Tafuta

Vatican News
PANAMA-AFYA -VIRUSI PANAMA-AFYA -VIRUSI  (AFP or licensors)

Panama:Vimekabidhiwa vipima joto kwa ajili ya watu asilia,wahamiaji na wafungwa!

Kufuatia na janga la corona linaloendelea,zawadi kutoka kwa Papa imekabidhiwa kwa Serikali ya Panama ambavyo ni vipima joto vya kidigitali kwa ajili ya wahamiaji,watu asilia na wafungwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Vipima joto vya kidigitali  kwa ajili ya jumuiya ya watu wa asilia, wahamiaji na wafungwa ndiyo kwa mara nyingine zawadi kutoka kwa  Papa Francisko kwa Jimbo Kuu Katoliki la Panama, Amerika ya Kati, na vifaa hivyo vilivyowasili na kukabidhiwa moja kwa moja kwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje Bwana Alejandro Ferrer, kutoka kwa Askofu Mkuu José Domingo Ulloa na uwakilishi wa mahusiano ya kitaasisi kutoka ofisi ya Balozi wa kitume padre Gilber Tsogli.

Uchaguzi wa watu maskini

Kwa ishara hii, Papa ameonesha kwa mara nyingine tena uchaguzi  kwa ajili ya wadhaifu zaidi na kuiweka Panama katika moyoni mwake, kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki akizungumza nje ya mkutano huo.  Aidha amesema, wahusika wa vifaa hivyo wako hatarini na wanaweza kuugua kwa sababu ya mlundikano mkubwa na matatizo ya huduma msingi, Askofu Mkuu Ulloa aidha analaumu kwa namna ya pekee  matatizo makubwa yaliyomo kwenye magereza. Kwa mfano katika magereza ambayo leo hii wanahesabu wafungwa 17.800, miongoni mwao wenye maambukizi ni 665 kwa mujibu wa vyombo vya habari visivyo vya kiserikali. Hata hivyo takwimu hizo ni za tarehe 4 Juni na kwa maana hiyo hadi leo kuna ongezeko kubwa.

Askofu Mkuu aidha amesema “Tunajua pia kuwa katika gereza la Santiago huko Veraguas, wafungwa 313 kati ya 500 wamonesha dalili za  virusi. Mmoja wao alikufa ”. Hali ya wasiwasi sana pia ni kwa ajili ya  wahamiaji: kwani “huko Darién kuna vituo viwili vya mapokezi vyenye msongamano ambapo Covid inazungukia humo”. Moja ya hali mbaya zaidi ni kituo cha  Peñita, ambapo mwezi Mei walikuwa ni watu 1,694 na  walikuwa au mara saba ya kiwango cha kukaa  ndani humo. Hatimaye wenyeji wa asilia “ambao wanawakilisha asilimia 11 ya wakazi  wote na karibu milioni nne, kwa mujibu wa Askofu mkuu wa Panama wanaishi katika maeneo matano ya nchi ambayo ni magumu sana kufikia. Hata pale  pia maambukizi yanaendelea.

29 August 2020, 12:07