Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Ibada ya Buriani kwa Kardinali Grocholewski Zenon, Mwenyekiti Mstaafu Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki. Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Ibada ya Buriani kwa Kardinali Grocholewski Zenon, Mwenyekiti Mstaafu Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki. 

Papa Francisko Aongoza Ibada ya Buriani kwa Kardinali Zenon

Kwa kifo cha Kardinali Zenon Grocholewski, (11 Oktoba 1939 hadi 17 Julai 2020” kwa sasa Baraza la Makardinali linaundwa na Makardinali 221 kati yao kuna Makardinali 122 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Makardinali wengine 99 wamekwisha kupoteza haki ya kupiga na kupigiwa kura wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Papa mpya!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki ambaye pia ni Makamu wa Dekano wa Baraza la Makardinali, Jumamosi tarehe 18 Julai 2020 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, ameongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumkumbuka na kumwombea Marehemu Kardinali Zenon Grocholewski aliyefariki dunia mjini Roma akiwa na umri wa miaka 81. Mara baada ya Misa Takatifu, Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Sala ya Mwisho na Ibada ya Buriani “Ultima Commendatio & Valedictio”. Kwa kifo cha Kardinali Zenon Grocholewski, (11 Oktoba 1939 hadi 17 Julai 2020” kwa sasa Baraza la Makardinali linaundwa na Makardinali 221 kati yao kuna Makardinali 122 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Makardinali wengine 99 wamekwisha kupoteza haki ya kupiga na kupigiwa kura wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro kutokana na umri wao kuwa mkubwa zaidi. Wakati huo huo, Askofu mkuu Stanisław Gądecki, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Poland, kwa niaba ya familia ya Mungu nchini Poland anapenda kuungana na waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuomboleza kifo cha Kardinali Kardinali Zenon Grocholewski, kilichotokea tarehe 17 Julai 2020 mjini Roma. Askofu mkuu Stanisław Gądecki, anawaalika watu wa Mungu popote pale walipo kumkumbuka na kumwombea, ili Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo, aweze kumpokea miongoni mwa watakatifu wake, amjalie mwanga wa milele ili aweze kupumzika kwenye usingizi wa amani. Amina.

Kardinali Zenon: Maziko
18 July 2020, 14:02