Tafuta

2020.09.09 Katekesi ya Papa Francisko 2020.09.09 Katekesi ya Papa Francisko 

Papa Francisko:Vijana wana haki ya kupata elimu licha ya vita na ugaidi!

Ni lazima kuhakikishia wavulana na wasichana wanapata elimu hata katika Nchi ambazo zimekumbwa na vita na ugaidi.Amesema hayo Papa Francisko mara baada ya Katekesi yake akikumbusha Siku ya Umoja wa Mataifa ya Kulinda Elimu dhidi ya mashambilizi katika muktadha wa migogoro na silaha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya katekesi yake Papa Francisko Jumatano, tarehe 9 Septemba 2020 amekumbusha Siku ya kwanza ya Kimataifa ya Kulinda Elimu dhidi ya mashambulizi katika muktanda wa migogoro ya kisilaha. Papa amewaalika wote kusali kwa ajili ya wanafunzi ambao wanazuiwa vibaya sana haki ya kupata elimu, kwa sababu ya vita na ugaidi. Kadhalika ameshauri Jumuiya ya Kimataifa kujikita kwa dhati ili iwezeshe kweli kuheshimiwa majengo ambayo yanapaswa kulinda vijana wanafunzi. Jitihada pia zisipungue kwa ajili ya kuhakisha mazingira salama ya mafunzo hasa katika hali ya dharura ya kibinadamu

Siku hi ni mpango uliochaguliwa na Umoja wa Mataifa UN ambao unaisherehekea tarehe 9 Septemba kwa mara ya kwanza huku ikilaani vikali kuhusu mashambulizi dhidi ya elimu na matumizi ya shule za kijeshi kwa watoto kama ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Kwa upande wake, katika ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) linaonyesha kuhusu janga hili kuwa ni maradufu ya Covid-19 na mashambulizi ya  shule, ambazo zinalenga walimu na wanafunzi, huku yakitishia kumaliza mafanikio ya elimu kwa wakimbizi na kuharibu ndoto za mamilioni ya vijana.

09 September 2020, 14:50