Papa amekumbuka majeraha ya tetemeko la ardhi miaka 40 iliyopita!

Papa Francisko katika salam zake mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana amezungumzia tukio la miaka 40 iliyopita tangu kutokea tetemeko la ardhi mnamo tarehe 23 Novemba 1980 katika Mkoa wa Campania na Basilicata nchini Italia na amewaalika wote kuwa na mshikamano na familia zilizo kwenye matatizo kiuchumi katika wakati huu ambapo wengi wamepoteza kazi.

Sr Angela Rwezaula - Vatican

Miaka 40 iliyopita janga kubwa la tetemeko la ardhi lilitokea katika eneo la Irpinia, ambalo lilisababisha vifo vingi na uharibifu mkubwa ambapo Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 22 Novemba 2020  mawazo yake yamewaendea watu wa Mkoa wa Campania na  Basilicata nchini Italia. Tukio hilo la kushangaza, ambalo hata majeraha bado hata leo hii hayajapona kabisa,na ambayo yalionesha laki ukarimu na mshikamano wa Waitaliano. Uthibitisho huo ni ushuhuda kwa zile nchi ambazo zilikumbwa na tetemeko la ardhi na zile za kaskazini na kituo ambacho kiungo chake bado kipo. Mipango hii imewezeshwa kwa njia ngumu ya ukarabati na zaidi udugu kati ya jamuiya mahalia za za peninsula.

Ilikuwa tarehe 23 Novemba 1980

Mtetemeko wa ardhi uliokea siku ya Jumapili  tarehe 23 Novemba 1980, liligonga eneo la zaidi ya kilomita 17,000 kusini mwa Italia, na kugusa juu ya majimbo yote ya Avellino, Salerno na Potenza na kuangamiza miji mingine chini na cha kushangaza idadi ya watu wapatao 3,000 walikufa, zaidi ya 8,000 walijeruhiwa na  watu 280,000 walihama makazi yao.

Mawazo ya Papa kwa familia wenye matatizo kwa sababu ya ukosefu wa kazi

Vile vile Papa Francisko katika salam zake amekumbuka watu wa Roma, mahujaji licha ya matatizo ya sasa ya janga lakini daima wakifuata sheria zilizo wekwa hadi kufika katika uwanja wa Mtakatifu Petro ili kushiriki sala ya Malaika wa Bwana. Mawazo ya Papa  pia yamewaendea familia nyingi ambazo kipindi hiki kigumu wanaishi katika matatizo. Papa amesema “Juu ya hali  hii fikirieni familia nyingi ambazo zina shida kwa sasa, kwa sababu hawana kazi, wamepoteza kazi zao, wana watoto mmoja au wawili, na wakati mwingine,wakiwa na aibu kidogo ya kuomba msaada, pa hawawaruhusu watu kujua hayo. Lakini ni ninyi mnapaswa kwenda na kutazama penye uhitaji. Mahali alipo Yesu, ni yeye anayehitaji. Fanya hivyo!”

22 November 2020, 18:18