Tafuta

Vatican News
Kanisa la Kabinda nchini Congo DRC limepata Askofu Mpya Padre Félicien Ntambue Kasembe,C.I.C.M., Kanisa la Kabinda nchini Congo DRC limepata Askofu Mpya Padre Félicien Ntambue Kasembe,C.I.C.M.,  

CONGO DRC:Padre Félicien NTAMBUE,C.I.C.M ni askofu mpya jimbo la Kabinda

Mhs.Sana Padre Félicien Ntambue Kasembe,C.I.C.M.,alizaliwa tarehe 8 Sepremba 1970 ambaye ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Kabinada nchini Congo DRC

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amemteua Askofu wa Jimbo katoliki la Kabinda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mheshimiwa sana Padre Félicien NTAMBUE KASEMBE, C.I.C.M., ambaye hadi uteuzi wae alikuwa ni mshauri wa Shirika la Moyo safi wa  Bikira Maria, C.I.C.M.(wamisionari wa Scheut). Padre Félicien Ntambue Kasembe, C.I.C.M., alizaliwa tarehe 8 Sepremba 1970 huko Kabinda, wilaya ya  Lomami.

Kunako mwaka 1988 alipata Diploma ya Biolojia na Kemia. Aliingia kwenye unovizi katika Shirika la  Mapadre wa Scheut huko Mbudi kunako (1989-1990).  Masomo yake ya Falsafa katika Seminari ya Mtakatifu Pierre Canisius wa Kinshasa (1990-1993). Kwa kipindi alifanya uzoefu wa kimisionari na kichungaji nchini Taiwan, Hong Kong, Singapore na Mongolia kunako (1993-1996). Alifunga nadhiri za milele kunako mwaka 1996. Masomo ya Taalimungu alifanyia nchini Ufillipino na Camerun mwaka  (1996-2001). Na alipewa daraja la Upadre kunako tarehe 12 Agosti 2001 huko Kabinda.

23 July 2020, 14:28