2020.10.20 Mkutano wa Kimataifa kwa ajili ya amani. 2020.10.20 Mkutano wa Kimataifa kwa ajili ya amani. 

Papa Francisko:Hakuna anayejiokoa mwenyewe,bali kwa pamoja!

Leo hii uchungu wa vita umezidishwa na janga la virusi vya corona na ukosefu wa uwezekano kwa Nchi nyingi kupata matibabu ya lazima.Mizozo inaendelea,pamoja na maumivu na kifo.Kumaliza vita ni jukumu la lazima kwa viongozi wote wa kisiasa mbele za Mungu.Amani ndiyo kipaumbele cha sera za kisiasa.Mungu atauliza sana ambaye hakutafuta amani au alioongezea chochezi na migogoro,kila siku,miezi,miaka ya vita iliyowakumba watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni sababu ya furaha na shukrani kwa Mungu ya kuweza kukutana nanyi hapa Campidoglio katika moyo wa Roma na ninyi wakuu wa kidini na mamlaka, idadi kuwa ya marafiki wa amani. Tumesali, kwa ajili mmoja na mwingine kwa ajili ya amani. Ninamsalimia Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella. Ninayo furaha ya kukutana na Patriaki wa Kiekumene Batholomew. Ninampongeza sana kutokana na  matatizo ya safari yake  na wengine ambao wamependelea kushiriki  mkutano huu wa sala. Katika Roho ya mkutano wa Assisi, uliokuwa umeitishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 1986, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambayo inaadhimisha kila mwaka katika miji na tukio hili la sala na mazungumzo kwa ajili ya amani kati ya madhehebu mbali mbali ya kidini. Ndivyo Papa Francisko alivyoanza Hotuba yake  alasiri  mara bada ya kutoka Kanisani ikiwa ni fursa ya Mkutano wa sala kwa ajili ya amani katika roho ya Assisi ulioongozwa na mada “hakuna anayejiokoa peke yake: amani na udugu”,  mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambao  ulikuwa umegawanyika katika sehemu mbili ya kwanza  ya  sala ya kiekumene na madhehebu mengine ya kikristo iliyofanyika  katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa  (Aracoeli) na baadaye kufuatia afla na wawakilishi wa dini kuu za ulimwengu, na viongozi mbali mbali wa nchi  katika Uwanja wa Manispaa ya Roma(Campidoglio).

Papa Francisko akiendelea na hotuba yake amesema katika maono yale ya amani kulikuwa na mbegu ya kinabii ambayo hatua kwa hatua, na neema ya Mungu imekomaa kwa njia ya mikutano muhimu, matendo ya dhati ya amani, na mawazo mapya ya udugu. Kiukweli kwa kutazama nyuma tunakutana kwa bahati mbaya katika miaka iliyopita na matukio ya uchungu kama vile migogoro, ugaidi au itikadi kali na wakati mwingine kutumia jina la dini, na  kinyume chake  lazima kutambua hata hatua zenye kuleta matunda ya mazungumzo kati ya dini. Na kwa njia hii tumefikia Hati muhimu sana kuhusu “Udugu wa kibinadamu kwa ajili ya amani na kuishi pamoja iliyotiwa sahini na yeye pamoja na Imam Mkuu wa al-Azhar, Ahmed al-Tayyeb, mamno  2019, Papa amesema. Kwa hakika akiendelea  amesisitizia kuwa amri ya amani imedikwa kwa kina katika tamaduni za kidini (Rej, Fratelli tutti(Ft,284). Waamini wametambua kuwa utofauti wa dini hauthibitishi kutokujali au uadui. Badala yake ni kuanzia kiukweli na imani ya dini inawezekana kuwa wajenzi wa amani na sio watazamaji wasiotambua ubaya wa vita na chuki. Dini ziko katika huduma ya amani na udugu. Kwa maana hiyo hata wakati huu wa mikutano unasukuma viongozi wa kidini na waamini wote kusali bila kuchoka kwa ajili ya amani na sio kukata tamaa na kujiachia katika vita bali kujikita kwa nguvu ya imani nyeyekevu ili kumaliza migogoro.

