Papa na Utume:Bila kuwa Naye hatuwezi kufanya lolote! Papa na Utume:Bila kuwa Naye hatuwezi kufanya lolote! 

Papa na Utume:Bila Yesu hatuwezi kufanya lolote!

Katika Mwezi wa Kimisionari kimetangazwa kitabu kipya kinachohusu mahojiano Papa Francisko na Gianni Valente,kutoka Shirika la Habari za Kimisonari Fides.Papa anatukumbusha kwamba Kanisa labda liwe tangazo au siyo Kanisa.Kitabu hicho kimechapishwa na LEV na Paulinus.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

‘Furaha ya Injili’ inajaza mioyo na maisha ya wale wanaokutana na Yesu. Ndivyo unaanza Wosia wa Kitume wa Evangelii gaudium, Yaani Injili ya Furaha iliyotangazwa na Papa Francisko mwezi Novemba 2013, miezi nane baada ya kuchaguliwa kuwa Askofu wa Roma na Mfuasi wa Mtakatifu Petro. Hati hiyo inaonesha programu ya kipapa ambayo inayo mwalika kila mtu kurekebisha kila kitendo, kuwa na tafakari ya kina na mpango wa Kanisa juu ya kutangaza Injili katika ulimwengu wa leo. Karibu miaka sita baadaye, katika mwezi Oktoba 2019, Papa alitangaza Mwezi Maalum wa Kimisionari na wakati huo huo akaitisha Mkutano Maalum wa Sinodi ya Maaskofu kwa Kanda ya Amazonia uliofanyika  mjini Roma, kwa lengo la kupendekeza  pia safari mpya za kutangaza Injili katika pafu la kijani kibichi, linaloteswa na kunyonywa na wale  wanaokiuka na kusababisha majeraha kwa ndugu zetu na dada zetu ulimwenguni (mafundisho ya Baba Mtakatifu kwa misa ya kufunga ya Sinodi ya Kanda ya  Amazonia).

Katika kipindi hicho chote Papa Francisko cha huduma yake kama papa ameweza kueneza nia nzima  akisisitiza katika magisterium yake juu ya asili ya utume wa Kanisa ulimwenguni. Kwa mfano, Papa Francisko amerudia mara kadhaa kwamba kutangaza Injili siyo kufanya propaganda, kugeuza imani, na kwamba Kanisa linakua kwa mvuto na kwa ajili ya kushuhudia.  Hayo yote na mengine yanapatika katika mkusanyiko wa maneno yote ambayo yanalenga kupendekeza dokezo ni nini nguvu inayofaa kwa kila kazi ya kitume, na chanzo chake kinaweza kuwa nini.

Kwa njia hiyo hayo  na zaidi yanapatika katika kitabu cha mahojiano kichopewa jina “ Bila yeye hatuwezi kufanya lolote’. Katika mazungumzo ya kuwa mmisionari leo hii katika ulimwengu. Shirika la habari za Kimisinoari Fides, limeweza kutoa hakikisho la dondoo kadhaa za kitabu hicho. Utume kwa maana ya Kanisa linalotoka nje, siyo mpango  badala yake ni nia ya kutekelezwa kwa juhudi za mapenzi mema. Ni Kristo ambaye hufanya Kanisa litoke ndani mwake binafsi. Katika utume wa kutangaza Injili, unasonga mbele kwa sababu Roho Mtakatifu anakusukuma na anabeba. Na unapofika, unatambua kwamba Yeye amewasili kabla yako na anakungojea. Roho wa Bwana alifika akiwa wa kwanza. Anatazamia mapema, pia anandaa njia yako na tayari yuko kazini kuandaa.

07 October 2020, 15:47