Papa:Tusali kwa ajili ya wanawake ili waweze kuwa na nafasi za uwajibikaji katika Kanisa!

Umetangazwa ujumbe kwa njia ya videoo wa nia ya maombi ya Papa Francisko kwa mwezi Oktoba 2020 ambapi ni kwa ajili ya kuombeana wanawake ili waweza kuwa na nafasi ya kuwajibika katika Kanisa.Leo hii bado kuna haja ya kupanua nafasi za uwepo wa wanawake zaidi katika Kanisa,anasema Papa.Ni Mtandao wa Utume wa Sala Kimataifa ambao unaeneza kila mwezi nia za Papa.

Na Sr, Angela Rwezaula- Vatican

Katika nia za maombi ya mwezi Oktoba 2020, Papa  Francisko anatamani ushiriki mkubwa wa wanawake walei katika nafasi za uwajibikaji katika Kanisa na hukabidhi shauku yake hiyo katika maombi ya Wakatoliki wote ulimwenguni kwa mwezi wa huu. Ushiriki ambao mizizi yake siyo katika madai yanayohusiana na nyakati, lakini katika sakramenti yenyewe ya Ubatizo kwa sababu hapo ndipo wahusika wakuu wa walei na kwa maana hiyo pia kwa wanawake katika maisha ya Kanisa na katika tangazo la Injili. “Hakuna mtu aliyebatizwa kama kasisi au askofu. Sote tumebatizwa kama watu walei. Walei wote kike na kiume wako mstari wa mbele wa Kanisa”, amethibitisha Papa.

Kati ya walei, hata hivyo, bado kuna nafasi ndogo sana kwa wanawake. Katika ujumbe kwa njia ya video, Papa Francisko anaendelea kusema “Leo hii bado kuna haja ya kupanua nafasi za uwepo wa wanawake zaidi katika Kanisa”. Na uwepo wa walei, kiukweli, ina maana ya kusisitiza hali ya kike, kwa sababu kiujumla wanawake wamewekwa kando. Kwa maana hiyo Papa hasemi juu ya uwepo wao tu kwa sababu anabainisha: “ni lazima tuhamasishe  ujumuishwaji wa wanawake katika maeneo ambayo maamuzi muhimu hufanywa”.

Mada inayojirudia mara kwa mara kwa upande wa  Papa Francisko ni ile ya mapambano dhidi ya ukiritimba, ambayo hutenga watu mbali na ambayo huharibu uso wa Kanisa. Papa, akionyesha nia ya sala ya mwezi Oktoba, anasema: “Tuombe ili kwamba, katika fadhila ya Ubatizo, waamini walei, hasa wanawake, waweze kushiriki zaidi katika taasisi za uwajibikaji wa Kanisa, bila kuangukia katika ukasisi ambayo inabatilisha karama ya walei” .

Kwa mtazamo wa Papa Francisko juu ya wanawake, kwa hakika Papa Francisko ametimiza ishara nyingi ambazo zinahamasisha shauku ya kuongeza uzito wa wanawake katika Kanisa na, tangu mwanzo wa upapa wake, amewaita hata wanawake zaidi na zaidi kushika nyadhifa za uwajibikaji. Maandiko  ya Mtandao kwa ajili ya nia za  Maombi kimataifa  ya Papa  mara zote yanambatana na video kwa mfano kunako   mwaka 2016 Papa Francisko  aliinua siku ya Mtakatifu Maria Magdalene kwa kiwango cha sikukuu ya kiliturujia, iliyofafanuliwa hata katika dibaji mpya ya misale ya  Misa kama 'mtume wa mitume': alifanya hivyo kwa kusisitiza umuhimu wa mwanamke huyo, wa kwanza kuona uso wa Yule aliyefufuka kati ya wafu, wa kwanza ambaye Yesu anamwita kwa jina, wa kwanza kupokea kutoka kwa Yesu ujumbe wa kutangaza Ufufuo wake

Kwa mujibu wa Padre Frédéric Fornos, mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa kimataifa, ananukuu kifungu cha Papa  Francisko katika Evangelii Gaudium: yaani Injili ya furaha  “Madai ya haki halali za wanawake, huanzia na imani thabiti kwamba wanaume na wanawake wana hadhi sawa, na huleta maswali mazito kwa Kanisa kwamba kuna changamoto na hiyo haiwezi kukwepa kijuujuu”. Na tena akimaanisha kile ambacho Papa Fransisko anachoandika katika Querida Amazonia, Padre Fornos amesema katika maandishi anasema  kwamba, “wanawake wengi, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, wanafanya Kanisa liwe hai katika sehemu mbali mbali za ulimwengu, kwa kujitoa, kwa kupendeza na imani ya bidii. Kwa maana hiyo ni muhimu kwamba washiriki kila wakati,  zaidi katika vyombo vyake vya kufanya uamuzi. Hii inahitaji mabadiliko makubwa ya fikra, inahitaji uongofu wetu, ambao unadokeza maombi”.

09 October 2020, 14:38