Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana. Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana.  

Mwaliko wa Papa ili kupenda Kanisa kwa sababu ni Nyumba Yetu.

Maneno yale ya Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana kuhusu kulipenda Kanisa.

VATICAN NEWS

 Papa Francisko wakati wa kuhitimisha Katekesi yake ya Jumatano tarehe 18 Novemba 2020,alitoa mwaliko kwamba "Ninawashauri kupenda Kanisa la Bwana" siku ambayo ilikuwa inaadhimishwa kutolewa kwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican na lile la Mtakatifu Paulo, lililoko Ostiense Roma. "Siku kuu hii ambayo inapendekeza kwa mwanga wenye maana katika Kanisa, nyumba Takatifu na mahali ambamo waamini wanakusanyika, iweze kutoa chachu kwetu sisi  ule utambuzi kuwa kila mmoja anaitwa kuwa hekalu la Mungu aliye hai, kushirikiana kwa ukarimu na shauku katika ujenzi wa Nyumba ya Bwana, makao ya Aliye juu katikati yetu” alisema Papa.  Katika kumnukuu maneno Papa Francisko, Dk. Sergio Centofanti Makamu Mkurugenzi wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican amejikita kutazama suala la msisitizo huo wa Papa Francisko wa amara kwa mara. Katika tafakari hiyo anasema “Kupenda Kanisa ndiyo kile ambacho yule anayeamini, yule ambaye anazingatia moyoni kama familia,na familia ya Mungu.

Katika Katekesi ya Papa Francisko mnamo tarehe 29 Mei 2013, alikumbuka kuwa “mpango wa Mungu ni kufanya sisi sote kuwa familia moja ya watoto wake ambamo kila mmoja anahisi kuwa karibu na anahisi kupendwa na Yeye”.  Kanisa siyo aina ya shirika moja,  bali ni kazi ya Mungu ambayo inazaliwa juu ya Msalaba kutoka ubavuni wa Yesu ambamo ni wakati wa kutoka damu na maji, ishara  za Sakramenti ya Ekaristi na Ubatizo na kuoneshwa wazi wakati wa pentekoste katika zawadi hiyo ya Roho Mtakatifu ambayo iliujaza moyo wa Mitume na kuwasukuma watoke nje na kuanza safari ya kutangaza Injili na kueneza upendo wa Mungu”.

Aidha “anayesema Kristo ndiyo na  Kanisa hapana, Papa anajibu kuwa ni Kanisa ambalo limleta Kristo na kumleta Mungu. Kanisa ni familia kubwa ya watoto wa Mungu. Papa alisema katika mantiki za kibadamu na ambazo zinawaunda Wachungaji na waamini kuna makosa na hata kutokuwa wakimilifu na dhambi, kwa sababu hata Papa anazo nyingi lakini uzuri ni kwamba tunapogundua kuwa wadhambi tunaomba msamaha na huruma kwa Mungu ambaye daima anasamehe na kuhurumia. Kanisa linatupatia maisha mapya na kutuelekeza kwake Kristo. Kanisa ni mama na hivyo lazima kulilinda, hata tunapoona kuna mikunyato wakati mwingine, ya dhambi ni  lazima kuchangia ili liweze kuwa daima zuri na angavu na ili liweze kuwa shuhuda wa Upendo wa Mungu ulimwenguni. Alisema hayo  katika ujumbe wa Siku ya Maombi kwa ajili ya miito tarehe, 31 Januari 2019. Papa anaalika kupenda Kanisa na kulinda familia hata wazazi  kaka na dada au wale wenye matatizo na wanaokosea. Alitoa mfano wa upendo wa Kanisa akimtaja Mtakatifu Pio ambaye alikuwa anapenda Kanisa na matatizo yake ambayo mara nyingi yanawakumba wadhambi wengi. Kanisa ni takatifu na mchumba wa Kristo , lakini sisi ni watoto wa Kanisa ambalo tu wadhambi.

Papa Francsiko alitoa onyo kwa wale ambao mara nyingi maisha yao ni kuwahumumu wengine na kumbe ni lazima kuepuka udanyaifu wa ibilisi ambaye hapendi kanisa bali anatsfuta kuligawa. Bila upendo ni tabia ya ibilisi (Hotuba kwa wanahija wa Jimbo la Benevento, 20 Februari 2019). Ibilisi anatenda kwa ajili ya kuharibu umoja wa Familia. Papa anasema mara nyingi kuwa shetani anapenda kugawanya ndugu, anataka kugawanya Kanisa kwa kuwatengenisha na Mungu  yeye mara nyingi yupo ndani na nje. Ni wa kuharibu au moto wa pembeni ulio hatari zaidi. Ubaya ambao unatukumba ndani (Hotuba kwa Sekretarieti ya Vatican 22 Desemba  2014).

Ibilisi ni mbaya kwani ni vita vichafu na anajua kuchezea udhaifu wetu ( Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta tareh 12 Septemba 2016). Ibilisi anatafuta kutengeneza vita vya ndani,yaani  aina ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kiroho. Vita ambavyo  havifanyiki kwa silaha, kama tunavyotambua, alisema Papa bali vita kwa njia ya ulimi (Mahubiri kwa Vikosi vya Ulinzi na usalama, Vatican 28, Septemba 2013). Vita hivyo, shutumu za chuki na ulaghai, alithibitisha Papa vinaweza kujibiwa kwa njia ya sala na upendo tu, kwani ni  kusali kwa ajili ya Kanisa na kulipenda kwa sababu Yesu Kristo na Kanisa ni  kitu kimoja tu (Katekesi 28 Mei 2013).

19 November 2020, 15:43