Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anafuatilia kwa umakini mkubwa mgogoro unaoendelea kufuka moshi huko Mashariki mwa Bahari ya Mediterrania kati ya Ugiriki na Uturuki. Baba Mtakatifu Francisko anafuatilia kwa umakini mkubwa mgogoro unaoendelea kufuka moshi huko Mashariki mwa Bahari ya Mediterrania kati ya Ugiriki na Uturuki. 

Papa Francisko: Hofu na Wasiwasi Kutokana na Mgogoro wa Mediterrania

Papa anafuatilia kwa umakini mkubwa mgogoro ulioibuka huko Mashariki wa Bahari ya Mediterrania, hali inayotishia amani na usalama. Baba Mtakatifu anwasihi wadau wote katika mgogoro huu, kujikita katika mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi, kwa kuheshimu na kuzingatia sheria za kimataifa, ili kutatua mgogoro huu unaoweza kuhatarisha amani kwa wananchi wa eneo hili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili, tarehe 30 Agosti 2020 amesema kwamba, anafuatilia kwa umakini mkubwa mgogoro ulioibuka huko Mashariki wa Bahari ya Mediterrania, hali inayotishia amani, usalama na utulivu katika eneo hili. Baba Mtakatifu anawasihi wadau wote katika mgogoro huu, kujikita katika mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi, kwa kuheshimu na kuzingatia sheria za kimataifa, ili kutatua mgogoro huu unaoweza kuhatarisha amani kwa wananchi wa eneo hili.

Wachunguzi wa mambo wanabainisha kwamba, katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita kumekuwepo na hali ya “kutunishiana misuri” kati ya Ugiriki na Uturuki. Chimbuko la mgogoro huu ni uwepo wa nishati ya gesi asilia pamoja na kiasi kikubwa cha hifadhi ya mafuta ghafi, yaliyogunduliwa katika miaka ya hivi karibuni katika eneo lenye mgogoro. Hivi karibuni, nchi mbili zilitiliana sahini mkataba kuhusu masuala ya baharini. Uturuki na Libya, ziliwekeana mkataba mwaka 2019 na hivi karibuni Ugiriki na Misri nazo zikawekeana mkataba. Mgogoro mkubwa umezuka baada ya Ugiriki na Uturuki, kila mmoja kudai haki ya kuchimba na kutumia nishati inayopatikana katika eneo hili. Nchi hizi mbili zimekwisha kutuma meli za kijeshi katika eneo husika tangu tarehe 10 Agosti 2020.

Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, EU imekwisha kutoa onyo kwa Uturuki kwamba, itawekewa vikwazo vipya vya kiuchumi, ikiwa kama haitaacha mpango wake wa kuvamia eneo la Ugiriki. Kwa sasa Uturuki inaendelea kufanya mazoezi ya kivita katika eneo hili. Ugiriki inaituhumu Uturuki kwa kutaka kuchimba nishati katika kisiwa cha Kastellorizo, kilichoko umbali wa maili moja kutoka Pwani ya Uturuki kwamba ni kitendo kinachokwenda kinyume cha haki. Huu ni mgogoro mkubwa unaozishirikisha nchi kama Ufaransa na Italia zinazounga mkono Ugiriki. Uturuki inaungwa mkono na Jeshi la Marekani. Uturuki inataka kunufaika pia na nishati inayozalishwa katika eneo hili. Jitihada za Ujerumani kutaka kupata kusuluhisha kwa njia za kidiplomasia hadi sasa zimegonga mwamba. Wanahistoria wanasema kwamba, tangu mwaka 1974 uhusiano kati ya Ugiriki na Uturuki umekuwa “ukichechemea sana” kiasi kwamba, kunako mwaka 1996, nchi hizi mbili zilikaribia kabisa kuingia katika mgogoro wa kivita kwa kugombania kisiwa cha Aegean.

Papa: Vita
31 August 2020, 14:27