"Uwape kwa ukarimu maskini (Sir 7,32)ndiyo kauli mbiu ya Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Maskini Duniani 2020 "Uwape kwa ukarimu maskini (Sir 7,32)ndiyo kauli mbiu ya Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Maskini Duniani 2020  

Uwape maskini kwa ukarimu ndiyo mada ya Ujumbe wa Papa wa Siku ya Maskini Duniani 2020!

Wape maskini kwa ukarimu ni mada inayoongoza ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Maskini duniani 2020.Vifungu kumi vya ujumbe huu vinafafanua jinsi ya kuwa karibu na maskini ambao Mungu anajitambulisha sura yao.Ujumbe unakumbusha kipindi cha janga,wahudumu wa afya wakiwa mstari wa mbele kuwa mashuhuda.Onyo kwa wenye sintofahamu,kutengeza silaha,ufisadi.Mgogoro wa uchumi,kifedha na kisiasa hautaisha ikiwa hakuna utambuzi wa uwajibikaji kwa wengine na kila mtu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican  

Jumamosi tarehe 13 Juni 2020 ambapo Mama Kanisa anakumbuka siku kuu ya Mtakatifu Antoni wa Padua, umetangazwa ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya IV ya Maskini Duniani” itakayoadhimisha katika Dominika ya XXXIII ya kipindi cha kawaida cha mwaka  tarehe 15 Novemba 2020. Ujumbe wa Papa unaongozwa na kauli mbiu  kutoka kitabu cha Sira kifungu kisemacho “Wape maskini kwa ukarimu ( rej Sir 7,32). Papa Francisko akianza na ujumbe  huo amebainisha kuwa hekima ya kizamani inatupatia maneno hayo kama kanuni takatifu ya kufuata katika maisha. Leo hii maneno hayo yanasikika kwa nguvu zake zote kwa maana ya kusaidia hata sisi kujikita kwa kina katika mtazamo juu ya kile ambacho ni msingi na kushinda vizingiti vya sintofahamu. Umasikini unajitokeza daima katika sura nyingi ambazo zinahitaji umakini kwa kila hali kwa namna ya pekee, kwa kila mmoja ya hawa ambamo tunaweza kukutana na Bwana Yesu ambaye alijionesha uwepo wake kwa ndugu zake walio wadhaifu zaidi (rej Mt 25,40).

Tufunue kitabu cha sira.Hekima inawafanya watu wawe bora zaidi

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya Maskini duniani, ameufafanua katika vipengele kumi, kwa maana hiyo katika kipengele cha kwanza anasema tushike mikononi mwatu kitabu cha Sira, mojawapo  ya vitabu vya Agano la Kale. Hapa tunakutana na maneno ya mwalimu wa busara aliyeishi karibu miaka miambili kabla ya Kristo. Yeye alikuwa akienda kutafuta hekima ambayo inawafanya watu wawe bora zaidi na wenye uwezo wa kuingia kwa undani  kuhusu matukio ya maisha. Alifanya hivyo wakati wa kipindi cha majaribu ya watu wa Israeli, kipindi cha uchungu, maombolezo na taabu kubwa kutokana na utawala wa mabavu ya wageni. Kwakuwa alikuwa ni mtu wa imani kubwa, yenye  mzizi wake katika  utamaduni wa mababa, wazo lake lilikuwa ni kumwelekea Mungu ili kuomba zawadi ya hekima kutoka kwake  Bwana hakuacha kumpatia msaada wake. Tangu sura za kwanza za kitabu cha Hekima ya  Sira, kinaonesh ushauri wake juu ya mambo halisi ya hali ya maisha, na umaskini ndiyo mojawapo ya  hayo.  Yeye anasisitiza hasa kutokana na kwamba wakati wa shida kuna haja ya kuwa na imani kwa Mungu. “Usiangaike wakati wa taabu  ambatana na Bwana wala usimwache kamwe, nawe utafanikwa mwishoni mwa  maisha yako. Uyapokee yote yatakayokupata hata ukiabishwa uwe na uvumilivu, kwa maana dhahabu hujaribiwa kwa moto na watu wanaokubaliwa na Mungu kwa tanuru ya aibu. Mtegemee Mungu naye atakusaidia, shika njia nyoofu na kumtumaini yeye. Enyi mnaomcha Bwana ngojeeni huruma yake, msigeuke upande, msije mkaanguka. (rej Sir 2,2-7)”.

