Mawimbi ya bahari Mawimbi ya bahari 

Msaada wa Papa kwa familia za mabaharia waliozama na meli Japan

Kwa upitia Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu,Papa ametuma msaada kwa wanafamilia wa mabahari waliofariki Dunia kunako Septemba 2 huko Japan baada ya kukumbwa na kimbunga kikali kiitwacho Maysak.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Meli ilikuwa inatokea katika Bandari ya New Zealand kuelekea Bandari ya Jingtang, huko Tangshan, nchini China iitwayo M/V Gulf Livestock 1 na ilizama karibu na bahari ya Japan katika  kisiwa cha Amami Oshima, kunako tarehe 2 Septemba 2020.

Kwa bahati mbaya kwa sababu ya injini kutofaulu wakati wa kupigwa na kimbunga cha nguvu kiitwacho Maysak, mabaharia hao walizama wote. Waliokuwamo ndani wafilippini 39, Waaustralia 2 na 2 kutoka New Zealand. Papa Francisko kwa maana hiyo ameweza kufikiria familia zao na waokoaji wawili wa janga hilo, kupitia Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya Watu kwa kutuma mchango wa kiuchumi pamoja na zawadi ndogo binafsi kama ishara ya ukaribu na mshikamano.

Msaada wa kiuchumi kwa ushirikiano na Ubalozi wa Kitume na Shirika la Kipapa la Stella Maris huko Uffilippini, Australia na New Zealand, utawakilishwa binafsi  kwa mujibu wa Baraza la Kipapa Vatican,  pamoja na zawadi binafsi ya Papa Francisko, ili kuonesha ukaribu wake na mshikamano. Ni ishara moja ambayo inawasindikiza kiroho, kisaikolokia na kihisia kwa familia za ufilippino kwa upande wa timu ya wataalam, makuhani na watawa katika Vituo vya Shirika la Stella Maris.

Msaada huo, ambao kwa kuzingatia vizuizi kutokana na janga la corona  hadi sasa umetekelezwa kupitia utumiaji wa vyombo vya kijamii na majukwaa la digitali na itaendelea kwa miezi michache ijayo. Kazi hii imekabidhiwa kwa Bikira Maria Msimamizi wa mabaharia kuweza kuwaimarisha ujasiri na nguvu kwa wanafamilia wote katika kukabiliana na siku za usoni ambazo hazina  uhakika, lakini kwa ujasiri na utulivu.

21 October 2020, 16:15