2020.09.12 Papa amekutana na wanafamilia wa vijana waliofariki katika klabu ya muziki huko Corinaldo (Ancona) (8 Desemba 2018) 2020.09.12 Papa amekutana na wanafamilia wa vijana waliofariki katika klabu ya muziki huko Corinaldo (Ancona) (8 Desemba 2018) 

Ukaribu wa Papa Francisko kwa wanafamilia katika uchungu na mateso!

Papa Francisko amekutana na familia na ndugu wa marehemu vijana watano na mama mmoja waliofariki katika ajali ya klabu ya muziki wa usiku huko Corinaldo,nchini Italia.Papa anaungana nao kwa sala na uchungu hasa katika shauku yao ya kupata ukwli na haki ya sababu zilizosababisha ajali hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Papa Francisko Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020 amekutana mjini Vatican na wanafamilia wa vijana 5 na mama mmoja waliofariki  katika Klabu ya muziki  wa usiku huko Corinaldo, Ancoana  nchini Italia.  Katika salam zake anawashukuru kufika kwao na kushirikishana naye uchungu wao na sala zao. Bado anayo kumbu kumbu ya janga hilo, ambalo lilimshitua sana. Lakini kadiri siku zinavyopita amesema, kwa bahati mbaya yamefuatia majanga mengine  ya kibinadamu ambayo yanasababisha kusahu. Mkutano wao huo ni fursa ya kumsaidia Papa na Kanisa wasiweze kusahau na kubaki kidete ndani ya moyo na hasa kwa kumkabidhi ndugu zao wapendwa katika moyo wa Mungu Baba mwenyezi.

Kila kifo cha ajali upelekea uchungu mkubwa sana. Lakini unapochukua vijana watano na mama mmoja kijana, ni uchungu usiolezeka bila msaada wa Mungu. Ata hivyo pia  Papa Francisko amesema hataki kuingilia kati juu ya sababu zilizosababaisha  ajali hiyo katika Disko, mahali ambamo walifariki ndugu zao. Yeye anaungana na uchungu wao na mateso yao na shauku yao ambayo wanataka  kupata ukweli na  haki ya chanzo cha ajali hiyo.  Papa Francisko hakuishia hapo bali ametaka kuwapa ushauri kwa kutumia   neno la imani, kiutulizo na matumaini. Corinaldo amesema ni mahali pa ajali, ambapo sehemu hiyo inapakana karibu na madhabahu ya Bikira Maria wa Loreto. Madhabahu yake siyo mbali sana. Kwa maana hiyo Papa anawashauri kufikiria Yeye kama Mama ambaye hajawahi kwenda mbali kwa mtanzamo wake juu yao, hasa katika wakati ule wa kuchanganyikiwa kwa ajali ile. Yeye aliwasindikiza kwa huruma yake. Ni mara ngapi imetamkwa Salam Maria. Utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu!  Na hata kama wakati huo huo wa ajali hiyo hakufanya lolote, Mama Maria hasahau maombi yetu, anasema Papa. Kwa uhakika aliwasindikiza katika mikono yake ya huruma kwa  mwanao Yesu Kristo

Ajali hiyo ilitokea usiku, katika masaa machache ya kwanza ya tarehe 8 Desemaba 2018, ambayo ni Siku kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili. Katika siku hiyo, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko amekumbusha na kusema: “nilisali na waamini kwa ajili ya vijana waathrika, kwa ajili ya majeruhi na kwa ajili yenu wanafamilia. Ninajua kuwa mambo mengi yaliyoanziswa na maaskofu wenu ambao wapo hapa, mapadre wenu na jumuiya zenu ziliwasaidia kwa sala na kwa upendo”. Hata sala yangu kwa ajili yenu inaendelea na kuwasindikiza kwa baraka zangu”.

Tunapopoteza baba au mama sisi ni yatima mvulana na msichana. Kuna kivumishi  ‘Yatima’. Katika ndoa anapotokea kifo cha mmoja,  mke au mme  hata hapa kuna kivumicha ‘mjane’. Lakini mtoto anapofariki hapo hukuna kivumishi. Na akiulizwa mtu anasema “Nimempoteza mwanangu”: lakini nini ...? Hapana, hapana: mimi siyo yatima wala mjane. Nilipoteza mtoto wa kiume au kike. Bila kuwa na kivumishi. Na hayo ndiyo maumivu yenu makubwa”, Papa Francisko amefafanua. Kwa kuhitimisha amewaomba kusali sala ya Salamu Maria kwa ajili ya marehemu Asia, Benedetta, Daniele, Emma,Mattia na Eleonora.

12 September 2020, 14:54