Tafuta

Vatican News
2020.08.26 Katekesi ya Papa 2020.08.26 Katekesi ya Papa  (Vatican Media)

Papa Francisko-Katekesi:Hatima ya mali za ulimwengu na fadhila ya matumaini!

Papa Francisko katika mwendelezo wa katekesi kuhusu uponyaji wa ulimwengu,amejikita kufafanua mada ya hatima ya wa mali za ulimwenguni na fadhila ya matumaini.Ameomba kufikiria watoto.Kusoma takwimu,je ni watoto wangapi leo hii wanakufa kwa njaa,ukosefu mzuri wa ugawanaji wa utajiri na kwa sababu ya mfumo wa kiuchumi.Je watoto wangapi leo hii hawana haki ya kwenda shule kwa sababu hiyo?

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mbele ya janga na madhara yake kijamii wengi wako katika hatari ya kupoteza matumaini. Katika wakati huu usio kuwa na uhakika na uchungu ni mwaliko kwa wote kupokea zawadi ya matumani ambayo inatoka kwake Kristo. Ni yeye anayetusaidia kupiga mbizi katika maji yaliyochafuka ya ugonjwa, ya kifo, ya ukosefu wa haki, mambo ambayo haya neno la mwisho katika hatima yetu ya mwisho. Ndivyo Papa Francisko ameanza tafakari yake ya Katekesi, Jumatano tarehe 26 Agosti 2020 ambapo ni mwendelezo wa kutafakari juu ya janga la kutisha la virusi vya corona au COVID-19 akitazama kwa karibu sana jyy ya madhara ya janga hili. Mada ya siku hii ameongozwa na “hatima ya mali za ulimwenguni na fadhila ya matumaini”. Papa Francisko akiendelea amesema majanga yameinua na kuzidisha matatizo kijamii hasa ya ukosefu wa usawa.

Baadhi ya mataifa wanavyo visenti na wengine hawana kukidhi mahitaji muhimu

Baadhi wanaweza kufanyia kazi nyumbani, wakati walio wengi haiwezekani. Badhi ya watoto, licha ya matatizo wanaweza kuendelea kupata elimu ya shule na wakati walio wengi sana hali hii imekatishwa ghafla. Baadhi ya mataifa yenye nguvu wanaweza kuweka hata senti ya kukabiliana na dharura, wakati wengine ina maaana ya kukosa wakati ujao. Dalili hizi za ukosefu  wa usawa zinaonesha ugonjwa wa kijamii. Ni virusi ambavyo vinakuja kutokana na uchumi uliougua,amesisitiza Papa. Ni tunda la kukua kwa uchumi usio sawa ambao unaanzia na thamani msingi za binadamu. Katika ulimwengu wa leo ni matajiri wachache wenye kuwa na ubinadamu zaidi. Ni dhuluma ambayo inalia mbinguni! Wakati huo huo, mtindo huu wa kiuchumi haujali uharibifu uliosababisha na nyumba yetu ya pamoja

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi

Papa Francisko amesema tuko karibu kushinda vizingiti vingi vya maajaribu yetu ya sayari lakini katika madhara mabaya na yasiyoweze kuzibika. Haya ni kuanzia kupotea kwa bayoanuai na mabadiliko ya tabianchi hadi kufikia kupanda kwa kiwango cha juu cha maji ya bahari na uharibifu wa misitu ya kitropiki. Ukosefu wa usawa kijamii na uharibifu wa mazingra vinakwenda sambamba na vyote vina mzizi mmoja (Laudato si 101). Na zaidi ile dhambi ya kutaka kumiliki na kutawala, kaka na dada , maumbile na Mungu mwenyewe. Lakini hiyo siyo ishara ya uumbaji! Papa amebainisha. Tangu mwanzo Mungu aliikabdihi nchi na rasilimali zake katika uendeshaji kwa pamoja wa ubinadamu na ili aweze kivitunza (KKK 2302)Mungu alituomba tutawale nchi kwa jina lake ( Mw 1,28) kulima na kuitunza kama vile bustani ya wote (Mw 2,15). Wakati kulima kuna maanisha juu ya shughuli za kufanya kazi (…) na  kuitunza ikiwa na maana ya  kuilinda, kuangalia na kuhifadhi (LS 67) .

Dunia isitumiwe kama tambara bovu la kufanya utakavyo

Pamoja na hayo Papa Francisko ameonya kwamba “ kuweni makini isije tafsiriwa hiyo kama karatasi nyeupe  kwa ajili ya kuifanya nchi jinsi unavyotaka. Hapana, kwa ni upo uhusiano wa pamoja wa kiuwajibikaji”.  Na hiyo na kati yetu na mazingira. Tunapokea kutoka kwa muumba na hivyo ni wajibu wa kumrudisha yeye kwa mara nyingine tena”. Kila jumuiya inaweza kupata mazao yoyote inayohitaji kutoka ardhini kwa ajili ya kujikimu lakini pia inao wajibu wa kuitunza dunia na kuhakikisha kuwa inaweza kuendelea kuzalisha kwa ajili ya vizazi vijavyo. Nchi inayoongoza na tulipewa, ilitolewa na Mungu kwa binadamu wote ( KKK 24.2.  Kwa maana hiyo wajibu wetu kufanya kwamba matunda yake yanawafikia wote na si kwa baadhi tu. Hili ndiyo jambo msingi na ufunguo wa uhusiano wetu na mali ya nchi.

