Papa Francisko kwa vijana:Oteni ndoto kuu na kumchagua Mungu!

Papa Francisko wakati wa mahubiri yake tarehe 22 Novemaba katika Siku Kuu ya Kristo Mfalme wa Ulimwengu amewashauri vijana wawe na ndoto kubwa zinazowafanya wawe huru na kutafuta zaidi ya mawazo yanayotawala.Amewapa onyo kupunguza raha zinazowanyima furaha ya kweli,uwepo wa homa ya kutumia hovyo,na kuhepuka upendo wa hisia tu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ameongoza  Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Kristo Mfalme wa Ulimwenguni na siku ambayo imetolewa kwa ajili ya kukabidhi ishara za Siku ya Vijana duniani itakayo fanyika nchini Ureno kunako mwaka 2023. Akianza aguburu amesema "Maneno yaliyosikika ni sura ya mwisho ya Injili ya Matayo kabla ya Mateso. Kabla ya kutupatia upendo wake juu ya msalaba. Yesu alitupatia mapenzi yake ya mwisho. Anasema wema ambao tutawatendea walio wadogo, wenye njaa, kiu, wageni, wenye kuhitaji, wagonjwa, na wafungwa tumemfanyia yeye (Mt 25,37-40). Bwana anatukabidhi orodha ya zawadi ambazo anatamani katika Dunia na ili yaweze kurudi na yeye mbinguni. Ni huduma za huruma ambazo zinafanya maisha yetu yawe ya milele. Kila mmoja anaweza kujiuliza: je ninajiwekwa katika matendo? Ninafanya kitu kwa ajili ya wenye shida? Au ninatimiza wema kwa ajili ya watu wapendwa tu na kwa marafiki? Ninamsaidia mwingine ambaye hawezi kunirudishia kitu? Je mimi ni rafiki wa Maskini? Yesu anasema. “mimi Niko hapo, ninakusubiri pale, mahalia ambapo wewe ufikirii na mahali ambapo labda hutaki hata kutazama, pale alipo maskini. Lakini Mimi Niko pale, katika wazo kuu linalotawala, lakini linalopingana na wazo la maisha mazuri ikiwa yote ni mema na wale hawana maslahi. Lakini  Yesu anakwambia “Mimi Niko pale”, wewe  kijana unayetafuta kujikamilisha kwa ndoto za maisha.

Historia ya Mtakatifu Martino na maskini

Katika mahubiri hayo Papa Francisko amedndelea kusema kuwa, Yesu alisema mimi niko hapo, kwa karne nyingi kwa askari. Huyo alikuwa karibu na miaka 20 ambaye alikuwa hajabatizwa. Yule kijana aliona maskini akiomba msaada lakini hakupata kwani watu walikuwa waliopita mbali. Kijana kuona hivyo kwamba hakuna aliyekuwa na huruma, akajua kuwa maskini huyo alikuwa anahitaji. Kwa bahati mbaya  hakuwa na  kitu mfukoni mbali na  nguo yake rasmi ya kazi. Kwa maana hiyo aliamua kukata katikati joho lake na kumpatia maskini, huku akichekwa kutoka kwa baadhi ya waliokuwa wamemzunguka. Usiku uliofuata, aliota ndoto. Alimwona Yesu aliyekuwa amevaa, sehemu vazi lake alilomfunika  maskini. Alisikia sauti ikimwambia “Martino ulinifunika na nguo hii (taz. Maisha ya Martino III). Mtakatifu Martino alikuwa ni kijana ambaye aliota ndoto kwa sababu aliishi, bila kujua, kama wale wenye haki wa Injili ya siku, Papa Francisko amefafanua.

Kutafuta utukufu wa kweli usiokuja na kutoweka

Papa Francisko kwa maana hiyo amewaomba vijana wasikatae ndoto kubwa. Wasiridhike na yale wanayoona wanawastahili. Bwana hataki kuona tunafupisha maono, na  wala kutuona tumesimama pembeni mwa maisha, lakini wenye kuwa na  matarajio makuu, kwa furaha na shauku. Hatukuumbwa kwa ajili ya kuota likizo au mwisho wiki, lakini kwa ajili ya kutumiza ndoto za Mungu katika ulimwengu huu. Yeye alituwezesha kuota ndoto kwa ajili ya kukumbatia uzuri wa maisha. Na kazi ya huruma ndiyo kazi zilizo nzuri sana katika maisha. Ikiwa una ndoto ya utukufu wa kweli na siyo ya utukufu wa ulimwengu ambao unakuja na kutoweka bali kuwa na utukufu wa Mungu na ndiyo hiyo njia,  Papa Francisko amesisitiza. Kwa sababu hii matendo ya huduma yanatoa utukufu kwa Mungu zaidi ya kila aina ya kitu chochote.

