2019.08.10 safari ya Meli ya Victoria (Kopi ya ramani) 2019.08.10 safari ya Meli ya Victoria (Kopi ya ramani) 

Miaka 500 tangu maadhimisho ya kwanza ya Misa nchini Chile

Katika ujumbe ulioandikwa kwa mkono wake na kutangazwa Dominika tarehe 8 Novemba,katika maadhimisho ya Ekaristi,kwa njia ya mtandao Jimbo la Mkoa wa Magellan,Papa Francisko anathibitisha kwa Askofu wa Punta Arenas kuwa tarehe 11 Novemba ni tarehe ya kihistoria,lakini si kwa ajili ya jimbo hilo tu bali kwa Kanisa zima katoliki la Nchi za Amerika ya Kusini.

Na Sr. Angela- Vatican

Kwa mujibu wa Tovuti ya Baraza la Maakofu nchini Chile wametangaza Ujumbe wa Papa Francisko aliouandikwa kwa mkono wake kufuatia na maadhimisho ya Miaka 500 tangu kuadhimishwa Misa Takatifu ya kwanza katika eneo la Chile. Katika ujumbe huo Papa amesema  kwamba “Bwana alipendelea kuingia kupitia katika mlango mfinyu wa Magellan kwa Askofu wa Punta Arenas amesema tarehe 11 Novemba ni tarehe ya kihistoria, si tu kwa ajili ya jimbo lakini kwa Kanisa zima katoliki la Nchi ya Amerika ya Kusini. Hii kiukweli ilikuwa ni tarehe hiyo mwaka 1520 ambapo Padre Pedro de Valderramae, kwa dhati aliadhimisha Misa Takatifu katika sehemu hiyo ya ulimwengu mpya uliofikiwa na wafanyakazi wakiwa katika  msafara wa Hernando de Magallanes (Ferdinando Magellano) wakati wa ziara yake ya  kwanza ulimwenguni katika historia ya ubinadamu

Miaka 500 iliyopita, ziara ya kwanza ya ulimwengu

Ni wakati muhimu na usiofutika wa kihistoria ambao Kanisa la Chile linaadhimisha kwa shukrani kubwa kwa Mungu na na mpaji  kama Papa Francisko mwenyewe anavyobainisha  katika barua yake mwenyewe iliyochapishwa na kutangazwa  Jumapili tarehe 8 Novemba 2020. Ujumbe huo ulisomwa mwanzoni mwa kuanza maadhimish ya misa iliyosambazwa kupitia mtandaoni kwa Jimbo nzima la Mkoa wa Magellan katika kumbu kumbu  na “chanzo cha kutia moyo na furaha, sio tu kwa jimbo la  Punta Arenas, bali kwa Chile yote, anasisitiza Papa Francisko. Hii ni kutokana na kwamba miaka 500 iliyopita, tarehe 11 Novemba 1520 Upendo mkuu ulipenda kuwa juu ya mlima wa Msalaba karibu na Magellan, ambapo Padre Pedro de Valderrama, aliyekuwa mchungaji wa msafara wa Hernando de Magallanes, aliinua kwa mara ya kwanza katika nchi hizo dhabihu ya Misa Takatifu.

Mungu aliingia kutoka Kusini

Akirejea  katika maana ya Ekaristi ambayo kwayo, kama Mtaguso wa  Pili wa Vatican unavyokumbusha, amesema “Neema inapita kuelekea kwetu ambayo inatufanya kuwa watakatifu, Papa anaongeza: Kwa sababu hiyo, katika karne hii ya tano tunaweza kusema ni sawa na kama kauli mbiu ya Jimbo la  Punta Arenas isemayo “Mungu aliingia kutoka Kusini”, na kwa maana hiyo Misa ya kwanza iliadhimisha kwa imani, katika unyenyekevu wa safari kwenye eneo ambalo wakati huo halikuwa likijulikana na kuleta Kanisa ambalo linaendelea kwenda kuhiji katika taifa hilo mpendwa”.

Hakuna kinachozui kutoa shukrani 

Papa  anakiri kwamba, hata ikiwa sherehe hiyo haiwezi kufanywa na vitendo vya kuwa pamoja katika  liturujia kwa sababu ya janga  lakini, “hakuna kizuizi kinachoweza kunyamazisha shukrani inayotoka mioyoni mwa  waamini wote” wa Kanisa la Chile ambao wanapyaisha kumjua Bwana  ambaye ni mwenzao  anayesafiri nao. Kutokana na hilo Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki na wakili wa Kristo amewatia moyo kuishi maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi, kwa roho ya kuabudu na kumshukuru Bwana, kwa sababu amesema “ni kwa ajili yetu kanuni ya maisha mapya na umoja, ambayo hutusukuma kukua katika huduma ya kindugu kwa masikini na wafanyakazi wa jamii yetu”. Mawazo na uaminifu ya Papa  Fransisko kwa kuhitimisha ulikuwa ni kumgeukia  Mama yetu wa Karmeli ili atufundishe kumtumainia Bwana na kufanya mapenzi yake, kwa upendo na haki, kutoa ushuhuda kwa ulimwengu wa furaha ya Injili”.

09 November 2020, 16:49