Tafuta

Vatican News
2020.08.28 zawadi kutoka kwa Papa imefika katika hospitali ya Porto Alegre, nchini  Brazil 2020.08.28 zawadi kutoka kwa Papa imefika katika hospitali ya Porto Alegre, nchini Brazil 

Brazil:Hospitali imekabidhiwa mashine za kupumulia kutoka kwa Papa

Hospitali ya Mtakatifu Luca ya Porto Alegre nchini Brazili imepokea baadhi ya vifaa vya matibabu vilivyotumwa kwa niaba ya Papa Francisko kwa ajili ya shughuli zinazoendelea za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa niaba ya Papa Francsiko, tarehe 17 Agosti 2020 zimetumwa nchini Brazil mashine 18 aina ya Graeger  za kupumlia kwenye vyumba vya mahututi  pamoja na  mashine 6 za ultrasound (aina ya fuji), na ni zawadi ambayo sasa imefika. Vifaa vya kupumulia mapafu na mashine ya uchunguzi katika maabara vimefikishwa katika hospitali ya Mtakatifu Lucas huko Porto Alegre, katika mkoa wa  Rio Grande do Sul. Ni moja ya zawadi nyingi kama hizo ambazo Papa Francisko amekwisha toa katika miezi ya hivi karibuni kwa nchi zilizoathiriwa na janga la covid-19 na nchini Brazil ni kati ya zile ambazo kwa muda mrefu zimepata athari nzito ya virusi  kwa idadi  kubwa ya watu.

Umakini kwa wasio na fursa

Utume wa kutoa msaada wa kibinadamu umeonekana wazi katika jitihada za Mfuko wa Kitume  Vatican pamoja na ule wa  chama cha Tumaini  kisicho cha kiserikali nchini. Katika miji tofauti ya Brazil wanaendelea kupokea vifaa na zana mbali mbali na wakati huo huo Askofu Mkuu Jaime Spengler wa mji wa Porto Alegre, amebariki vifaa vilivyo kabidhiwa katika hospitali ya kizalendona kusisitiza kwamba ishara hiyo ni kielelezo cha mshikamano wa wanaume na wanawake wanaotaabika kutokana na maisha yasiyo na fursa.

Msaada wa kulinda maisha

Mashine za kupumulia  na ultrasound vitawekwa katika  kitengo cha wagonjwa mahututi, ambacho kinapokea wagonjwa walio na Covid-19 tu. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Kipapa cha Rio Grande do Sul (PUCRS), Padre  Evilázio Teixeira, aliyekuwapo wakati wa uwasilishaji wa vifaa hivyo amesema ni ishara  ya mshikamano kwa upande wa Kanisa ni muhimu kutoa nguvu kwa utume wao  wa  utunzaji na kuhamasisha maisha.

Mkoa  Rio Grande do Sul

Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Shirikisho la Rio Grande do Sul (UFRGS), kilichochapishwa Jumanne iliyopita, unaonyesha kwamba pigo la maambukizi ya Covid-19 hata hivyo  katika mji wa Porto Alegre umepungua, lakini mwenendo wa kesi lazima uendelee kudhibitiwa. Hadi leo hii  katika mkoa huo ni watu 115,000 walioambukizwa na vifo zaidi ya elfu tatu wa virusi vya corona!

28 August 2020, 14:26