Tafuta

2019.08.19 Mkutano Rimini 2019.08.19 Mkutano Rimini 

Ujumbe wa Papa kwa mkutano wa Rimini:kuwa mashahuda wa nguvu ya imani ya kuvutia!

Uzuri wa Mungu na furaha ya imani ndiyo ufunguo wa ujumbe wa Papa Francisko uliotiwa sahini na Katibu wa Vatican,Kardinali Parolin ambapo Papa anawabariki washiriki wa Mkutano wa kiutamaduni wa "urafiki kati ya watu", “Meeting per l’amicizia fra i popoli” uliondaliwa na Jumuiya ya Comunione e Liberazione utakaofunguliwa tarehe 18-23 Agosti 2020 katika mtindo tofauti kutokana na Covid 19.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kuanzia tarehe 18 hadi 23 Agosti 2020  unafunguliwa mkutano wa toleo la 41 kwa ajili ya “urafiki kati ya watu” au Meeting per L’amiciza fra i popoli”. Ni mkutano ambao kiutamaduni umekuwa ukifanyika katika kipindi cha kiangazi na ambao unafunguliwa kwa mtazamo wa macho ya imani ulioandaliwa na  Jumuiya ya 'Communione e Libarazione'.  Mkutano huo unaongozwa na kauli mbiu isemayo:  “Bila kuwa na mshangao tunabaki viziwi mbele ya ukuu”. Mkutano huo utafanyika katika mtindo tofauti kutokana na janga la Covid 19 ambapo wataendeleza mada kutazama changamoto ya kukabiliana na ni fursa ya kujikita katika mada za kiroho na kijamii kwa ujumla. Kutokana na fursa hiyo Papa Francisko ametuma ujumbe wake. Katika ujumbe huo uliotiwa sahini na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, anawafikishia matashi mema ya  ufanisi kupitia  kwa Askofu Francesco Lambias wa jimbo Katoliki la Rimini na kwa njia yake  anawakumbuka washiriki wote ambao wataweza kubadilishana mada mbali mbali hadi tarehe 23 Agosti ikiwa ni pamoja na majukwaa ya kidigitali na uwepo wa umma kwenye makao ya Mikutano ya maonyesho huko Rimini, Italia.

Mshangao ni njia ya utambuzi na imani

“Ukosefu wa mshangao tunabaki viziwi mbele ya ukuu” ni kauli mbiu maalum ya mwaka huu iliyochukuliwa kutoka kwa mwanafalsafa wa kiyahudi, Abraham Joshua Heschel na kutajwa na Padre Giussani, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Comunione e Liberazione  na ambapo kauli hiyo imetoa msukumo hata katika ujumbe wa Papa Francisko uliotiwa sahini na Katibu wa Vatican kwa kusisitiza ni kwa jinsi gani “mshangao ni jambo ambalo linaweka na kuwasha injini ya maisha, kwa kuwezesha kuanza safari kwa kila hali  na zaidi ni zawadi kama asemavyo Papa Francisko kwamba inazuia maisha yasiwe kijivu, ya kuwa na mazoea kama inavyojikeza katika imani. Hata Kanisa linahitaji kupyaishwa na mshangao wa kuweza kuishi Mungu aliye hai, Mchumba wa Bwana na Mama anayezaa watoto wake anasisitiza Papa. Janga la ungojwa wa mapafu limetufanya tuwe na uzoefu wa hali ya mshangao ambayo inachukua mtindo wa kuwa na huruma mbele ya mateso. Janga hili limewasukuma mashujaa wengi wa kila siku kama vile madaktari, wauguzi, waalimu ili kukabiliana na changamoto ya Corona kwa kujitolea na juhudi na limeruhusu wengi kupata nguvu ya kukabiliana na ugumu na uchovu kwenye nyuso na mbele ya wanafamilia, Papa anabainisha katika ujumbe huo.

Utafutaji wa Mungu

“Kwa mantiki hii, kauli mbiu ya Mkutano huo ni wito wenye nguvu ya kuweza kushuka kwenye vilindi vya moyo wa mwanadamu kupitia kamba ya mshangao” na  ambayo kiukweli ni njia ya kufahamu  ishara za mada kuu, yaani  ambayo ni fumbo linalofanya mzizi na msingi wa vitu vyote. “Ni kwa njia ya mshangao tu unajua”. Kwa upande mwingine anaeleza Papa kwamba  ikiwa macho hayana mwanga, tanakuwa kipofu mbele ya ugumu, yanafumba ndani mwake binafsi na kubaki kuvutiwa visivyo dumu, huku akiacha kujihoji kuhusu hali halisi iliyopo. Hata hivyo janga hili pia limesukuma watu wengi kujihoji kuhusu utafutaji wa maana ya maisha, maumivu, kifo na hasa wakati wa karantini na kuona ukosefu wa nini la kufanya  na ndicho kinathibitisha ile kiu isiyokoma ambayo inaashiria moyo wa mwanadamu kuwa hajaweza kutosheka na majibu ya kijuu juu.

Ndani ya mwanadamu anakuwa  na hamu ya pumzi isiyoisha 

Baba Mtakatifu Francisko anasema  katika ujumbe wake kuwa ndani yake mwanadamu ana hamu ya pumzi isiyo isha, huzuni usiyo na mwisho, tamaa isiyoridhika na jibu  sawa  lisilo isha. Maisha yatakuwa ni shauku ya upuuzi, ikiwa jibu hili lisingelikuwepo. "Hali kama hii kubwa ya ugonjwa huu kwa maana hiyo umeweza kurudisha, angalau kwa muda mfupi, njia ya kweli  na zaidi ya kuthamini uwepo wa mtu, bila ugumu wa usumbufu na maoni ambayo huchafua mitazamo, uzuia mitazamo ya mambo, uondoa utupu na kuwa na mshangao na kutuondolea tusijiulize kuwa sisi ni nani”

Changamoto kwa wakristo: ushuhuda wa uzuri wa Mungu

Uzuri pia umeunganishwa na kushangaa, ujumbe unaosomeka kuwa ni “uzoefu wa kuamua kufikia ukweli”. Kwa sababu hii, kauli  mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni changamoto ya Wakristo, wanaoalikwa kushuhudia na kuwa kivutio kikubwa cha kushuhudia kwa kina ambacho imani ukita kwa uzuri wake yaani  kivutio cha Yesu, kwa mujibu wa usemi wa mpendwa Mtumishi wa Mungu Padre Luigi Giussani. Kwa mjia hiyo basi  moyo wa ujumbe wa Papa  Francisko ni mwaliko wa kuendelea kushuhudia uzoefu wa uzuri wa Mungu, ambaye alijifanya  mwili ili macho yetu yashangae na kuona uso wake na mitazamo yetu ipate kutoka kwake ule mshangao wa kuishi. Ni kazi ambayo hatuwezi kuepukana nayo, hasa katika hali hii nyembamba na yenye makona mengi katika historia. Ni wito wa kuwa wazi kwa uzuri ambao umetubadilisha maisha yetu, mashuhuda halisi wa upendo unaookoa na zaidi kuwa na mtazamo wa  wale ambao wanateseka sana.

17 August 2020, 15:01