Papa kwa UN:Mgogoro wa janga ni fursa kujenga jamii ya kidugu

Katika kumbukizi la miaka 75 tangu kuanzishwa Umoja wa Mataifa,Papa Francisko amewatumia ujumbe kwa njia ya video katika mkutano mkuu unaoendelea siku hizi na karibu kwa njia ya mitandao.Papa anashauri Jumuiya ya kimataifa kuhusu matumizi ya silaha,wahamiaji wasio kuwa na haki,kufikiria tena mifumo ya kiuchumi na fedha,aidha emelaani utoaji wa mimba.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa Umoja wa Mataifa UN katika fursa ya Juma lao kuu. Katika ujumbe wao, anawasalimia kuanzia na Rais wa Mkutano huu Mkuu, wawakilishi wanaoshiriki siku hii muhimu ya maadhimisho ya miaka 75 ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Kwa namna ya pekee salama zake kwa Katibu Mkuu Bwana António Guterres, wakuu wa nchi ambao wanashiriki na wale wote ambao wanafuatilia mjadala Mkuu. Miaka 75 ya Umoja wa Mataifa ni fursa ya kuonesha shauku ya Vatica kuwa Shirika hili ni ishara ya kweli na chombo cha umoja kati ya Mataida na huduma ya familia yote ya binadamu. Kwa sasa ulimwengu wetu umepata pigo na janga la Covid-19, ambalo limepelekea kupotea kwa maisha ya wengi. Mgogoro huu uko unaleta mabadiliko katika mtindo wetu wa maisha, kuongezeka kwa mijadala ya mifumo yetu ya kiuchumu, kiafya na kijamii wakati huo huo kuonesha udhaifu wetu kama viumbe. Papa amesema.

Janga hili linatuita kwa dhati kupokea kipindi hiki cha majaribu kama kipindi cha kufanya uchaguzi (…): kipindi cha kuchangua ni jambo gani la muhimu, na lipi linapita, kutengenisha kile ambacho ni cha lazima na kile ambacho siyo. Kinaweza kuwakilisha fursa ya kweli kwa ajili ya uongofu, mabadiliko na kwa ajili ya kufikiria tena mitindo yetu ya maisha na mifumo yetu ya kiuchumi na kijamii ambayo inazidi kuongeza umbali kati ya maskini na matajiri, kufuatia na ukosefu wa haki ya ugawanaji wa rasilimali. Lakini pia inaweza kuwa uwezekano wa mafungu ya kujihami na tabia ya kibinafsi na ya wasomi. Kwa maana hii wakati huu unakabiliwa na uchaguzi kati ya mojawapo ya njia mbili zinazowezekana: moja inaongoza kwa kuimarishwa kwa pande nyingi, kielelezo cha uwajibikaji mpya wa ushirikiano wa ulimwengu, mshikamano unaotegemea haki na juu ya kutimiza amani na umoja wa familia ya wanadamu, mpango wa Mungu kwa ajili ya ulimwengu; inapendelea mitazamo ya kujitosheleza, utaifa, kujilinda, ubinafsi na kujitenga, ukiwaondoa maskini, walio hatarini zaidi, wakazi wa maeneo ya pembezoni mwa maisha. Na hakika utadhuru jamii yote, ikiwa ni kujidhuru kwa wote. Na hii haipaswi kushinda.

