Papa Francisko na wazee babu na bibi. Papa Francisko na wazee babu na bibi. 

Papa Francisko:sala ya Yohakimu na Ana ni kisima na mlango wa Maria!

Tarehe 26 Julai Mama Kanisa anawakumbuka wazazi wa Bikira Maria,babu zake Yesu.Hawa ni watakatifu Yohakimu na Ana ambapo mara nyingi Papa Francisko amekuwa akikumbusha kuhusu wazee kuwa ni zawadi ya Kanisa.Ni hekima kubwa hata katika jamii ya kibanadamu hasa kwa ile ambayo imezungukwa na mambo mengi ya kufanya hata kujisahau.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Babu ni kumbu kumbu ya watu na wazee ni kama miti ambayo inaendelea kuzaa matunda. Papa Francisko tangu aanze utume wake kama Papa amekuwa akikumbusha mara nyingi juu ya hilo na hata kumkumbuka mwanamke mmoja ambaye alimwonyesha ishara muhimu za mchakato wa safari yake ya imani.  Kwa maneno yake anasema,“alikuwa hasa bibi yangu, mama mzazi wa baba” ambaye iliimarisha  safari yangu ya imani. Alikuwa ni mwanamke anayesimulia mambo ya Yesu na alikuwa anatufundisha katekisimu. Ninakumbuka daima siku ya Ijumaa Kuu ambayo alikuwa anatupeleka kwenda kwenye  maandamano ya mishumaa usiku na baada ya maandamano hayo yalimfikia Yesu aliyekuwa amelazwa na bibi alikuwa anatuomba sisi watoto tupige magoti, na alikuwa anatuleza kwamba “tazameni amekufa  lakini kesho atafufuka”. Kwa maana hii nilipokea tangazo la kwanza la kikristo kutoka kwa mwanamke huyu, ni  bibi yangu”, alisema Papa Francisko wakati wa mkesha wa  Pentekoste tarehe 18 Mei 2013. 

Sala ya babu ni zawadi

Babu na bibi mara nyingi ni nguvu ya injini ya kurithisha imani. Shukrani kwao, zawadi hii inaendelea kurithishwa kizazi hadi  kizani na katika upendo wa familia. Kwa mfano   Mtakatifu Paulo akimwelekea Timeteo anaandika “ kumbuka imani yako thabiti ambayo uliipokea kutoka kwa bibi Loide  na mama yako Eunice”.  Maneno na mafundisho ya babu na bibi pia ni njia kwa ajili ya kutangaza kila mahali Neno la Mungu. “Babu na bibi ni zawadi kubwa hata kwa  ajili ya Kanisa. Sala za wazee na babu na bibi ni zawadi na ni utajiri,  alisisitiza Papa Francisko tena katika Katekesi yake tarehe 11 Machi 2015.  Ni hekima kubwa hata katika jamii ya kibandamu hasa kwa ile ambayo imezungukwa na mambo mengi ya kufanya na kujisahau.

Maneno ya wazee yana jambo muhimu

“Maneno ya babu na bibi yana jambo fulani maalum kwa vijana. Na wao wanatambua hilo. Maneno ambayo bibi yangu aliyonikabidhi kwa maandishi katika siku ya upadirisho wangu, hadi leo ninazunguka nayo kwenye kitabu changu cha sala na mara nyingi ninayarudia kusoma” alisema hivyo akifafanua umuhimu wa naafsi ya wazee.(Papa Francesco Umuhimu wa nafasi ya wazee ,katekesi tarehe 4-03-2015)

Johakimu na Ana

Hata wazazi wa Mama Maria, Johakimu na Ana ni sura za kutafakari kwa ajili ya kupyaisha mtazamo juu ya wito wa uzee. Jina Ana linatokana na neno la Kihebrania ‘Hannah’maana yake ‘neema’, wakati Yohakimu kwa kihebrania “Yule aliyeinuliwa na nguvu ya Mungu”. Mzee huyo anaheshimiwa kama baba wa Bikira Maria na babu wa Yesu kadiri ya mapokeo ya Ukristo na Uislamu, ingawa hatajwi katika Biblia isipokuwa katika kitabu cha karne ya 2 kinachoitwa Injili ya Yakobo na vingine vilivyofuata. Humo anatajwa pia mke wake Ana. Wote wawili wanaheshimiwa kama watakatifu katika madhehebu mengi ya kiristo,na shereha yake ni tarehe 26 Julai ya kila mwaka.

Sala kwa ajili ya watu wa Uturuki

Watakatifu hawa wawili hawakuwa na watoto kwa zaidi ya miaka 20 kadiri ya mapokeo hayo. Ana alitumia muda wake akiomba Mungu neema ya kuwa mama. Wakati alikuwa ndani ya nyumba anasali, aliona katika kona akitokea malaika na kumtangazia. Ana Ana Bwana amesikiliza sala zako na wewe utachukua mimba na kumzaa mtoto ambaye atazungumza katika ulimwengu wote. Anna akamzaa Maria. Mtoto akakulia katika upendo mkuu wa baba na mama wakiwa makini sana. Maria alipotimiza miaka miatatu, Baba yake na Mama yake walimpeleka katika hekalu kwa ajili ya kutoa shukrani.

25 July 2020, 15:50