Bendera ya Umoja wa Ulaya. Bendera ya Umoja wa Ulaya. 

Ndoto ya Papa Francisko ni Ulaya ya mshikamano na rafiki wa watu

Papa Francisko katika barua anajikita kutazama historia nzima na maadili ya bara la kizamani huku akiwa na matarajio ya mabadiliko ya kidugu katika kipindi kikubwa cha ukosefu wa usalama na hatari zitokanazo na hali ya sasa ya kiafya.Papa anaonya kuwa sii kama kutazama kama ndani ya album ya kumbu kumbu za picha bali ni jambo gani litolewe katika ulimwengu kwa ajili ya wakati ujao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameandika barua iliyo elekezwa kwa Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican katika fursa ya kumbu kumbu ya miaka 40 ya Tume ya Mabaraza ya Maaskofu Ulaya(Comece), Miaka 50 tangu uwepo uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Umoja wa Ulaya, vile vile miaka 50 tangu kuwepo kwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Baraza la Umoja wa Ulaya. Katika barua hiyo Papa anabinisha ndoto nne kwa sababu  amesema karne ya ustaarabu haijamaliza ule msukumo wake wote unaoongzwa na imani moja  na kwamba inawezekana ikawepo Ulaya ya kweli yenye nguzo ambazo zinalekeza kupanga  kama ilivyokuwa tangu mwanzo shauku ya kuwa na nafasi ya watu ambao wameunganishwa na mshikamano, mara baada ya mataifa hayo kugubikwa na vita na kuta. Katika barua  aliyomwelekeza Kardinali Parolin ni  wazi kwamba inalenga Bara la kizamani ,mbayo kwa maono yake, mawazo yake pamoja na ukweli wa hali halisi ya virusi anasema  vinasonga ndoto za waanzilishi wa Muungano wa Ulaya wawili tofauti mmoja akiwa ni Robert Schuman,Mwanzilishi wa Ulaya na Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye alitetea kwa dhati mizizi ya kikristo

Mtetemeko wa migawanyiko au udugu

Kumbukizi zilizomo, katika barua hiyo ni kuona  miaka 70 iliyopita tangu kutoa tamko la Schuman ambapo wakati ule Ulaya ilikuwa imegubikwa nyuma yake na migawanyiko ya vita. Lakini hii ni migawanyiko ambayo hata leo hii inawezekana, katika historia na ambayo imekuwa msukumo wa wa papa Fracisko kurudia mara nyingi akisikika “janga ni kama kitengenishi ambacho kinalazimisha kufanya mang’amuzi na uchanguzi hasa wa kuendelea katika njia ambayo imeendelezwa kwa miaka ya hivi karibuni inayoongozwa na vishawishi vya kujitosheleza kwa kwenda mbele kwa kukabiliana n kutokuelewana, vipingamizi na migogoro, au ni katika kugundua njia mpya ya udugu”.

Ulaya ijitafute yenyewe

Kiukweli ni mgogoro wa covid anabainisha Papa Francisko kuwa umeonesha wazi yote hayo kuwa kishawishi cha kutaka kufanya binafsi, katika kutafuta  suluhisho la muungano katika matatizo ambayo yanakumba kila kona ya mataifa na wakati tangu mwanzo wa kuundwa kwa Ulaya, baada ya vita, ilizaliwa kwa utambuzi wa upamoja na kwamba kuungana ni kufanya umoja uwe na nguvu zaidi na kama unavyobainisha wosia wa "Evangelii gaudium" kuwa umoja ni una nguvu zaidi ya migogoro na kwamba mshikamano unaweza kuwa mtindo wa ujenzi wa historia. Katika moyo wa Papa Francisko, mwangwi ni ule wa kile alichosema Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 9 Novemba 1982 huko Santiago ya Compostela, mara  baada ya hija yake ya Kitume nchini Uhisipania.

Mizizi ya kina ya karne

Maneno yake maarufu  ni kwamba "Ulaya unajikuta, kuwa yenyewe na iwe yenyewe” na ambayo sasa inatafsiriwa na Papa Francisko sawa sawa na nguvu hiyo na hivyo ameandika kwamba “ninataka kusema kuwa wewe Ulaya ambaye kwa karne nyinyi umekuwa kioto cha mawazo na sasa unaonekana kupotea kasi yako, usisimame na kutazama historia yako ya zamani kama vile picha za kumbu kumbu” walakini katika kipindi hiki hata kumbu kumbu nzuri zaidi ambazo hazifutiki na ambazo zinaishia kutokumbukwa tena”. Kujikuta mwenyewe  ni sawa, na kujikuta katika mawazo yenye mizizi ya kina. Kwa mujibu wa Papa Francisko ina maana ya kusema kutokuwa na hofu  ya historia binafsi, ya historia ya milenia ambayo ni dirisha ya  siku zijazo badala ya zamani . Na kwa maana hiyo anasisitza kwamba hakuna kuogopa hitaji la ukweli linalo chochewa na maswali ya fikira za zamani za kigiriki, hitaji la haki, lililoendelezwa na sheria ya Kirumi, hitaji la umilele, lililotajirishwa kwa kukutana na utamaduni wa Kiyahudi na Ukristo".

