Papa Francisko kiini cha uchumi ni wito,utamaduni na agano kwa ubinadamu!

Papa Francisko akizingumza kwa njia ya video katika tukio la “The Economy of Francesco” amejikita na mambo matatu:Wito wa Assisi kwa maana ya Mtakatifu Francis na wito wao.Pili utamaduni mpya unaopaswa kujengwa katika haki ya kubadili uchumi na hatimaye agano.Papa amekazia kuwa ni kipindi cha vijana wanauchumi,wajasiriamali, wafanyakazi na wakuu wa makampuni,kuthubutu ili kuwezesha mtindo mpya unaojali wote na waliobaguliwa.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko akizungumza kwa njia ya video, kwa washiriki wa Mkutano wa ‘the Economy of Francesco’ ameanza kuwashukuru uwepo wao na kazi ambayo wanaendelea kuifanya, kwa jitihada  ya miezi na ambayo ameitambua kwa ngazi ya tafakari, ubora na uamuzi wa kweli na uwajibikaji ambao wameweza kuuonesha katika kazi hiyo. Papa anasema vijana hawakuweza kuacha wasumbuliwe na chochote kinacho wapa furaha, wasiwasi, hasira na kuwasukuma kubadilisha.  Aidha katika ujumbe wake kwa njia ya video Papa Francisko anakumbusha wazo la kwanza lilivyokuwa ni kukutana Assisi ili kuweza kuongozwa na nyayo za Mtakatifu Francisko. Na msalaba wa Mtakatifu Damiano na nyuso nyingine kama ile ya mkoma, ambaye Bwana alimtuma kukutana naye, alimwita na kumkabidhi utume;  Alimvua na kila muungu uliokuwa unampa kichwa, na mambo mengi yaliyokuwa yanamgandisha na kumfanya ajifungie ndani ya udhaifu wake usemwao tumezoea kufanya hivi.  Papa amesema huo ni udhaifu au huzuni wa kukosa utamu na kutoridhika kama wale wanaoishi kwa ajili yao binafsi na wakati huo akamzawadia uwezo wa kuimba wimbo wa sifa, kilelezo cha furaha, uhuru na kujitoa mwenyewe. Kwa maana hiyo Mkutano huu kwa njia ya mtandao Assisi, Papa Francisko anasema kwa upande wake ni kama wa kufika  japokuwa kwa msukumo wa mchakato ambao wanaalikwa wote kuishi kama wito, kama utamaduni na kama agano.

Wito wa Assisi

Papa Francisko akianza kuchambua kuhusu wito wa Assisi amesema “Francis nenda ukakarabati nyumba yangu maana tazama inaharibika”. Maneno hayo yalimsukuma kijana Francis na kugeuka kuwa  kama wito maalum kwa kila mmoja wetu. Papa Francisko amewashauri ikiwa wanahisi kuitwa, kuhusishwa na kuwa mstari wa mbele wa kawaida  katika kujenga, wao watambue kuitikia tazama mimi hapa, hali hiyo inatoa matumaini. Aidha Papa amesema kuwa anatambua jinsi ambavyo walikubali kwa haraka wito huu kwa sababu wao wanao uwezo wa kuona, kuchambua, na kufanya uzoefu ambao hatuwezi kwenda mbele namna.

Hii inajionesha kwa dhati katika jibu lao, orodha yao na ushiriki wa Mkutano huo ambao umekwenda zaidi ya uwezo. Wao wanaonesha wazi masuala nyeti sana ambayo yanachangamotisha. Mmeyafanya kwa matarajio maalum, kama uchumi ambao ni mantiki yao katika utafiti, mafunzo na kazi. Wao wanatambua jinsi ambavyo kuna hitaji la kuelezea uchumi tofauti, ndiyo hitaji la simulizi ya uchumi tofauti amesisitiza na kuwa  ni kujiweka kwenye matendo ya uwajibikaji kwa maana ya kwamba mfumo wa sasa ulimwenguni hauwezi kustahimili mitazamo kadhaa na unatoa pigo kwa dada yetu dunia ambaye anatendewa vibaya sana, amevuliwa na pamoja na maskini zaidi na waliobaguliwa. Mambo haya yanakwenda pamoja Papa amekazia. Ikiwa wewe unavua Dunia jua kuwa ndani  kuna maskini wengi waliobaguliwa.  Hawa ndiyo wa kwanza kuharibiwa… na hata walio wa kwanza kusahuliwa.  Papa Francisko ametoa angalisho ya kuwa wasikubali kuamini kwamba hii ndiyo hali ya kawaida ambayo iendelee hivyo.

