Papa Francisko ashukuru vijana kuandaa tafakari ya Majilio kwa nyayo za Laudato si’

“Wahusishe hata vijana wengine kupitia masafa na majukwa ya mitandao ya kijamii katika maadalizi ya Majilio kuelekea kuzaliwa kwa Bwana na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja kupitia Neno la Mungu na Waraka wa Laudato si’.Amehimiza Papa kwa vijana wa Chuo kikuu cha Venezia na Verona cha Kisalesiano na kuwashukuru huku akiwatia moyo kwa ujumbe kwa njia ya video.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe wake mfupi kwa njia ya video kwa vijana wa Cube Radio", ambayo ni masafa ya Taasisi ya Chuo Kikuu cha Kisalesiano huko Venezia na Verona nchini Italia, tarehe 26 Novemba 2020. Huo ni mpago unaoitwa Majilio Ndoto ya kijani” ambo unaanza Dominika tarehe 29 Novemba hadi mkesha wa Siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana.

Katika ujumbe huo Papa anawashukuru Vijana hao kwa ajili ya kuandaa mchakato wa safari ya Majilio kwa tafakari huku wakiongozwa na Neno la Mungu la kila Dominika na Waraka wa Laudato si’.

Papa anawaalika kuwahusisha hata vijana wengine wengin na masafa mengine ya majukwa ya kidigitali  katika mchakato wa safari ya Majilio ya maandalizi ya siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, kwa kuengeza hata kupitia mitandao yote ya kijamii ya Vatican News, katika Neno la Mungu na kuwaalika kutunza nyumba yetu ya pamoja. Papa amerudia kuwashukuru sana na kwamba anasali kwa ajili yao, pia wao wasisahau kusali kwa ajili yake.

26 November 2020, 16:44