Ulaya ni familia moja

Kwa kufuata maadili hayo Papa Francisko ndipo ametoa maono yake manne, la  kwanza amebainisha kuwa “ninaota Ulaya rafiki wa mtu na watu. Ardhi ambamo hadhi ya kila mmoja inaheshimiwa, mahali ambamo mtu anakuwa na thamani yake na siyo kitu cha kuhesabiwa kiuchumi au kibiashara”. Ulaya katika maono hayo kwa mujibu wa Papa anabainisha  iwe ni ardhi ambayo inalinda maisha, kazi, mafunzo, utamaduni na ambayo inatamba kulinda yule ambaye ni mwathirika na mdhaifu, hasa kwa wazee, wagonjwa na ambao wanahitaji utunzaji kwa gharama na walemavu. Kufuatana na matokeo hayo ni wazi kwamba maono yake yanaleta ndoto ya pili ya Papa Francisko ambayo  amesema “Ninaota Ulaya ambayo iwe familia na jumuiya,  kwa maneno mengine, familia ya watu wenye uwezo wa kushinda kwa umoja na kufanya utofauti uwe tunu msingi kuanzia na ya mwanaume na mwanamke. Hapo Papa Francisko kwa ufupi wa ndoto yake  anazungumzia Jumuiya ya Ulaya, ya mshikamano na kidugu kinyume cha ardhi iliyogawanya katika hali halisi na ya kutaka kujitegemea, ambayo itajikuta haiwezi kukabiliana na changamoto za siku za usoni.

Ulaya ifungue mitazamo na milango wazi

Ndoto ya tatu ya Papa Francisko ni ile ya Ulaya ya Mshikamano na ukarimu, yaani kuwa mahali pa kukaribisha wageni na mahali ambamo hisani na upendo mkuu ndiyo inakuwa  fadhila ya kikristo. Ulya iweze kushinda kila aina ya mtindo wa sintofahamu na ubinafsi. Ili kuweza kuwa na mshikamano inahitaji kuwepo ukaribu na kwa maana hiyo Ulaya maana yake kwa namna ya pekee ni kuwa na uwezekano wa kuwa karibu, kuwa na shauku ya kusadia, kwa njia ya ushirikiano kimataifa na mabara mengine. Kwa kwa kutoa mfano Papa Francisko amefikiria hasa Afrika, ili isadiwe kuondaoa mgogoro mingi inayozidi kutanda. Aidha Papa ameshauri kuelekeza msaada kwa wahamiaji na si tu katika mahitaji ya haraka, lakini jitihada za muda mrefu katika njia ya ufungamanishwaji. Kwa hakika Papa Francisko anaota ndaoyo ya Ulaya ambayo iwe kweli jumuiya ya mshikamano ambao ndiyo kilio kimojawapo cha kuweza kukabiliana na changamoto mbele na kwa namna ya kubainisha kila aina ya suluhisho la sehemu ambazo tayari zimethibitisha upungufu wake.

Dini na ulimwengu

Ndoto ya nne ya Papa Fracisko amebainisha kuwa “ Ulaya ni ya kidunia na  yenye afya, ambayo Mungu na Kaisari ni tofauti lakini hawapingani. Na kwa namna hiyo Papa Francisko anataka kusema kuwa  Ulaya iwe ardhi iliyojifunguliwa kwa  aliye juu na mahali ambamo waamini wanakuwa huru kukiri wazi imani yao na kupendekeza mitazamo yao katika jamii. "Ulaya ambayo katika kipindi  cha kukiri kimesua sua lakini akiwa na matumaini ya kwamba watoto wake wanaweza kurudi katika kurudi dini fulani na ambayo inafungulia milango wengine na zaidi ya yote kwa Mungu, kwani  amebainisha kwamba utamaduni au mfumo wa kisiasa ambao hauheshimu Mungu ni wazi hauwezi kufungua vya  kutosha na kuheshimina hadhi ya mtu”.

Wakati ujao ni wa kuandika

Mawazo ya mwisho ya Papa Francisko kwa ajili Ulaya ni uwajibikaji mkubwa wa kikristo katika kuongoza mabadiliko kwa mantiki zote na mahali ambamo tunaishi na kufanya kazi kwa ajili ya kukabidhi Ulaya iwe  njema na kwa njia ya maombezi ya wasimamizi watakatifu wake Benedikto, Cyril, Metodius, Brigida, Caterina, na Teresa Benedetta wa salaba. Kwa njia hiyo ni matumaini makubwa ya Papa Francisko kwamba Ulaya bado ina mambo mengi ya kuweza kutoa kwa ajili ya ulimwengu.

27 October 2020, 13:48