya yule labda anayetaka bila kutambua kutumia Bwana ili kujihamasisha mwenyewe kama asemavyo Mtakatifu Paulo, aneyetafuta mafao yake na siyo ya Kristo ( Fil 2,21). Katika hilo Mtakatifu Agostino,  Papa amesema (N.46) anatoa takafari nzuri ya kichungaji ambayo  ni vuzuri kuisoma katika ofisi ya masifu. Yesu baada ya kuwasikiliza Yakobo na Yohane, hakukata tamaa wala kukasirika. Hekima yake kiukweli haina kipimo. Aliwajibu kuwa hawajuhi wanacho kiomba. Kwa maana nyingine anawaomba sahamani lakini pia wakati huo huo kuwashumu kuwa “ hamjuhi jinsi ambavyo mnakwenda nje ya njia” Kiukweli mara baada ya hapo mitume wengine waliwakemea watoto wa Zebedayo kwa kile ambacho walifanya. Papa Francisko akiendelea, amesema “sisi sote tunampenda Yesu, sisi sote tunataka kufuata lakini lazima kukesha ili kubaki katika njia yake. Kwani kwa kwa miguu, na mwili tunaweza kuwa naye, lakini kiroho tunaweza kuwa mbali na kupelekwa njia nyingine. Tufikirie aina nyingine ya  ufisadi katika maisha ya ukuhani.   Kwa mfano Papa amesema rangi ya vazi jekundu la ukardinali ambalo, linaweza kugeuka kuwa roho ya ulimwengu tofauti na ushauri wake. Na hautakuwa mchungaji tena karibu na watu. Utasikia kuitwa mheshimiwa  lakini ukisikia hayo, umepotea.

Yesu daima yuko katika njia sahihi lakini sisi nje ya njia

Kile ambacho kinashangaza daima katika simulizi hii ya Injili, Papa amesema ni ule unyeti wa kinyume kati ya Yesu na mitume wake. Yesu anajua, anatambua na kuwavumilIa. Lakini kinyume hiki kinabaki. Yeye ni katika njia, wao ni nje ya njia. Ni michakato miwili ya njia ambazo haziendi pamoja. Ni Bwana peke yake kiukweli anaweza kuookoa marafiki zake ambao wako hatarini, na kupotea, ni kwa njia ya msalaba na ufufuko wake. Kwa ajili yao zaidi kwa ajili ya wote, yeye anapanda huko Yerusalemu. Kwa ajili yao na kwa ajili ya wote amemega mwili wake na kumwaga damu yake. Kwa ajili yao na kwa ajili yetu amefufuka kutoka kwa watu na kwa zawadi ya Roho Mtakatifu anatusamehe dhambi na kubadilisha. Atawaweka hatimaye katika njia yake. Mtakatifu Marko na hata Matayo na Luka, waliweka simulizi hiyo katika Injili kwa babu ni Neno linalookoa na ambalo ni la lazima kwa Kanisa la nyakati zote. Hata kama mitume kumi na mbili wanaabisha, maandiko hayo yaliingia katika Kanoni kwa sababu inaonesha ukweli juu ya Yesu na juu yetu sisi. Ni neno la kufuata hata kwa ajili yetu sisi. Hata kwa ajili ya Papa na Makardinali, lazima kujimulika katika Neno la ukweli. Ni upanga ambao unatukata na uchungu lakini wakati huo huo linatuponesha. Linatupa uhuru na kutupatia uongofu. Uongofu ndiyo huo wa kutoka nje ya njia ili kwenda katika njia ya Mungu amehitimisha Papa na kusema kuwa  Roho Mtakatifu leo hii na daima atupatie neema hii.

28 November 2020, 16:20