Je ni wapi  pa kuanzia ili utimize ndoto

Je ni wapi pa kuanzia ili kutimiza ndoto kubwa? Katika kufafanua, swali hili Papa Framcisko amesema ni kutokana na changuzi kubwa. Injili ya siku inalezea wazi hata hilo. Kiukweli wakati wa hukumu ya mwisho Bwana anajikita  juu ya chaguzi zetu. Utafikiria karibu siyo kuhukumu. Yeye anatengenisha kondoo na mbuzi, lakini kuwa wema na wabaya inategemea na sisi. Yeye anachukua matokeo tu ya chaguzi zetu,na kuzipeleka katika mwanga na kuziheshimu. Maisha, kwa maana hiyo ni kipindi cha kuwa na chaguzi za nguvu, uamuzi msingi na wa milele. Chaguzi zisizofaa zinapelekea katika maisha yasiyofaa, na uchaguzi kuu na muafaka zinapelekea mambo makuu katika maisha. Sisi kiukweli tunageuka kuwa kile tunachochagua, katika wema na katika ubaya. Ikiwa tunachagua kuiba tunakuwa wezi, ikiwa tunachagua kufikiria sisi binafsi tunageuka kwa wabinafsi, ikiwa tunachagua kuchukia, tunageuka kuwa wenye hasira, ikiwa tunachagua kupita masaa mbele ya simu za mikono, tunakuwa watumwa wake. Lakini ikiwa tunachagua Mungu tunageuka kila siku kupendwa zaidi na ikiwa tunaamua kupenda tunageuka kuwa wenye furaha. Ndiyo kwa sababu ujue kwamba chaguzi zetu zinategemea na upendo, Yesu anajua kuwa ikiwa tunaishi tumejifunga na kutojali, tunabaki tumegandamana, lakini ikiwa tunajitoa kwa wengine basi tunakuwa huru. Bwana wa maisha anataka tujazwe na maisha na kutupatia siri ya maisha ya kwamba unapokea zaidi ukiwa unatoa.

Vizingiti vinavyojitokeza katika chaguzi

Papa amebai isha kwamba kuna vizingiti ambayo vinajitokeza katika chaguzi. Mara nyingi hofu, kutokuwa na uhakika,na kwanini hakuna jibu. Upendo, lakini unataka upendo zaidi yake, usibaki unapeperushwa na zile kwaini ,  ya maisha ukisubiri kutoka Mbinguni yafike majibu. Hapana, kwani upendo unasukuma kupitia juu ya zile kwanini, kwa ajili ya nani, aidha kutoka  kwanini ninaishi hadi kufikia ninaishi kwa ajili ya nani; kutoka katika swali  la “ kwanini yananitokea  mimi hadi, kufikia nimtendee wema  nani. Papa Francisko ameongeza  “ kwa nani?  Siyo kwa ajili yangu tu, maisha tayari yamejaa chaguzi tunazofanya kwa ajili yetu sisi na kwa ajili ya cheo cha mafunzo yetu, ya marafiki, ya nyumba, na kwa ajili ya kuridhika na upendeleo wetu (hobby) na matakwa yetu. Lakini hayo ni kuhatarisha kukaa  miaka ukijifikiria binafsi bila kuanza kupenda. Mwandishi Manzoni alitoa ushauri mzuri kuwa “ Inatakiwa kufikiria zaidi kutenda wema, badala ya kukaa vizuri na kwa kufanya hivyo hatimaye ingewezekana kukaa vizuri zaidi (I Promessi Sposi, cap. XXXVIII).

Chaguo ni kujitoa, siyo kufungwa, ni kujua jinsi ya kukataa ujuu juu

Papa Francisko amebainisha kwamba lakini hakuna shaka hizo tu ambazo kwa nini zinazosonga chaguzi karimu, badala yake kuna hata vizingiti vingine. Kuna homa ya kutumia, ambayo inalewesha mioyo ya kutaka kuwa na mambo mengi zaidi. Kuna kutamani sana na raha, ambayo inaonekana ndiyo njia pekee ya kutoroka kutoka katika  shida na badala yake ni kuahirisha tu shida. Kuna marekebisho juu ya haki za mtu zinazodaiwa akisahau jukumu la kusaidia. Halafu kuna udanganyifu mkubwa juu ya mapenzi, ambayo yanaonekana kuwa na uzoefu na hisia na kupenda, wakati kupenda ni juu ya zawadi, chaguo na kujitoa. Kuchagua, hasa leo, siyo kufungwa na ufananisho, siyo kutuliza maumivu na njia za utumiaji ambazo hazifanyi uhalisi, ni kujua jinsi ya kukataa na kuonekana kijuu juu tu. Kuchagua maisha ni kupambana dhidi ya utupaji hovyo na mawazo yote ya sasa, ili kuongoza na uwepo kuelekea lengo la Mbingu,yaani kuelekea ndoto za Mungu.

Kuchagua maisha ni kuishi

Papa Francisko amesema “Kuchagua maisha ni kuishi  kwa maana tulizaliwa kuishi, siyo kupata. Hii ilisemwa na kijana kama wewe”, Papa amesema. “Nataka kuishi, sio kufaulu”. Kila siku, chaguzi nyingi huukabili moyo. Papa ameongeza “ Ngoja nikupe njia moja ya mwisho ili ujizoeshe kuchagua vizuri. Ikiwa tunaangalia ndani, tunaona kwamba maswali mawili tofauti mara nyingi huibuka ndani mwetu. Moja ni: ninataka kufanya nini? Ni swali ambalo mara nyingi hudanganya, kwa sababu linasisitiza kuwa jambo muhimu ni kufikiria juu yako mwenyewe na kufurahisha tamaa na misukumo yote inayokuja”. “Lakini swali ambalo Roho Mtakatifu anapendekeza katika moyo ni jingine: siyo hivyo unavyotaka? lakini ni kitu gani kizuri kwako? Hapa kuna chaguo la kila siku, nijisikie kufanya au ni nini kinachofaa kwangu? Kutoka kwa utaftaji huu wa ndani uchaguzi mdogo au uchaguzi wa maisha unaweza kutokea Papa amesisitiza: inategemea sisi. Kwa maana hiyo tuache tumtazame Yesu, tumwombe ujasiri wa kuchagua kile kinachofaa kwetu, kutembea nyuma yake, katika njia  ya maisha ya  upendo na ili kuweza kupata furaha. Kuishi, na siyo kufaidika.

22 November 2020, 16:10