MEXICO:Kumbu kumbu ya mauaji ya watu 72 nchini Mexico MEXICO:Kumbu kumbu ya mauaji ya watu 72 nchini Mexico  

Papa asali kwa ajili ya wanaoteswa kwa sababu ya imani na kwa ajili ya wahamiaji!

Mara baada ya sala na tafakari ya Malaika wa Bwana,Papa Francisko amekumbusha siku ya kimataifa kuhusiana na vurugu dhidi ya dini au imani iadhimishwayo kila tarehe 22 Agosti.Amekumbusha siku ya kumbukizi la mauaji ya wahamiaji 72 nchini Mexico.Mawazo yake na ukaribu pia kwa watu wa Capo Delgado nchini,Msumbiji wanaoteseka kwa sababu ya ugaidi wa kimataifa

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari na sala ya malaika wa Bwana Jumapili tarehe 23 Agosti 2020, Papa Francisko amewageukia waamini na mahujaji wote kuwakumbusha kuhusu siku ya kimataifa ya matendo ya vurugu dhidi ya dini au imani inayoadhimishwa kila tarehe 22 ya kila mwaka. Kwa maana hiyo ameomba kusali kwa ajili ya ndugu kaka na dada na kuwaalika kwa sala na mshikamano kwa maana ni wengi leo hii ambao wanateswa kwa sababu ya imani yao ya kidini.

Mexico:wahamiaji ni waathirika wa utamaduni wa kibaguzi

Tarehe 24 Agosti, ni siku ya kukumbuka mauaji ya wahamiaji sabini na mbili wa huko Mtakatifu Fernando, Tamaulipas, nchini Mexico ambapo Papa Francisko amesisitizia juu ya haki na ukweli katika mantiki hiyo.“ Walikuwa wakitafuta maisha bora, anasema Papa huku akielezea mshikamano wake wote na familia na kwamba “Walikuwa watu kutoka nchi tofauti ambao walikuwa wakitafuta maisha bora. "Ninaonesha mshikamano wangu na familia za wathiriwa ambao hadi leo wanatafuta haki na ukweli juu ya kile kilichotokea. Bwana atatuuliza  kuhusiana na  wahamiaji wote ambao wamefia kwenye safari za tumaini na ambao wamekuwa waathiriwa wa utamaduni wa ubaguzi".

Wahamiaji walikuwa wa mataifa tofauti

Siku hii inakumbusha tarehe 24  Agosti 2010 ambao ilipatikana miili ya wahamiaji 72 nchini Mexico ya Kati kwa kuongozwa na kijana mmoja wa taifa la Equador aliyepata fursa ya kutoroka. Kati ya wale waliotambuliwa ilikuwa ni miili ya watu wa taifa la Honduras, Salvador, Guatemala, Equador, Brazil na mtu kutoka India. Kiasi hiki cha juu cha dhuluma inabainisha kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Msumbiji: Ukaribu wa Papa kwa watu wa Capo Delgado

Papa Francisko akiendelea na kumbu kumbu hizi kadhaa, amekumbuka hata waathirika wa mateso huko Kaskizini mwa Msumbiji, mahali ambapo ugaidi wa kimataifa unaendelea kusababaisha hali mbaya ya  mamia ya watu kurundikana. Na kama livyokuwa amefanya Jumatano iliyopita kwa simu ya mshangao kwa Askofu wa Pemba nchini Msumbiji, Papa Francisko amerudia kuonyesha ukaribu wake wote  wa nchi ya Msumbiji ambayo inazidi kuwa hali  mbaya ya kibinadamu katika mkoa wa kaskazini wa Capo Degado. “Napenda kurudia kuonyesha ukaribu wangu kwa watu wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, wanaoteseka kwa sababu ya ugaidi wa kimataifa. Bado ninazo kumbukumbu zilizo  wazi ya ziara niliyofanya katika nchi hiyo pendwa karibu mwaka mmoja uliopita”. Papa amebainisha.

Mateso ya watu na mlundikano

Hata hivyo kama alivyo kuwa amemwambia tayari Askofu  Fernando Lisboa, Papa Francisko amekumbuka ziara yake ya kwenda Msumbiji na jinsi hali ilivyo katika eneo hilo, tajiri na  mali za asili,lakini wakati huo huo bado ni ngumu, hasa tangu Machi iliyopita, ambapo kumejitokeza mashambulizi yaliyo sababishwa na vikosi vyenye silaha ambavyo shughuli zao zinaongezeka zaidi kuwa chanzo cha wasiwasi  mkubwa  hata kwa nchi majirani. Vurugu za Cabo Delgado zimeibua mazingira ya kero kati ya watu na kusababisha waathiriwa wengi na maelfu ya watu waliohamishwa katika makazi na ambao tayari ni maskini na waliotengwa.

23 August 2020, 13:24