Kwa kutumia mali hizi lazima kunufaisha wote

Kwa mujibu wa Mababa wa mtagusi wa II wa Vatican unakumbusha kuwa “mtu kwa kutumia mali hizi, lazima afikirie mambo ya nje ambayo kisheria yanamiliki lakini si kama kwamba ni yake bali ya ya pamoja, kwa maana yaweze kunufanisha si yeye pekee lakini hata kwa wengine, (Gaudium et spes 69). Sisi ni wasimamizi wa mali na sio mabwana Papa Francisko amekazia. Wasimamizi ndiyo lakini mali siyo ayngu. Ni kweli  yako, lakini umepewa  kuisimamia, siyo ya kwako binafsi. Ili kuhakikisha kuwa kile tulicho nacho kinaleta faida kwa jamuiya, “mamlaka ya kisiasa ina haki na jukumu la kudhibiti matumizi halali ya haki ya mali katika kufanya kazi kwa ajili ya ustawi wa pamoja (KKK 2406). Kanuni ya umiliki binafsi kuwa chini ya umiliki wa pamoja na haki ya kila mtu kutumia mali ni kanuni msingi ya tabia ya jumuiya na kanuni ya kwanza ya utaratibu wote wa maadili-kijamii (LS 93).

Mali na fedha ni zawadi za kusaidia utume 

Mali binafsi na fedha ni zawadi  ambazo zinaweza kusaidia utume. Lakini itawezakana hivyo ikiwa tubabadilisha kwa haraka kwa ajili ya mambo mengine, ya ubinafsi au upamoja. Na ikiwa hilo linatokea ndipo wanashambulia thamani msingi za ubinadamu. Mtu mwenye hekima anabadilika na kugeuka kuwa aina ya mtu wa kiuchumi kwa maana ya uharibifu, ubinafsi, mwenye kuhesabu na kutawala au mamlaka. Tunasahau kuwa pamoja na kuumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, tunakuwa wajamii, wabunifu na wenye mshikamano, wenye uwezo mkubwa wa kupenda. Kiukweli sisi ni zaidi ya washirikia kati ya aina zote, tunazochagua kwenye jumuiya kama inavyoonekana vizuri katika uzoefu wa watakatifu.

Tamaa ya kumiliki ikiondoa mali za mamilioni ya watu ni hatari kubwa

Ikiwa tamaa ya kumiliki inaondoa mali zilizo msingi za mamilioni ya watu, ikiwa ukosefu wa usawa kijamii na kiteknolojia ni sawa na kururua kiungo cha kijamii, kiukweli  mategemeo ya maendeleo ya zana zilizo finyi zinahatarisha nyumba yetu ya pamoja, kwa maana hiyo basi hatuwezi kukaa na kutazama. Papa Francisko amekazia kusema, hapana hii siyo ya kunyamaza. Kwa njia ya mtazamo wa Yesu ( Eb 12,2 ) na kwa uhakika kuwa, upendo wake unaofanya kazi kwa njia ya jumuiya ya wafuasi wake, lazima tutende wote, kwa matumaini ya kuzalisha lolote tofauti na lililo bora. Matumaini ya kikristo, yaliyosimika mzizi katika Mungu ndiyo nanga yetu. Hayo yanasaidia utashi wa kushirikishana, kukuz utume wetu kama wafuasi wa Kristo ambaye alishirikishana kila kitu na sisi.

Janga limetufanya sisi sote kuwa katika mgogoro

Hta hivyo Papa Francisko kwa kutoa mifano mfano hai amesema haya yaliweza kutambuliwa vema na jumuiya za kwanza za Kikristo ambao kama sisi waliishi kipindi kigumu. “Na jamuiya ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika, wakatoa ushuhuda kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote” (Mdo 4,32-35). Kwa kusisitiza zaidi amesema:Sisi tupo tunaishi mgogoro. Janga limetuweka sisi sote katika mgogoro. Lakini kumbukeni kwamba  kutokana na  mgogoro inawezekana kuondokana tukiwa bado tuko vile vile au kuondokana nao tukiwa bora, au kuondokana tukiwa vibaya. Hii ni chaguo letu. Baada ya mgogoro tutaendelea na mfumo huu wa kichumi na usio wa haki kijamii na kudharau kutunza mazingira na kazi ya uumbaji wa nyumba yetu ya pamoja? Tufikirie! Ni swali la Papa Francisko.

Jumuiya ya kikristo ya karne ya 21 inapewa mwaliko wa kutunza kazi ya uumbaji

Maombi yake Papa Francisko ni kwamba Jumuiya  za Kikristo ya karne ya ishirini na moja iweze   kurudia kweli  katika hali halisi ya kutunza kazi ya uumbaji na hali kijamii mambo ambayo yanakwenda sambamba kama chanda na pete kushuhudia ufufuko wa Bwana. Ikiwa tutatunza mali ambazo Muumba wetu  hutupatia, ikiwa tutaweka kwa pamoja  kile tulicho nacho  kwa njia ambayo hakuna mtu anayekosa, basi tutaweza kuhamasisha kiukweli tumaini ili  kuzalisha kwa upya ulimwengu wenye afya na usawa zaidi. Kwa kuhitimisha Papa ameongeza kusema “Tukifikirie watoto. Someni takwimu: ni watoto wangapi leo hii wanakufa kwa njaa kutokana na ukosefu mzuri wa ugawaji wa utajiri, kwa sababu ya mfumo wa kiuchumi; ni watoto wangapi leo hii hawana haki ya kwenda shule kwa sababu hiyo hiyo. Picha hii ya watoto wenye kuhitaji kutokana na njaa na ukosefu wa elimu itusaidie kutambua kuwa baada ya mgogoro huu lazima tutoke tukiwa bora”.

26 August 2020, 14:00