Wao ni zaidi ya kelele ya kijuu juu ambao wanaweza kulala tu na kuleweshwa na wakati. Ikiwa hawataki hili litokee, vijana wanaalikwa  kuwa na uamuzi  wa kweli katika miji yao, vyuo vikuu vyo , katika kazi na katika miji, katika makampuni na harakati , katika ofisi za umma na binafsi na akili, jitihada na kuamini, ili kweza kufikia kiungo na moyo mahali ambao panafanya kazi.  Vijana lazima wanaamini mada na  ndoto zao  kuhusu maisha na mwingiliano mpya kati ya wanadamu lakini unaoibuka pamoja na utamaduni mpya na miji isiyonekana.  Yote hayo Papa amethibitisha yamemsukuma kuwaalika ili wachambue na kutimiza mkataba wa agano. Hali ngumu ya sasa, iliyotokana na janga la covid imefanya kuona kwa mara nyingine tena haja ya kuwa na uwajibikaji,  kuwa na dhamiri kwa wadau wote wa kijamii, sisi sote, kati ya wale walio  na nafasi ya kwanza. Matokeo ya matendo  yetu na maamuzi yatagusa kwa namna moja binafsi na kwa maana hiyo vijana hawawezi kubaki nje ya maeneo  na siyo tu kwa wakati  ujao bali hata wakati uliopo. Wao hawawezi kwenda nje ya mahali panapozaliwa wakati uliopo na wakati ujao. Au wawe wahusika  au historia hii itawapitia juu yao

Utamaduni mpya

Kuna haja ya mabadiliko,Papa anasema, akifafanua fungu la pili kuhudu utamaduni kuwa tunataka mabadiliko, tunatafuta badiliko. Tatizo linazaliwa ikiwa tunagundua kuwa matatizo mengi yaliyopo yanakuta kuwa hatuna majibu ya kutosha na jumuishi. Badala yake ni kujisikia kumegeka vipande vya tathimini na vipimo  ambavyo vinaishia kuzuia kila uwezekano wa kuleta suluhisho. Kichini chini unakosekana utamaduni ulio wa  lazima ambao unawezesha na kutoa chachu ya ufunguzi wa maono tofauti, muhimu katika aina ya mawazo , kutoa mtindo mmoja wa kisiasa, kwenda mtindo mwingine wa kufikiri será,  mpango wa elimu, aidha  kunakosekana tofauti ambayo haishi kujifungia katika mantiki moja inayotawala. Ikiwa kuna haja ya kupata majibu, ni muhimu kufanya yakue  makundi yanayoongoza na yenye uwezo wa kufanya kazi katika utamaduni na kuanzisha michakato… Papa Franciso amehimiza wasisahau neno hilo “ kuanzisha michakato,, kugundua  michato, kupanua maoni, kuunda ushiriki… Kila jitihada, ya kutunza, na kuborsha nyumba yetu ya pamoja , ikiwa tunataka kuwa na maana ya juhudi  ambayo inatakiwa kubadili mitindo ya maisha, namna ya kuzalisiaha na kutumia miundo ya thahibiti ya uwezo ambao leo hii unasimiamia jamii. Bila kufanya hivyo hawatafanya lolote.