Jitihada nyingi kuu za kimataifa za kukabiliana na shida hizi zinaanza na ahadi kubwa, pamoja na Hati mbili za Mkataba wa Ulimwenguni juu ya Wakimbizi na Uhamiaji, lakini wengi hawana msaada wa kisiasa unaohitajika kufanikiwa. Wengine hushindwa kwa sababu majimbo binafsi hukwepa majukumu na ahadi zao. Walakini, shida ya sasa ni fursa: ni fursa kwa Umoja wa Mataifa (UN), ni fursa ya kuzalisha jamii ya kindugu na yenye huruma zaidi, Papa Francisko amesisitiza. Papa amesema kuwa Jumuiya ya kimataifa lazima ijitahidi kumaliza dhuluma za kiuchumi. Wakati mashirika ya kimataifa ya mikopo yanatoa ushauri kwa mataifa tofauti, ni muhimu kuzingatia dhana kubwa za haki ya kifedha, bajeti za umma zinazohusika na deni lao, na juu ya yote, kukuza kwa ufanisi, na kuwafanya wahusika wakuu, ambao ni maskini zaidi katika njama hiyo kijamii. Tuna jukumu la kutoa msaada wa maendeleo kwa mataifa maskini na kupunguza deni kwa mataifa yenye deni kubwa. Maadili mapya yanaonyesha kuwa na ufahamu wa hitaji la kila mtu kujitoa kufanya kazi pamoja ili kufunga makao ya ushuru, kuepuka ukwepaji wa kodi na utapeli wa pesa ambazo zinaibiwa kwa jamii, na kama ilivyo kuwambia mataifa juu ya umuhimu wa kutetea haki na faida ya wote juu ya maslahi ya kampuni zenye nguvu na mashirika ya kimataifa.

Huu ni wakati muafaka wa kusasisha usanifu wa kifedha wa kimataifa. Hatuwezi kupuuza matokeo mabaya ya shida ya Covid-19 kwa watoto, pamoja na wahamiaji na watoto wa wakimbizi wakisindikizwa. Ukatili dhidi ya watoto, pamoja na janga baya la unyanyasaji wa watoto na picha mbaya zimeongezeka sana. Kwa kuongezea, mamilioni ya watoto hawawezi kurudi shuleni. Katika sehemu nyingi za ulimwengu, hali hii inatishia kuongezeka kwa ajira kwa watoto, unyonyaji, unyanyasaji na utapiamlo. Kwa bahati mbaya, nchi na taasisi za kimataifa pia zinahimiza utoaji wa mimba kama moja ya kile kinachoitwa "huduma muhimu" katika jibu la kibinadamu. Inasikitisha kuona jinsi ilivyo rahisi na rahisi kwa wengine kukataa uwepo wa maisha kama suluhisho la shida ambazo zinaweza na lazima zitatuliwe kwa mama na mtoto ambaye hajazaliwa. Papa Francisko amewasihi viongozi wakuu wa raia ili kwa haraka na umakini kuwasaidia watoto ambao wanakataliwa haki zao na hadhi msingi kwa namna ya pekee ya kuonekana katika mwanga wa maisha na katika elimu.

Papa amewakumbusha hata wito wa kijana jasiri Malala Yousafzai, ambaye miaka mitano iliyopita katika Umoja wa Mataifa alikumbusha kuwa “mtoto, mwalimu, kitabu na kalamu vinaweza kuubadili ulimwengu”. Hatutoki sawa kutokana na shida ya janga, ama tunatoka tukiwa bora au vibaya. Kwa njia hiyo, katika wakati huu muhimu, jukumu letu ni kufikiria tena siku zijazo za nyumba yetu ya pamoja, mipango yetu ya pamoja. Ni kazi ngumu, ambayo inahitaji uaminifu na mshikamano katika mazungumzo, ili kuboresha ujamaa na ushirikiano kati ya mataifa. Mgogoro huu unasisitizia zaidi mipaka ya kujitosheleza na udhaifu wetu wa pamoja na unatuongoza kutamka wazi jinsi tuvyotaka kuondokana nao tukiwa bora au vibaya sana. Kwa sababu hiyo, Papa amerudia kusema kuwa, katika mgogoro huu hatutoki salama, ama tunatoka bora au tunatoka vibaya zaidi. Janga hilo limetuonyesha kuwa hatuwezi kuishi bila kutegemeana mmoja kwa mwingine, au mbaya zaidi, dhidi ya kila mmoja. Umoja wa Mataifa uliundwa kuunganisha mataifa, kuyaleta karibu, kama daraja kati ya watu; kwa maana hiyo uashuri wa mwisho wa Papa ni kwamba “basi tuutumie wakati kubadilisha changamoto tunayokabiliana nayo kuwa fursa ya kujenga pamoja, kwa mara nyingine tena, wakati endelevu tunaoutaka”.

25 September 2020, 15:50