Papa Francisko:Yesu anajitambulisha katika wahitaji&hukumu ya mwisho ipo!

Papa Francisko katika tafakari ya Injili kuhusu uhukumu ya mwisho katika Siku kuu ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu amesema kuwa hukumu itakuwa juu ya upendo na siyo hisia.Tutahukumiwa kutokana na matendo yetu,juu ya huruma ambayo tumeonesha wengine,ukaribu na kutoa msaada kwa maskini.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican.

Bwana atatuhukumu juu upendo tulitoa au kukatalia wengine. Ni maneno aliyo sema Papa Francisko siku ya Jumapili, tarehe 22 Novemba 2020 mara baada ya misa ya Siku Kuu ya Kristo Mfalme na ikiwa ni siku ya kukabidhiana Msalamba wa Siku ya Vijana dunia. Papa Francisko katika tafakari kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, ameshauri kwa nguvu, kujiuliza ndani ya moyo ili kuweza kutambua hasa wenye kuhitaji msaada. Katika Siku kuu ya Bwana Yesu Kristo Mfalme wa ulimwengu ambayo inafunga mwaka wa kiliturujia, Papa Francisko amesema Yeye ni 'Alfa na Omega' yaani 'Mwanzo na Mwisho' wa historia; ambapo liturujia ya siku inajikita kuelezea mwisho wa dunia.  Maana ya maisha kwa hakika yanatambuliwa mbele ya macho ya matendo siku ya mwisho. Papa amesisitiza kuwa kinyume na ukristo Yeye ni Bwana wa historia, Mfalme wa ulimwengu, hakimu wa wote, Yeye hana mamlaka ya kutisha, lakini ni mchungaji aliyejaa upole na huruma. Katika kifungu cha Injili cha siku, Papa amesema, Yesu hajitambulishi kama mchungaji tu na mfalme, bali pia kama kondoo aliyepotea. Tunaweza kusema juu ya utambulisho wake maradufu. Kwanza mchungaji mfalme, pia Yesu na kondoo zake, yaani anajitambulisha na ndugu wadogo na wahitaji zaidi, amesisitiza Papa.

Hukumu ya mwisho itakuwa katika msingi wa upendo

Yesu analekeza kigezo cha hukumu kitachukuliwa katika msingi wa upendo halisi uliotolewa au kunyimwa watu hawa, kwa sababu yeye mwenyewe,ni hakimu, ambaye yuko katika kila mmoja wao. Yeye ndiye hakimu. Yeye ni Mungu, mwanadamu, lakini pia ni maskini, amejificha, yupo katika hali ya maskini anayemtaja. Yesu anasema: “Kweli ninawambia: kila kitu mlichofanya (au haukufanya) kwa mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea (au hamkufanya) mimi. Tutahukumiwa , hivyo hukumu itakuwa juu ya upendo. Siyo juu ya hisia, hapana: tutahukumiwa juu ya kazi, juu ya huruma ambayo ni ukaribu na msaada wa kujali wengine, Papa amesisitiza.

Je ninakwenda kukutana na wale wanaoteseka?

Swali kuu ambalo Papa ametaka tujiulize je ninamwendea Yesu aliye katika uso wa wagonjwa, maskini, wanaoteseka, wafungwa, wale ambao wana njaa na kiu cha haki?, Je ninamkaribia Yesu aliko huko? Mwisho wa ulimwengu, kiukweli, Bwana atapitia kundi lake, sio tu kwa upande wa mchungaji, bali hata kwa upande wa kondoo, ambaye amejitambulisha, amesema  Papa: "Umekuwa mchungaji wangu kwamba nilikuwepo katika watu hawa ambao walikuwa na uhitaji, au wewe haukujali?  Papa Francisko ametoa onyo “Kaka na dada, tujihadhari na mantiki ya kutokujali, ya kile kinachokuja akilini mara moja tu na baadaye unaangalia njia nyingine wakati tunaona shida.”

Inawezekana kufuata mantiki nyingine:Msamaria mwema

Papa Francisko ameshauri kufuata mantiki nyingine na kupata msukumo kutoka kwa Msamaria Mwema. Mantiki hiyo smeonesha Yesu mwenyewe “Kile mlichofanya kwa huyo mmenifanyia mimi. Na kile ambacho humkumtendea huyo na yule hamkunitenda mimi, kwa sababu nilikuwa ndani mwao.”  “Ninaomba Yesu atufundishe mantiki hii, mantiki hii ya ukaribu, ya kumsogelea, kwa upendo, katika mtu wa mateso zaidi”. Yesu, katika mfano huu wa hukumu ya mwisho, anatumia picha ya mchungaji, akimaanisha nabii Ezekieli, ambaye alikuwa amezungumza juu ya uingiliaji wa Mungu kwa niaba ya watu, dhidi ya wachungaji wabaya wa Israeli, wale ambao walikuwa mataifa yenye ukatili na unyonyaji, yakipendelea kujichunga badala ya ya kuchunga zizi”.

Ahadi kutimizwa kwa njia ya mchungaji mwema Yesu Kristo

Papa akiendelea amesema Mungu mwenyewe aliahidi kulitunza kundi lake, akililinda kutokana na dhuluma na ukosefu wa haki na kubaguliwa, na huku  akibainisha kuwa ahadi hii iliyotimizwa kikamilifu katika Yesu Kristo, Mchungaji Mwema. Kwa njia ya Mama Maria alieyemfuata Mwanawe kwa uaminifu kwenye njia ya upendo, lazima  tumwombe ili atufundishe kutawala kwa njia ya kutumikia na kujifunza kutoka kwake ili kuingia katika Ufalme wa Mungu kuanzia sasa, kupitia mlango wa huduma ya unyenyekevu na mkarimu .

22 November 2020, 18:11