Tafuta

2013.03.20 Papa Franisko akiwa na Patriaki Bartholomew I wa kiekuemene 2013.03.20 Papa Franisko akiwa na Patriaki Bartholomew I wa kiekuemene  

Papa Francisko:migogoro itaisha ikiwa kuna utambuzi wa udugu

Papa Francisko amemwandikia Patriaki wa Kiekumene Bartholomew I katika siku ambayo ni maadhimisho ya Sikukuu ya Mtakatifu Andrea msimamizi wa Upatriaki wa Constinoples.Kardinali Kurt Koch ameshiriki akiongoza uwakilishi wa Vatican katika Liturujia ya Misa Takatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika mtazamo wa utamaduni wa kubadilishana na kufanya sherehe, wawakilishi katika Siku kuu mbili ya Wasimamizi tarehe 29 Juni mjini Roma kwenye sherehe za Mtakatifu Petro na Paulo na ile ya tarehe 30 Novemba huko Istanbul kwa ajili ya sherehe ya Mtakatifu Andrea, Cardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja wa Kikristo ameongoza Uwakilishi wa Vatican kwa ajili ya Sherehe za Upartiaki wa kiekumene ambapo umejumuisha Katibu wa Baraza hilo Askofu Mkuu Brian Farrell, Katibu Msaidizi Askofu Andrea Palmieri kwenda Istanbul, kuungana na Balozi wa Kitume nchini Uturuki, Askofu Mkuu Paul F. Russell. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa vyombo vya habari amesema uwakilishi huo wa Vatican umeshiriki Liturujia Takatifu ambayo imeongozwa na Patriaki wa Kiekumene Bartholomew I katika Kanisa la Upatriaki la Mtakatifu George huko Fhanar. Kardinali Kurt Koch amemkabidhi Patriaki wa Kiekumene Ujumbe uliondikwa na Papa Francisko  mwenyewe na ambao umetangazwa mara baada ya Maadhimisho ya kiliturujia.

Katika Ujumbe Papa Francisko uliokabidhiwa  unasema kwamba katia siku kuu ya Mtume Andrea, Kaka yake mpendwa Mtakatifu  Petro na msimamizi wa Upatriaki wa Kiekume, anafurahi pamoja na Yeye kwa njia ya uwakilishi wake.  Anamshukuru Mungu kwa utajiri mkubwa wa matunda ya Mungu na Mpaji ayejionesha katika Maisha ya Mtakatifu Andrea. Papa Francisko anaandika kuwa kwa njia ya nguvu ya maombezi kwa Bwana wetu, ambaye alimwita kwake kuwa mmoja wa mitume wa kwanza anaweza kumbariki Patriaki na ndugu wote wajumbe wa sinodi takatifu, makuhani, watawa na walei ambao wameshiriki liturujia takatifu ya kusheherekea katika Kanisa la Upatriaki la Mtakatifu Geoege huko Phanar.  Papa Francisko anamkumbuka kwa furaha kubwa uwepo wake katika Mkutano wa pamoja kwa ajili ya kuombea amani uliofanyika mjini Roma tarehe 20 Oktoba iliyopita, kwa ushiriki wa viongozi mbalimbali wa Makanisa na tamaduni nyingine za idini.

Papa Francisko aidha katika ujumbe huo anaonesha kuwa pamoja katika changamoto zilizotokana na janga la sasa, vita vinavyoendelea, migogoro katika sehemu nyinyi za ulimwengu na zaidi  kwa wakati migogoro mingine ya kisilaha  inaibuka na kuiba maisha ya wanawake na wanaume wengi.  Bila shaka mipango yote iliyochukuliwa na taasisi za kitaifa na kimataifa zinazolenga kukuza amani zinafaa na zinahitajika, lakini mizozo na vurugu hazitakoma mpaka watu wote wafahamu zaidi kwamba wana jukumu la pamoja kama ndugu na dada. Kwa kuzingatia hilo, Makanisa ya Kikristo, pamoja na  tamaduni  nyingine za kidini, wana jukumu msingi la kuonesha mfano wa mazungumzo, kuheshimiana na ushirikiano wa vitendo.

Katika shukrani kubwa kwa Mungu, Papa amesema “nimepata uzoefu wa udugu huu kwa mara ya kwanza katika mikutano mbalimbali  ambayo tumeshiriki. Katika suala hili, ninakiri kwamba hamu ya ukaribu na maelewano kati ya Wakristo imedhihirika katika Jumuiya ya Dini ya Kiekumeni ya Constantinople kabla ya Kanisa Katoliki na Makanisa mengine kujishughulisha na mazungumzo.” Hii inaweza kuonekana wazi katika barua ya Sinodi Takatifu ya Upatriaki wa Kiekumeni iliyoelekezwa kwa Makanisa ulimwenguni hasa miaka mia moja iliyopita. Hakika, maneno yake Papa amesema  yanabaki kuwa muhimu leo hii. 

Papa Francisko anamshukru Mungu kwa uhusaino huu kati ya Kanisa katoliki na Upatriaki wa Kiekumene kwamba umeongezeka sana kwa karne nyingi zilizopita hata tunapoendelea kutamani kusudi la urejesho  wa muungano kamili ulioonyeshwa kupitia ushirikiano katika sadaka ya Ekaristi. Ingawa vizuizi vimebaki, Papa Francisko amesema ni uhakika  kwamba kwa kutembea pamoja kwa upendo wa pamoja na kufuata mazungumzo ya kitaalimungu, tutafikia lengo hilo. Tumaini hili linategemea na imani yetu ya pamoja katika Yesu Kristo, aliyetumwa na Mungu Baba kukusanya watu wote katika mwili mmoja, na jiwe la pembeni la Kanisa moja na takatifu, hekalu takatifu la Mungu, ambamo sisi sote ni mawe ya kuishi, kila mmoja kulingana na karama yetu au huduma tuliyopewa na Roho Mtakatifu.

30 November 2020, 15:51