Tafuta

2020.07.05 Sala ya Malaika wa Bwana 2020.07.05 Sala ya Malaika wa Bwana  

Papa Francisko:Waamini na wenye mapenzi mema wasaidie wenye kuhitaji!

Wakati wa tafakari ya Papa Francisko kabla ya Malaika wa Bwana tarehe 5 Julai 2020 amekumbusha kuwa hata leo hii Yesu anawataka waamini na watu wenye mapenzi mema kuwa wapole na wanyenyekevu kama Yeye ili kuwasaidia na kuwashibisha maskini ambao Kanisa limeitwa kuinjilisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Somo la Injili ya Dominika hii kutoka(Mt 11,25-30) limejikita katika sehemu tatu. Awali ya yote, Yesu anatoa wimbo wa baraka na shukrani kwa Baba yake kwa sababu amejionesha kwa maskini na walio rahisi mafumbo ya Ufalme wa Mbingu; baadaye anafunua uhusiano wa kweli na wa pekee uliopo kati yake na Baba yake; na mwisho anawaalika kwenda kwake na kumfuata ili kupata nafuu. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Papa Francisko Jumapili tarehe 5 Julai 2020 kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro.  “Busara ya kweli inakuja hasa kutoka katika moyo na siyo kutoka tu katika mawazo. Busara ya kweli inaingia hasa katika moyo. Na ikiwa unajua mambo mengi na una moyo uliofungwa, wewe siyo mwenye busara”.

Yesu anawafunulia siri za ufalme watoto

Papa Francisko akianza kufafanua sehemu hizo kwanza   anasema Yesu anamshukuru Baba kwa sababu ameficha siri za Ufalme wa ukweli zilizofichwa kwa wenye hekima na akili (Mt 11,25).  Mafumbo ya Baba yake, Yesu anawafunulia watoto, yaani wale ambao wanamfungulia matumaini katika Neno la wokovu, wanahisi uhitaji wake na kusubiri kila kitu kutoka kwake. Moyo ulifunguliwa na wenye imani kwa Bwana. Baadaye Yesu anaelezea alivyopokea kutoka kwa baba yake kila kitu. Anamwita “Baba yangu” ili kudhihirisha muungano wa uhusiano na Yeye. Kiukweli kati ya Mtoto na Baba kuna uhusiano kamili. Mmoja anamfahamu mwingine na mwingine anaishi kwa ajili yake. Lakini muungano huo mmoja ni kama ua linapochanua ili kuonesha uzuri wa zawadi yake ya bure na wema wake. Na ndiyo tazama mwaliko wa Yesu ni huu “njooni kwangu ninyi nyote msumbukao (Mt 11,28). “Yeye anataka kujitoa kama anavyoichota kutoka kwa Baba yake.  Anataka kutupatia Ukweli na ukweli wa Yesu daima ni wa bure. Ni zawadi, ni Roho Mtakatifu, yaani  Ukweli”.

Baba apendezwaye na watoto ndivyo Yesu kwa walioelemewa

Papa Francisko aidha anasema Baba apendezwaye na watoto, ndivyo hata Yesu anavyowaelekeza  “walioelemewa na mizigo na kusumbuka”. Na zaidi anajiweka Yeye binafsi kati yao kuwa Yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo (Mt 11,29). Na ndiyo anajieleza hivyo. Ni kama ilivyo katika heri ya kwanza na ya tatu, ile ya unyenyekevu au maskini wa roho; na ile ya wapole (Mt 5,3.5) yaani upole wa Yesu. Yesu anaishi yote hayo kwa ukamilifu wa Baba na kwake yeye anachota mafundisho yake anayoita ‘nira’ kama ilivyokuwa ikitumia kuitwa wakati ule wa Sheria na walimu tofauti. Yeye lakini anahaidi nira iliyo laini (Mt 11,33) kwa sababu mbili, kwanza inatoka kwa Mungu Baba na pia kwa sababu Yeye mwenyewe yuko chini ya nira hiyo, ili kuibeba pamoja na sisi. Kwa maana hiyo Yesu mpole ni mnyenyekevu siyo mtindo wa kujikabidhi na wala kuwa mwathirika kirahisi, badala yake ni mtu ambaye anaishi kwa moyo katika hali halisi ya uwazi kamili wa upendo wa Baba kwa maana ya Roho Mtakatifu. Yeye ni mtindo wa maskini wa roho na heri nyingine zote zilizopo katika Injili ambazo zinatimiza mapenzi ya Baba na zinashuhudia Ufalme wake.

Furaha ya mapumziko ni Yesu mwenyewe

Mapumziko ambayo Kristo anatoa kwa wasumbakao na kuelemewa na mizigo ni kitulizo cha kisaikolojia na sadaka iliyokubalika japokuwa furaha kwa maskini ni kwa sababu ya kuinjilishwa na kuwa wajenzi wa ubinadamu mpya. Papa Francisko amesisitiza furaha ya mapumziko anayotupatia Yesu ni furaha ya pekee ambayo ndiye yeye mwenyewe. Ni ujumbe kwa ajili yetu sisi sote na kwa watu wenye mapenzi mema, ambao Yesu anawalekeza leo hii katika Dunia ambayo inajionesha zaidi na wanaojifanya matajiri na wenye nguvu… lakini ni mara ngapi tunasema “ mimi ninataka kuwa kama  huyo na kama  yule, ambaye ni tajiri, mwenye nguvu sana na ambaye hakosi kitu…” Ulimwengu unamsifia tajiri na mwenye nguvu na wala haujali ni kwa zana zipi na wakati mwingine hata kukanyaga utu wa  binadamu  na hadhi yake. Haya yote sisi tunayaona siku zote Papa Francisko amesisitiza, kwa maskini waliokanyagwa…  Ni ujumbe kwa ajili ya Kanisa ambalo linaalikwa kuishi matendo ya huruma na uinjilishaji kwa maskini na kuwa na upole na unyenyekevu. Na ndiyo Bwana anataka liwe Kanisa lake yaani sisi.

Mama maria atuombee kuwa na hekima ya roho

Papa Francisko amehitimisha kwa kuseam Maria, mnyenyekevu zaidi na kiumbe wa hali ya juu zaidi, atuombee kwa Mungu kuwa na hekima ya roho ili tuweze kujua kung’amua ishara zake katika maisha yetu na kuweza kushiriki yale mafumbo ambayo yamefishwa kwa wenye kiburi  na kuwafunulia hekima wanyenyekevu.

05 July 2020, 13:33