Tafuta

Vatican News
Kanisa Kuu la  Nice nchini Ufaransa. Kanisa Kuu la Nice nchini Ufaransa.  (AFP or licensors)

Papa anasali kwa ajili ya wathirika;turudi kutazamana kama ndugu

Papa Francisko alaani tendo la ugaidi ambalo limetokea katika Kanisa Kuu la Mama Yetu “Notre-Dame” huko Nice nchini Ufaransa na kusababisha vifo vya watu watatu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika ujumbe wake uliotiwa sahini na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, Papa Francisko anaungana na familia za waathirika na kuwaalika katika umoja wa kitaifa. “Ni kipindi cha uchungu, ni kipindi cha mahangaiko. Ugaidi na kutumia nguvu haviwezi kamwe kukubalika. Shambulizi la leo hii limepanda vifo katika mahali pa upendo na faraja, katika nyumba ya Bwana”.

Huzuni wa Papa katika janga kigaidi la Nice umekuja katika hatua mbili ndani ya dakika chache wakati majira ya alasiri, tarehe 29 Oktoba 2020 kupitia kwa katibu mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, ambaye ametuma ujumbe alioutia saini kwa askofu wa Nice, André Marceau, kutoka kwa  Papa Francisko ambaye amelaani kitendo hicho na anaonesha ukaribu wake kwa  jumuiya yote ya wakatoliki nchini  Ufaransa lakini pia  kwa watu wote wa Ufaransa akiwaomba waungane pamoja.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Bruni akitoa taarifa kwa waandishi wa habari amesema, Papa Francisko ametaarifiwa hali halisi na kwa maana hiyo yuko karibu na jumuiya nzima katoliki katika maombolezo. Papa anasali kwa ajili ya waathirika na wapendwa wao kwa sababu vurugu hizi zipata kusitishwa na ili kurudia kutazamana kama kaka na dada na siyo kama adui na kwa sababu watu wapendwa wa Ufaransa waweze kujikimu kuuungana  pamoja na kupinga kila ubaya kwa wema.

29 October 2020, 16:37