Kwa sasa Mashirika mapya ya kidini yataridhiwa na Vatican. Kwa sasa Mashirika mapya ya kidini yataridhiwa na Vatican.  

Itakuwa ni Vatican itakayoridhia taasisi mpya za kidini

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 4 Novembre 2020 katika barua yake binafsi ya Motu Proprio “Authenticum charismatis” anabadilisha kanuni ya Sheria ya Kanisa ambayo inafanya kudhibitiwa,kwa sheria,zamani ilikuwa ya ushauri tu na kwa mujibu wa maoni ya Kitume sasa utambuzi wa jamuiya yoyote mpya ya maisha ya wakfu katika muktadha wa jimbo itaridhiwa na Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila karama, hata ikiwa imechanua katika mazingira maalum ya eneo, katika asili yake ina tabia ya ulimwengu na kama vile Papa anavyothibitisha katika Waraka wake kwa watu waliowekwa wakfu ya 2014, kuwa “kila uzoefu wa maisha ya wakfu kama zawadi kwa Kanisa, sio ukweli iliyotengwa au wa pembeni, lakini inamilikiwa sana, na uko katika kitovu cha Kanisa kama sehemu ya uamuzi wa utume wake”. Huu ndio upeo ambao unapelekea uamuzi wa Papa Fransisko kubadilisha Sheria ya Kanuni n. 579, iliyoidhinishwa na Barua yake binafsi ya Kitume “Motu Proprio” “Authenticum charismatis”, ambayo imetangazwa tarehe 4 Novemba 2020. Kimsingi, pamoja na kumwacha askofu binafsi wa jimbo mwenye uwezo katika kuongoza na kuweka taasisi ya maisha ya wakfu kwa kanuni rasmi katika eneo lake, kanuni mpya ya sasa inahitaji kwamba uchaguzi wa askofu ufanywe chini ya kuidhinishwa na makao makuu ya Kitume” wakati hapo awali katika kifungu cha kanuni ya 579 ilisomeka  kwamba “mradi tu Kitengo cha Kitume kimetaarifiwa”.

Kuepuka idhini zisizo na busara

Ishara hii dhahiri ya ukweli wa karama anasema Papa Francisko katika Barua yake ya Motu proprio,  kuwa ni kanisa lake, uwezo wake wa kujumuika kwa usawa katika maisha ya Watu Watakatifu wa Mungu kwa faida ya wote na mang’amuzi juu ya Kanisa na uaminifu wa karama ni jukumu la kikanisa la Wachungaji wa Makanisa mahalia”. Wakati huo huo, Papa Francisko  anasisitiza, akitoa mfano wa agizo kamili la “Perfectae caritatis” yaani upendo kamili kuwa  ni muhimu kuepusha kuibuka kwa taasisi ambazo hazina busara na maana au kukosa taasisi za nguvu ya kutosha”.

Utambuzi na hukumu

Kwa njia  hiyo Papa Francisko, anaendelea, kusema Kitengo cha Kitume kinawajibika kuwasindikiza Wachungaji katika mchakato wa kufanya mang’amuzi ambayo upelekea kuwa na utumbuzi wa kikanisa kwa Taasisi mpya au Jumuiya mpya yenye haki kijimbo na anakumbusha kwamba Wosia kitume wa maisha ya Wakfu  unasisitiza kwamba nguvu ya Taasisi mpya na vyama vya kitume, lazima ichunguzwe na mamlaka ya Kanisa, ambayo inawajibika kwa uchunguzi unaofaa ili kupima ukweli wa lengo la kuhamasisha na kuzuia kuzidisha kupindukia kwa taasisi kama hizo na hatari inayoweza kusababisha kugawanyika vibaya katika vikundi vidogo mno”. Anahitimisha Papa kuwa Taasisi mpya za maisha ya wakfu na Vyama vya kitume lazima vitambuliwe rasmi na Kitengo cha Kitume Vatican, ambacho peke yake kina hukumu ya mwisho.

04 November 2020, 16:39