Papa Francisko:katika kipindi hiki kigumu cha Majilio kiwe tumaini kubwa
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.
Matumaini katika ukweli ambayo yanaokoa, katika mwanga wa nguvu zaidi kwenye giza, ni safari ambayo inabadili moyo. Yote hayo ndiyo majilio. Amesema hayo Papa Francisko mara baada ya Katekesi yake leo hii, tarehe 25 Novemba 2020 akiwakumbusha Kanisa lote ulimwenguni umuhimu wa maandalizi ya liturujia inayokaribia ya Majilio. Katika kipindi kigumu kwa walio wengi, tujitahidi kugundua matumaini makuu na furaha ambayo tulipewa kwa njia ya kuja Mwana wa Mungu ulimwenguni. Amesema hayo Papa akiwageukia waamini kwa lugha ya kifaransa huku akisisitiza pia juu ya sikukuu iliyopotia ya Kristo Mfalme n wa ulimwengu na kwamba alituokoa dhidi ya nguvu ya giza na kutuingiza katika ufalme wake ili kuwa mashuhuda waaminifu na ukweli unaookoa.
Papa Francisko akiwasalimia waamini kwa lugha ya Kiitaliano, vile vile amesema Siku kuu ya Kristo Mfalme ambayo tumesheherekea Jumapili, ilihitimisha mwaka wa kiliturujia, na iwezeshe kuwa na utambuzi kwamba Kristo alitukomboa kutoka katika nguvu za giza, ili kutuingiza katika ufalme wa Mung, na kutufanya sisi kuwa shuhuda amini katika ukweli wa ukombozi. Mawazo yake yamewaendea kama kawaida wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Kristo ambaye anatawal kutoka Msalabani, awape nguvu wote wakati wa majaribu na mateso kwa kufungua ndani mwao mioyo ya matumaini. Papa Francisko amesalimiwa waamini wanaozungumza lugha ya kiingereza: " wakati tunajiandaa kuingia katika safari ya kipindi cha Majilio mwanga wa Kristo uweze kuonesha njia zetu na kuondoa giza la mioyo yetu". Kwa familia zote amewatakia furaha na amani ya Kristo Yesu.