Sehemu ya mashambulizi ya silaha huko Vienna Sehemu ya mashambulizi ya silaha huko Vienna 

Papa Francisko awakumbuka wathirika wanyonge wa ugaidi na chuki!

Papa Francisko mara baada ya Katekesi yake katika lugha mbali mbali amewasalimia watu wote.Amekumbuka janga la virusi na pia matukio ya mashambulizi ya kigaidi kwa walio wanyonge huko Vienna na Nice.Hakusahau kwa namna ya pekee kukumbusha Mtakatifu Karoli Borrome,aliyekuwa Askofu Mkuu wa milano,Italia ameomba kufuata fadhila zake za kinyenyekevu

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko akiwa katika Maktaba ya Jumba la Ktume, tarehe 4 Novemba 2020 akiwasalimu waaamini kwa lugha ya kiitaliano amekumbuka suala la janga la virusi na wale ambao wanateseka na wanakabiliwa na athari za chuki inayojaribu kuathiri ushirikiano wa kindugu kati ya dini. Aidha, amewakumbusha katika liturujia kumbukizi la Mtakatifu Karoli wa Borrome, mchungaji aji ambaye alijikita maisha yake  yote kwa ajili ya wema wa watu. Amewashauri kuiga mfano wa fadhila za Askofu Mkuu huyo wa Milano aliyechagua moto wa kiasikofu wa kumuongoza katika maisha yake 'unyenyekevu'. Tabia hiyo diyo iwafanye waamini kutatufa na kuhudumia Ukweli na Wema amesisitiza. Aidha mawazo yake kama kawaida yamewaendea wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Anawatia moyo wote kujitoa kwa ushuhuda wa kweli katika ukuu wa sala kwenye maisha ya waamini. Sala ni kisima daima cha matumaini na faraja!.

Hata hivyo Papa akikumbuka matukio ya hivi karibu amesema  “Katika siku hizi za kuombea marehemu tumekumbuka na bado tunawakumbuka waathiriwa wanyonge  wa ugaidi ambao kwa ukatili usioelezeka unandelea kuenea Ulaya. Ninafikiria hasa mashambulio mazito ya siku za hivi karibuni huko Nice, mahali pa ibada na ile iliyofanywa juzi katika mitaa ya Vienna ambayo ilisababisha mshtuko na wasiwasi kwa idadi ya watu na kwa wale wanaojali amani na mazungumzo”.

Kufuatia na tendo hili  Papa Francisko amewakabidhi kwa Mungu ubinadamu wote ulioundwa na watu na familiana kwa kusema: “Ninawakabidhi watu waliopotea kwa njia ya kusikitisha kwa huruma ya Mungu na ninaelezea ukaribu wangu wa kiroho na familia zao na kwa wale wote wanaoteseka kwa sasabu shida hizi mbaya ambazo zinajaribu kuathiri ushirikiano wa kindugu kati ya dini na vurugu na chuki”.

 

 

04 November 2020, 15:37