2020.07.20 - LAUDATO SI : HISTORIA 2020.07.20 - LAUDATO SI : HISTORIA 

Papa:Dunia haitafakariwi nje ya binadamu ni ndani mwake na utambuzi wa uhusiano na Mungu!

Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 katika ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya mtandao anasema kuwa kwa upande wa mwamini,DUNIA hautafakariwi nje yake mwanadamu bali ndani mwakena kuwa na utambuzi wa uhusiano ambao Baba alituunganisha sisi kama binadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni katika muktadha wa Kipindi cha Kazi ya uumbaji, kinachoangazia na kutukumbusha waraka wa Papa Francisko wa  Laudato si, kuhusu Utunzaji bora wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja. Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 katika ujumbe wake  kkwenye mtandao ya kijamii amesema kwa upande wa mwamini, DUNIA haitafakariwi kupitia nje yake bali ndani mwake na kuwa na utambuzi wa uhusiano ambao Baba alituunganisha sisi kama binadamu.

Papa Francisko katika Sura ya pili ya wosia wa Laudato si  anasema mazingira ni zawadi kutoka kwa Mungu baba ambao ni urithi wa pamoja unaopaswa kutunzwa na wala si kuuharibu, kwani ni amana ya binadamu wote na zaidi kwa ajii ya kizazi kijacho. Papa Francisko aidha katika kuelekeza zaidi anatoa hata mambo matatu msingi ya kuzingatia na ambayo hayawezi kuachwa kwa maana unakwenda sambamba au kama kidole na pete.

Awali ya yote ni mahusiano ya dhati na Mungu, pili uhusiano wa mtu na jirani yake na tatu ni ardhi inayomzunguka. Kwa njia hiyo ni wazi katika ujumbe wake wa siku ya leo ambao  yeye anasisitiza juu ya kutafakari dunia kama waamini tukiwa ndani mwake na zaidi kuwa na utambuzi kwa yule Mungu ambaye ni muumba yaani ndiye chanzo na mwisho wa mwanadamu huyo na kila kiumbe. Hii ina maana ya kwamba kila kiumbe kina nafasi yake ambayo kwayo inaangazia wema wa Mungu tuliopewa bure na  tunazidi kupewa bure lakini tukiwa na hitaji la kuweza kuitunza. tunu hii msingi. Kutumia vibaya kazi ya Mungu ni kwenda kinyume cha utu wa binadamu aliyeumbwa kwa mfano na sura yake.

Kutafakari kazi na utunzaji wa viumbe hai  au kazi ya v uumbaji wa  Mungu inahitaji kusindikizwa na wema na wajibu kwa ajili ya binadamu. Ni mwaliko Papa kwetu sote Katika kipindi cha Kazi ya Uumbaji kutoa kipaumbele cha  utunzaji wa mazingira kwa ajili ya wote na kwa ajili ya matumizi binafsi ambayo yazingatie kanuni msingi.

11 September 2020, 15:52