2015.11.28 Misa ya Papa Fracisko kwa ajili ya wafiadini wa Uganda katika Mabadhabahu katoliki  ya Namugongo, Kampala Uganda. 2015.11.28 Misa ya Papa Fracisko kwa ajili ya wafiadini wa Uganda katika Mabadhabahu katoliki ya Namugongo, Kampala Uganda. 

Ni mwaka wa 5 tangu Papa atembelee nchini Uganda na nchi nyingine za karibu!

Francisko Papa Francisko alifanya ziara yake ya kitume nchini Uganda,Kenya na Afrika ya Kati kunako mwezi Novemba 2015.Ni ziara iliyowajaza moyo wa matumaini na furaha kutokana hotuba zake na wingi wa watu waliofika kumlaki na kumsikiliza.Lakini katika nchi hizo hali halisi ya kijamii bado inaendelea kuwa na vikwazo mbali mbali vya kijamii na kisiasa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika harakati za uchaguzi mkuu nchini Uganda unaotarajiwa hivi karibuni  na ambao kwa sasa unaonesha hali halisi isiyo kuwa na utulivu ni vema kukumbuka maneno yake Papa Francisko, wakati wa ziara yake ya kitume nchini humo mwezi Novemba 2015.  Ikiwa ni mwaka 5 tangu afanya ziara hiyo na ambayo inatukumbusha zaidi juu ya maneno ambayo wakati ule aliwahimiza hasa  kuwataka wawasha moto mpya wa mshikamano wa kitaifa kwa vitendo na siyo kwa maneno, moto wanaopaswa kuudumisha hata wakati wa uchaguzi wa kisiasa.  Papa aliwahimiza kuwa na umoja, kama yeye alivyoonyesha mshikamano wa uekumeni, kwa kukukutana na watu wa madhehebu mengine hata yale yasiyokuwa ya Kikristo.

Kwa kutembelea Nyumba ya Upendo ya Nalukolongo, jijini Kampala, tarehe 28 Novemba 2015, Papa Francesco alihutubia kwa kusisitizia matendo hayo ya upendo kama vile yupo Yesu. Papa alisema: “Leo, kutoka katika nyumba hii, ningependa kutoa wito kwa parokia zote na jamuiya zilizopo nchini Uganda na katika nchi zote barani Afrika kutowasahau maskini, na kusahau maskini! Injili inatuhitaji twende kwenye maeneo ya jamuiya na kumtembelea Kristo katika mateso na kwa wale wanaohitaji. Bwana anatuambia, kwa maneno yasiyo na shaka, kwamba atatuhukumu juu ya hili! Inasikitisha wakati jamuiya zetu zinaruhusu wazee kutupwa au kusahauliwa! Ni mbaya  sana wakati vijana wananyonywa na utumwa wa sasa wa usafirishaji haramu wa binadamu! Ikiwa tunaangalia kwa uangalifu ulimwengu unaotuzunguka, inaonekana kwamba ubinafsi na kutokujali kumeenea katika maeneo mengi. Ndugu kaka na dada zetu ni wangapi waathiriwa wa utamaduni wa leo wa kutupa, ambao unaleta dharau hasa kwa watoto ambao hawajazaliwa, vijana na wazee?.

Baadaye Papa Francisko, akikumbuka jinsi Bwana alivyokuja si kutumikiwa, lakini kuhudumia, alitoa mwaliko wa nguvu kwa Wakristo kuwa mashuhuda madhubuti wa upendo wa Yesu, kwa vitendo na , sio kutazama. “Kama Wakristo, hatuwezi tu kusimama karibu, kuangalia kinachotokea, na kutofanya chochote. Kitu kinapaswa kubadilika! Familia zetu lazima ziwe ishara dhahiri zaidi za upendo wa subira na huruma ya Mungu, sio tu kwa watoto wetu na wazee wetu, bali kwa wale wote ambao wanahitaji”. Parokia zetu hazipaswi kufunga milango na masikio yao kwa kilio cha maskini. Hii ndiyo njia kuu ya ufuasi wa Kikristo. Hivi ndivyo tunavyomshuhudia Bwana, ambaye hakuja kutumikiwa, bali kutumikia. Kwa hivyo tunaonyesha kuwa watu ni muhimu kuliko vitu na kwamba sisi ni muhimu kuliko vitu  tulivyo navyo zaidi. Kabla ya Francisko kwenda Uganda alitanguliwa na , Papa Paulo VI kunako  1969 na Papa Yohane  Paulo II,  kunako 1993. Na ikumbukwe  Papa alitembelea miji miwili wa Entebbe na Kampala. Hotuba sita zilitolewa, Misa ya kukumbukwa ni ilie iliyoadhimishwa katika madhabahu ya Mashahidi wa Uganda Namugongo  tarehe  28 Novemba kwa kuudhuriwa mamiaelfu ya waamini katoliki na wasio katoliki.

25 November 2020, 16:17