Vatican News
Mazishi ya Monsinyo Georg Ratzinger, Kaka yake Mkubwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI yanatafanyika tarehe 8 Julai 2020 kwenye Kanisa kuu la Regensburg, Ratsbon, Ujerumani. Mazishi ya Monsinyo Georg Ratzinger, Kaka yake Mkubwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI yanatafanyika tarehe 8 Julai 2020 kwenye Kanisa kuu la Regensburg, Ratsbon, Ujerumani.  (Vatican Media)

Salam za Rambirambi kwa Papa Mstaafu Benedikto XVI

Baba Mtakatifu anamshukuru Papa Mstaafu Benedikto XVI kwa kupatia kipaumbele na hivyo kuwa mtu wa kwanza kabisa kuweza kumfahamisha juu ya msiba mzito uliokuwa umemkumba kwa kuondokewa na kaka yake mpendwa! Ibada ya mazishi ya Monsinyo George Ratzinger itafanyika kwenye Kanisa kuu la Regensburg huko Ratsobn, Ujerumani tarehe 8 Julai 2020: Saa 4:00 Asubuhi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Papa Francisko amemtumia salam za rambirambi Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kufuatia kifo cha kaka yake mkubwa Monsinyo Georg Ratzinger kilichotokea Jumatano tarehe 1 Julai 2020, huko nchini Ujerumani, akiwa na umri wa miaka 96. Baba Mtakatifu anamshukuru Papa Mstaafu Benedikto XVI kwa kupatia kipaumbele na hivyo kuwa mtu wa kwanza kabisa kuweza kumfahamisha juu ya msiba mzito uliokuwa umemkumba kwa kuondokewa na kaka yake mpendwa! Baba Mtakatifu Francisko anapenda kumwonesha uwepo wake wa karibu kwa njia ya maisha ya sala na maisha ya kiroho katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Papa Francisko anapenda kumhakikishia sala zake, katika kipindi cha maombolezo makubwa, ili Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo, aweze kumpokea kwenye makao ya uzima wa milele mbinguni, ambako amewaandalia watumishi waaminifu wa Injili. Baba Mtakatifu Francisko anapenda kumhakikishia Papa Mstaafu Benedikto XVI sala zake mbele ya Mwenyezi Mungu, ili kwa maombezi ya Bikira Maria, Mama wa matumaini ya Kikristo, aweze kumwombea faraja kutoka mbinguni. Baba Mtakatifu anahitimisha salam zake za rambirambi kwa Papa Mstaafu Benedikto XVI kwa kusema kwamba, wako wanaendelea kuungana pamoja chini ya Kristo Mfufuka, chemchemi ya matumaini na amani! Taarifa rasmi inaonesha kwamba, Ibada ya mazishi ya Monsinyo Georg Ratzinger itafanyika tarehe 8 Julai 2020 kwenye Kanisa kuu la Regensburg, huko Ratsbon, Ujerumani kuanzia saa 4: 00 kwa Saa za Ulaya. 

Papa: Rambirambi
02 July 2020, 13:58