Tafuta

Vatican News
2019.09.12 Mzani ni mfano haki 2019.09.12 Mzani ni mfano haki 

Papa Francisko:usijiamini kuwa mwenye haki maana ni kosa la kiroho!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwenye mtandao wa kijamii tarehe 25 Agosti 2020 mzizi wa kila kosa la kiroho ni kujiamini mwenye haki.Kujiamini kuwa mwenye haki ni kuacha Mungu awe mwenye haki pekee nje ya nyumba.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Katika ujumbe wa kila siku ambao utoa Papa  kwenye mitandao ya kijamii, Jumanne tarehe 25 Agosti 2020, Papa Francisko amesema “mzizi wa kila kosa la kiroho ni kujiamini mwenye haki. Kujiamini kuwa mwenye haki ni kuacha Mungu awe mwenye haki pekee nje ya nyumba”. Lakini je kujifikiria mwenye haki maana yake ni nini?  Kwa kawaida, wanadamu huelewa haki kuwa utekelezaji wa sheria bila upendeleo. Haki inahusiana na sheria, wajibu, haki za watu, na madaraka, nayo hutekelezwa bila kupendelea na kwa yule anayestahili.’Hata hivyo, Mungu hatekelezi haki kwa kushikilia tu sheria bila kujali ili kutimiza tu wajibu.

Mungu peke yake ndiye mwenye haki. Tunaweza kuelewa kwa undani haki ya Mungu kwa kuchunguza maneno ya lugha nyingi  zilizo tumiwa katika Biblia Takatifu kuanzia Agano la Kale hadi Agano jipya. Katika Maandiko ya Kiebrania, maneno matatu muhimu yanatumiwa. Neno ambalo mara nyingi hutafsiriwa “haki” linaweza pia kumaanisha “yaliyo sawa.” soma kitabu cha Mwanzo 18:25. Maneno mawili yanayosalia hutafsiriwa kwa kawaida kuwa “uadilifu.” Katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, neno linalotafsiriwa “uadilifu” linafafanuliwa kuwa “sifa ya kuwa sawa au mwenye haki.”

Kwa maana hiyo tunaweza kusema kuwa , hakuna tofauti kati ya uadilifu na haki,   soma katika kitabu cha  Amosi 5:24. Kwa hiyo katika Biblia inaposema kwamba Mungu ni mwenye haki, inamaanisha kwamba siku zote yeye hutenda yaliyo sawa bila kupendelea na bila ubaguzi.  Ni wazi kwamba usijamini kuwa mwenye haki bali kumwachia Mungu awe mwenye haki tu.

Tunapsoma kutoka 2, 11 kikweli, Mungu hawezi kamwe kutenda isivyo haki. Tunakumbuka katika Biblia neno la haki kwa upande wa Ayubu 34:10 ?  “Ni kweli kwamba Mungu hawezi kamwe “kutenda udhalimu.” Kwa sababu mbili muhimu awali ya yote  yeye ni mtakatifu na ni mwadilifu kabisa. Kwa hiyo, hawezi kutenda uovu au kutenda isivyo haki. Tusijamini kuwa wenye haki, maana ni Mungu peke yake kama anavyosisitiza Papa Francisko, na tujifunze kutenda haki kuliko kujiamini maana ni kosa la kioroho kama anavyofundisha Papa.

25 August 2020, 15:19