Kuna haja ya makundi yanayoongoza jumuiya na taasisi zinazoweza kubeba matatizo bila kubaki wafungwa wa kutosheka na kwa namna ya kuwekwa chini na changamoto na matukio yake  ni kuzaliwa kwa aina za kiitikadi na ambazo zinaishia kuhalalisha na kugandasha kila aina ya matendo mbele ya ukosefu wa haki. Papa amekumbusha jinis ambavyo Papa Mstaafu Benedikto XVI alivyosema “ haitegemei sana uhaba wa nyenzo, lakini badala ya uhaba wa rasilimali za kijamii, ambayo muhimu zaidi ni ya asili ya kitaasisi” . Ikiwa utaweza kutatua hili, utakuwa na njia wazi kwa siku zijazo. Papa FRancisko kwa kusisitiza “Narudia mawazo ya Baba Mtakatifu Benedikto: njaa “haitegemei sana uhaba wa nyenzo, lakini badala ya uhaba wa rasilimali za kijamii, ambazo muhimu zaidi ni ya asili ya taasisi”.

Agano la Assisi

Hatuwezi kuruhusu kuendelea kuacha badhi ya masuala, amesisitiza Papa Francisko katika kufafanua mambo matatu muhimu. Kazi hiyo kubwa ya ukarimu kwa mantiki ya utamaduni, katika mafunzo ya elimu na katika utafiti wa kisayansi bila kupoteza mitindo ya kiakili au kiitikadi ambayo ni kisiwa na vile vile ,ambacho kinatutengenisha na maisha,  kutoka katika matatizo ya kweli ya watu. Papa amesema hiki ni kipindi sasa cha vijana wanauchumi, wajasiriamali, wafanyakazi na wakuu wa makampuni, ni kipindi cha kuthubutu, kujihatarisha ili kuwezesha na kutoa chachu za mitindo mipya  ya maendeleo, ya uendelezwaji ambao ni kwa ajili ya watu na  walioaguliwa hasa.( kati ya hawa hata dada dunia). Ni muhimu kuacha  kutawaliwa na kile kiitwacho kazi au kufanya kazi kwa ajili ya kugeuka kuwa mstari wa mbele wa maisha kama kiungo kizima cha kijamii. Siyo jambo la kutaja tu, bali wapo kweli maskini na waliobaguliwa ,anasema Papa, uwepo wao usiwe ni katika kutaja wala kiufundi au kazi. Ni kipindi cha kugeuka kuwa mstari wa mbele kwa ajili yao  na maisha yao yote,kwa ajili ya watu na hakuna lolote bila kuwa na watu. Tusifikirie kwa ajili yao bali tufikirie pamoja nao, Papa amekazia kuwa  wafikirie urithi wa wa watu.

Kutokana na watu maskini amesema wajifunze  mitindoa ya  kiuchumi ambayo itaweza kuwa na faida kwa wote, kwa sababu mfumo na maamuzi yatakuwa ya kweli  ya maendeleo fungamani  kama inavyo fafanuliwa na Mafundisho jamii ya Kanisa. Siasa haipaswi kuwa chini ya uchumi, wala uchumi kuendeshwa na msukumo wa ufanisi wa dhana ya teknokrazia.  Leo hii kwa kuzingatia ustawi wa pamoja, kuna haja ya haraka ya siasa na uchumi kuwa na muafaka kamili kwa ajili ya kulinda uhai  hasa maisha ya mwanadamu. Bila kiini hiki na mwelekeo huo Papa amesema tutabaki wafungwa wa kuendelea katika mwendendo wa ubaguzi, vurugu na kujisikia. Kila mpango unaofanyiwa kazi ili kuongeza uzalisha hauna sababu nyingine zaidi ya kuwa katika huduma ya mtu. Kazi yake ni kupunguza ukosefu wa usawa,  uhalifu, kutoa uru kutoka katika utumwa (…) Haitoshi kukuza utajiri wa pamoja kwa sababu  lazima uwe na usawa, haitoshi kuhamasisha ufundi kwa sababu ardhi iwe ya nyumba ya pamoja… lakini hiyo pia bado inatosha kabisa.

21 November 2020, 17:30