Papa Francisko amesisitiza kwamba kuna haja ya amani, yaani  zaidi ya amani!,  “hatuwezi kubaki na sintofahamu. Leo hii ulimwengu unawaka kiu ya amani. Katika Nchi nyingi zinateseka kwa sababu ya vita, na mara nyingi zimesahauliwa lakini daima zinasababisha mateso na umaskini (Rej. Hotoba katika Siku ya Maombi kwa ajili ya amani ulimwenguni, Assisi, Septemba 20, 2016).  Ulimwengu, sera za kisiasa, maoni ya umma yapo hatarini kukinai ubaya wa vita, kama asili ya kampeni ya historia ya watu. “Tusiishie kwenye majadiliano ya kinadharia, badala yeke tuwasiliane na vidonda, tuguse nyama ya wale wanaopata uharibifu. [...]. Tuzingatie kwa umakini wakimbizi, wale ambao wamepata mionzi ya atomiki au shambulio la kemikali, kwa wanawake ambao wamepoteza watoto wao, kwa watoto ambao wamekeketwa au kunyimwa utoto wao”(Ft,261). Leo hii uchungu wa vita umezidishwa tena na janga la virusi vya corona na uwezekano kwa Nchi nyingi kutopata matibabu ya lazima. Wakati huo huo, mizozo inaendelea, na pamoja nao maumivu na kifo. Kumaliza vita ni jukumu la lazima la viongozi wote wa kisiasa mbele za Mungu. Amani ndiyo kipaumbele cha sera za kisiasa. Mungu atauliza sana ambaye hakutafuta amani au alioongezea chochezi na migogoro, kila siku, miezi, miaka ya vita iliyowakumba watu!

Neno la Bwana Yesu linapendekeza hekima yake ya kina. “Rudisha upanga wako mahali pake, anasema kwa maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga” (Mt 26,52). Wanashika upanga wote labda kwa kuamini kuwa wanasuluhisha hali ngumu kwa haraka, wanafanya uzoefu juu yao, juu ya wapendwa wao, juu ya Nchi yao, kifo ambacho kinakuja kwa upanga. “Basi” (Lk 22,38 alisema Yesu wakati mitume walipomwonesha panga mbili. Ile “basi”! ya Yesu Papa Francisko amesisitiza, inashinda karne na kufika kwa nguvu hadi kwetu leo hii: basi na mapanga, silaha, kutumia nguvu na vita!  Mtakatifu Paulo VI katika ziara yake kwenye Umoja wa Mataifa kunako mwaka 1965 alitoa mwangwi wa wito huo akisema “kamwe pasiwepo na vita tena” Hilo ndilo ombi letu sisi sote, wanaume na wanawake wenye mapenzi mema. Ni ndoto ya wote watafutao na wajenzi wa amani, kwa kutambua vema kuwa kila vita vinafanya ulimwengu kuwa mbaya sana kuliko tulivyoukuta (Ft 261).

Je ni Jinsi gani ya kutoka kwenye mizozo iliyokwama na iliyosugu? Jinsi gani ya kuyeyusha vifundo vilivyo jiviringisha vya mapambano mengi ya silaha? Jinsi gani ya kuzuia migogoro? Jinsi gani ya kuleta amani kwa mabwana wa vita au kwa wale wanaoamini katika nguvu za silaha? Hakuna watu, hakuna kikundi cha kijami kinaweza kutafuta peke yake amani, wema, usalama, na furaha. Hakuna. Fundisho la hivi sasa la janga, ikiwa tunataka kuwa wakweli, Papa amesema ni utambuzi wa kweli kuwa jumuiya ya kimataifa inapiga kasia katika mtumbwi ulio sawa, na mahali ambamo kuna ubaya wa mtu huangukia kwa hasara ya wote. Tulisahau kwamba hakuna mtu anayeokolewa peke yake, na kwamba mtu anaweza kuokolewa tu kwa pamoja (Ft,32).

Udugu unaobubujika kutokana na dhamiri ya kuwa binadamu pekee, unapaswa kuruhusu maisha ya watu, katika jumuiya, kati ya watawala na katika mikataba ya kimataifa. Kwa namna ya kuweka chachu ya utambuzi kuwa tunaokolewa tu kwa pamoja, kwa kukutana, kufanya michakato na kuacha kupigana, ili kupatana, kudhibiti lugha ya siasa na propaganda na  kukuza njia thabiti za amani ( Ft ,231). Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema “tuko pamoja jioni hii kama watu wa tamaduni za kidini tofauti, ili kuwasilisha ujumbe wa amani. Hii inaonesha wazi kuwa dini hazitaki vita. Kinyume chake, zinakanusha wale wanaopendelea vurugu, zinaomba kila mtu aombee upatanisho na afanye hatua za matendo ya udugu unaofungua njia mpya za matumaini. Kiukweli, kwa msaada wa Mungu, inawezekana kujenga ulimwengu wa amani na kwa maana hiyo kuokolewa pamoja.

20 October 2020, 18:49