Mkutano wa Papa na Mwenyekiti wa Msalaba mwekundu kimataifa!
Migawanyiko yenye kule uchungu sana na ambayo inasababaisha athari kwa watu wengi na zaidi walio katika mazingira magumu, kwa ajili ya wahamiaji, uhamisho wa ndani kwa sababu ya vita na kutumia nguvu, kwa ajili ya watu ambao wameambukizwa na harakati ya kununua silaha, mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa maendeleo, ubaguzi umasikini na ukosefu wa haki. Haya yote na masuala mengine mengi zaidi yameyozungumzwa. Dk.Maurer pia amebainisha juu ya mtazamo wa pamoja wa Papa wenye utashi wa kujenga madaraja kwa ajili ya kukamilisha jamii shirikishi. Hatimaye Dk. Maurer amesisitiza pia kuhusu mada ya Wosia wa “Fratelli tutti” yaani Wote ni ndugu kwamba inaweza kufikiriwa kama kaulimbiu ya shughuli za Msalaba Mwekundu Kimataifa.
Mahojiano kamili na Mwenyikiti huyo Dk. Peter Maurer yatatakangazwa kesho kupitia Tovuti ya Vatican News na Ukurasa wa Gazeti la Osservatore Romano.