Papa Francisko wakati wa katekesi yake Papa Francisko wakati wa katekesi yake 

Papa Francisko amesali kwa ajili ya waathirika wa vurugu za kivita

Katika salam zake kwa waamini wa mataifa mbali mbali mara baada ya katekesi yake,Papa amekumbuka marehemu wote waliokufa wakati wa vita na ametaja maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyo wambia vijana kwamba uhuru wa kweli siyo kufanya kile ambacho mtu anataka bali maana yake ni kuwa mtu kwa ajili ya wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni katika kumbukumbu ya marehemu waliouwawa wakati wa vita, ambayo imeadhimishwa tarehe 11 Novemba katika nchi nyingi na ndiyo, mawazo ya Papa Fransisko wakati wa kusalimia waamini kwa lugha ya kifaransa mara baada ya katekesi yake ambayo amejikita kuhusu msisitizo wa sala. Katika mtazamo huo amewasihi wote kuwaombea waathiriwa wote wa vurugu duniani na kuwatia moyo ili wotre wawe vyombo vya amani na upatanisho.

Kuwa huru haina maana ya  kufanya kila kitu unachopenda

Maneno amani na upatanisho yamemrudisha  Papa katika kaulimbiu ya uhuru wakati wa kusalimia waamini wa Kipoland. Papa amekumbuka kuwa leo ni Siku ya Kitaifa ya Uhuru inayoadhimishwa katika nchi yao, inayowakumbusha mika ya nyuma  123 ya mgawanyiko na utawala wa kigeni mnamo 1918 kufuatia na Vita vya Kwanza ya Dunia kama Jamhuri ya Pili ya Poland. Papa amesema "wakati tunamshukuru Bwana wa historia kwa zawadi ya uhuru wa kitaifa na wa kibinafsi, ninaijiwa  akilini na kile ambacho Mtakatifu Yohane Paulo II alifundisha vijana kwamba: “Kuwa huru kweli haimaanishi kufanya kila kitu ninachopenda, au kile ninachotaka kufanya". (…) "Kuwa huru kweli kunamaanisha kutumia uhuru wa mtu kwa kile kilicho kizuri na cha kweli. (…) Kuwa huru kweli kunamaanisha kuwa mtu wa dhamiri safi, kuwajibika, na kuwa mtu kwa ajili ya wengine" (Barua kwa vijana,13). Bwana abariki wapoland wote na wape amani na ustawi!" amehitimisha Papa Francisko.

Mtakatifu  Martino askofu wa Tours

Katika salamu kwa Wahispania, pia ametaja muktadha ulioundwa na Covid-19 wakati Papa anataja nyakati za shida ambazo wanadamu wote kwa sasa wanapatia. Na kwa waamini wanaozungumza Kiitaliano, Papa amekumbuka  siku kukuu ya Mtakatifu Martino askofu wa Tours. "Mchungaji huyu mashuhuri wa Kanisa la kale alijitambulisha kwa upendo wake mkuu wa kiinjili kwa maskini na waliotengwa. Mfano wake na uwafundishe kila mtu kuwa na ujasiri zaidi katika imani na ukarimu katika upendo", amehitimisha Papa.

11 November 2020, 15:49