Tafuta

2020.11.28 Kusimikwa kwa Makardinali 13 wapya 2020.11.28 Kusimikwa kwa Makardinali 13 wapya  

Papa na makardinali wapya wamtembelea Papa Benedikto XVI

Katika mkutano mfupi kwenye kikanisa cha Monasteri ya“Mater Ecclesiae”Makardinali wapya wamemsalimia kila mmoja Papa mstaafu Benedikto XVI na kusali kwa pamoja na hatimaye amewabariki.Hii ni tukio ambalo limetokea mara baada ya Makardinali wapya kusimikwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya maadhimisho ya kusimikwa kwa makardinali wapya kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,  Jumamosi jioni tarehe 28 Novemba 2020, Baba Mtakatifu  Francisko na makardinali wapya 11 waliopo jijini Roma, wamekwenda kumtembelea Papa Mstaafu Benedikto XVI kwenye Kikanisa cha Monasteri ya “Mater Ecclesiae”.

Makardinali wapya wamtembelea Papa Mstaafu Benedikto XVI
Makardinali wapya wamtembelea Papa Mstaafu Benedikto XVI

Hivyo ndivyo inavyosomeka taarifa kutoka kwa  Msemaji wa vyombo vya habari Vatican kwamba “ katika hali ya upendo makardinali wamejiwakilisha kila mmoja kwa Papa Mstaafu ambaye ameonesha furaha yake kwa kutembelewa nao na baada ya wimbo wa Salve Regina, yaani Salam Malkia, amewabariki kwa Baraka yake. Ziara yao imeitimishwa kabla ya saa 11.00 jioni hivi.

Utamaduni sasa wa ziara ya Monasteri Mater Ecclesiae

Ziara ya Monasteri ya Mater Ecclesiae mjini  Vatican sasa  imekuwa ya  kawaida na kama  utamaduniaambao unapyaishwa kuanzia kusimikwa kwa makardinali wapya mnamo 2016. Matukio mawili ya kwanza katika fursa ya mwaka 2014 na 2015, Papa Mstaafu aliweza kushiriki maadhimisho hayo moja kwa moja katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Hata hivyo inakumbukwa kuwa mwaka jana akikutana na makardinali wapya, Papa Mstaafu Benedikto XVI alikuwa amewakumbusha juu ya  thamani ya imani kwa Papa.

Salam ya Papa Francisko kwa Papa Benedikto XVI
Salam ya Papa Francisko kwa Papa Benedikto XVI
28 November 2020, 18:23