Migogoro bado inaendelea ya Armenia na Azerbaijani Migogoro bado inaendelea ya Armenia na Azerbaijani  

Papa Francisko:Maombi kwa ajili ya amani ya kudumu huko Caucaso!

Kwa mujibu wa azimio la hivi karibuni la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Papa amesasisha wito wa kuzimisha moto wa ulimwengu na mara moja.Anafuatilia kwa wasiwasi kuhusu machafuko mapya na mivutano ya silaha katika mkoa wa Caucaso kati ya Armenia na azerbaijani.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika kipindi hiki ambacho janga la virusi bado halisimami, ninapenda kuwahakikishia ukaribu wangu kwa wale wote wanaokabiliana na ugonjwa na matokeo ya kiuchumi na kijamii. Wazo langu linawaendea kwa namna ya pekee  watu ambao mateso yao yanazidi kuongezeka kutokana na hali ya migogoro. Ndilo wazo la Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili, tarehe 19 Julai 2020 kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican.

WITO WA PAPA BAADA YA SALA YA MALAIKA WA BWANA

Papa Francisko akiendelea amesema kuhusiana na “Azimio la hivi karibuni la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ninasasisha wito wa kusitisha mapigano ulimwenguni na mara moja, ambayo inaruhusu amani na usalama muhimu wa kutoa msaada muhimu wa kibinadamu. Papa Francisko aidha emeongeza kusema  mesema “Nafuatilia kwa wasiwasi juu ya kuongezeka kwa mvutano wa silaha katika mkoa wa Caucaso kati ya Armenia na Azerbaijani katika siku za hivi karibuni. Wakati nikiwahakikishia maombi yangu, kwa familia za wale waliopoteza maisha wakati wa mapigano ni matumaini kwamba, kwa jitihada za jumuiya ya kimataifa na kupitia mazungumzo na utashi mwema  wa vyama vyote wanaweza kupata suluhisho la amani ya kudumu na kuwafikiria kwa moyo wote watu wapendwa”. Na hatimaye amewasalimia mahujaji na waamini  wote kutoka Roma na sehemu zote za Italia na nchi nyingine. Amewatakia Dominika  njema na wasisahu kusali kwa ajili yake.

 

20 July 2020, 07:43