Tafuta

Pope Francisko huko Assisi katika Kaburi la Mtakatifu Francis Pope Francisko huko Assisi katika Kaburi la Mtakatifu Francis 

Papa Francisko:Udugu na utunzaji ndiyo njia ya maendeleo na amani!

Mara baada Sala Malaika wa Bwana,Papa amezungumzia juu ya Waraka mpya wa “Fratelli Tutti”uliotiwa sahini jana.Amekumbusha hitimisho la Kipindi cha Kazi ya Uumbaji pia kuhusu kiapo cha kikosi kipya cha wanajeshi wa Uswiss mjini Vatican.Amekumbuka kutangazwa Mwenyeheri Padre Olinto Marella na maadhimisho ya miaka 100 ya Stella Maris.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana amekumbusha ziara yake mjini Asisi tarehe 3 Oktoba 2020 ili kuweka sahini katika  Waraka mpya  wa “Fratelli tutti” yaani Wote ni ndugu.  “Nilimtolea Mungu  juu ya kaburi la Mtakatifu Fransisko, ambaye alinihimiza, kama vile hapo  awali kwa Laudato si. Ishara za nyakati inaonesha wazi kwamba udugu wa kibinadamu na utunzaji wa kazi ya uumbaji ndiyo njia pekee ya kuelekea maendeleo fungamani na amani, ambayo tayari imeoneshwa na Papa Mtakatifu Yohane  XXIII, Papa Paul VI na Yohane Paulo II. Na kwa kutangaza Waraka mpya wa Kitume katika toleo lisilo la kawaida la Osservatore Romano, limesambazwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Na kwa chapisho hili maalum, Papa amefafanua linaanza tena “toleo la kila siku la gazeti la Osservatore Romano".  Na kwamba " Mtakatifu Francis aongoze safari ya udugu katika Kanisa kati ya waamini wa kila dini na kati ya watu wote".

Toleo maalum la osservatore Romano
Toleo maalum la osservatore Romano

Kipindi cha Kazi ya uumbaji

Papa Francisko aidha amekumbusha kuwa tarehe 4 Oktoba imehitimishwa Kipindi cha Kazi ya Uumbaji kilichoanza tarehe Mosi Septemba. “Tumeadhimisha Jubilei ya Dunia Mama pamoja na ndugu zetu wa Makanisa mbalimbali ya kikristo. Kwa maana hiyo Papa Francisko amewasalimia wawakilishi wa vyama kiharakati katoliki ulimwenguni vinavyo hamasisha hali halisi ya tabianchi na vingine vinavyo jihusisha na Laudato si, vile vile vyama ambavyo vinajikita katika michakato ya ekolojia fungamani.

Hitimisho la kipinid cha kazi ya uumbaji
Hitimisho la kipinid cha kazi ya uumbaji

Kikosi cha Uswiss

Papa Francisko amewasalimia kwa namna ya pekee hata wanafamilia wa kikosi kipya cha walinzi wa kipapa waliofika Jijiji Roma kwa ajili ya kushuhudia afla ya watoto wao wakila kiapo kwa Papa. Vijana hawa watu ni wazuri!  amesema Papa. Walinzi wa Uswiss hufanya safari ya maisha kwa ajili ya  huduma ya Kanisa, ya Baba Mtakatifu. Ni watu wazuri ambao hufika hapa kwa miaka miwili, mitatu, minne na zaidi. Ninawaomba tuwapigie  makofi mazito kwa ajili ya Walinzi hawa wa Uswiss” amesema Papa.

Kikosi cha Ulinzi wa Papa Vatican  kutoka Uswiss
Kikosi cha Ulinzi wa Papa Vatican kutoka Uswiss

Mwenyeheri Olinto Marella

Moja ya mawazo ya Papa Francisko pia baada ya Sala ya Malaika wa Bwana yamekwenda moja kwa moja katika maadhimisho Jimbo kuu Bologna kwa ajili ya kutangazwa mwenyeheri Padre Olinto Marella, kuhani wa jimbo la Chioggia aliyekuwa  mchungaji kwa mujibu wa moyo wa Kristo, baba wa maskini na mtetezi wa wadhaifu. “Ushuhuda wake maalum uweze kuwa mfano wa kuigwa kwa wengi makuhani ambao wanaitwa kuwa wanyenyekevu na wajasiri katika kuhudumia watu wa Mungu" amesema Papa.

Mwenyeheri Padre Olinto Marella
Mwenyeheri Padre Olinto Marella

Stella Maris:utume wa bahari  

Papa Francisko hatimaye amekumbuka maadhimisho maalum hasa ya tarehe kama hii  4 Oktoba, ya miaka 100 iliyopita, ambapo ilianzishwa kazi ya “Stella Maris” yaani Utume wa habarini huko Scotland ili kusaidia watu wa baharini. “Katika maadhimisho haya muhimu, ninawatia moyo Mapadre wasimamizi wa kiroho wa mabaharia  na watu wa kujitolea ili kushuhudia kwa furaha uwepo wa Kanisa katika bandari, kati ya mabaharia, wavuvi na familia zao”.

Miaka 100 ya Stella Maris
Miaka 100 ya Stella Maris
04 October 2020, 15:51