Kusoma kurasa baada ya kurasa kuna thamani ya ushauri.Sala na jirani

Katika kifungu cha pili anaendelea kusema Papa Francisko kuwa kurasa baada ya ukurasa, tunagundua thamani kubwa iliyopo ya ushauri wa jinsi ya kutenda katika mwanga wa uhusiano wa kina na Mungu muumbaji na anayependa maisha, mwenye haki na anayewajali watoto wake. Akiwa thabiti katika Mungu haimwondolei kutazama mtu kwa uhalisia na udhaifu wake, kinyume chake, mambo hayo mawili yanasukana. Inaonesha wazi katika kifungu cha kauli mbiu ya ujumbe “Wape maskini kwa ukarimu(rej Sir 7,29-36).  Sala kwa Mungu na mshikamano kwa maskini na wanaoteseka ni mambo mawili yasiyotenganishwa. Ili kuweza kuadhimisha dhabihu yenye kumpendeza Bwana ni lazima kujua kuwa kila mtu hata wale wasio na hali na wanaodharauliwa wanachukua ndani mwao sura ya Mungu. Umakini huo unatokana na zawadi ya baraka ya Mungu, ambayo inavutia kutokana na mazoezi ya ukarimu mbele ya maskini. Hata hivyo muda wa kujikita katika sala hauwezi kuwa kizingizio cha kuacha kutazama jirani mwenye matatizo. Ni kinyume kwani Baraka ya Bwana inashuka juu yetu na sala inafikia lengo lake hasa kwa kusindikizwa na huduma kwa maskini.

Neno la Mungu linapita nafasi, wakati,sababu na utamaduni

Ni jinsi gani mafundisho hayo ni halisi ya wakati huu kwa ajili hata ya sisi! Papa anasitiza katika kifungu cha tatu. Kiukweli Neno la Mungu linapita nafasi, wakati, sababu na utamaduni. Ukarimu unaowasaidia wadhaifu, unafikiri wenye taabu, unalainisha mateso, na kurudisha hadhi ya aliyekosa, ni hali halisi ya maisha ya kudumu ya binadamu. Uchaguzi wa kujikita kuwa makini kwa  ajili ya maskini, mahitaji yao mengi tofauti, hawezi kudharauriwa na wakati au kuwa masuala ya kibinafsi, hata mipango ya kichungaji au kijamii. Haiwezekani kusukuma nguvu ya neema ya Mungu kutokana na kuwa na tabia ambayo mara nyingi ni kujiweka katika nafasi ya kwanza. Kuweka mtazamo kwa maskini ni ngumu lakini ni muhimu kwa ajili yakujika katika maisha yetu binafsi na ya kijamii katika mwelekeo wa haki. Hii siyo suala la kuwa na maneno mengi badala ya kuwa ni katika matendo ya maisha halisi, yanayosukumwa na upendo wa Mungu. Kila mwaka katika Siku ya Maskini ulimwenguni, hali halisi hii inajirudia kuwa msingi wa maisha ya Kanisa, kwa sababu maskini watakuwapo daima na sisi (rej Yh 12,8) kwa ajili ya kutusaidia kukarimu na kisindikiza Kristo katika maisha ya kila siku.

Maswali mengi ya kujiuliza wakati wa kukutana na maskini 

Kukutana na mtu aliye katika hali ya maskini, daima inatuchangamotisha na kutupatia maswali, Papa anabainisha katika kipengele cha nne. Je ni jinsi gani ya kuchangia kuondoa au kurahisisha hali yake ya kubaguliwa na mateso yake? Tunawezaje kumsaidia katika umaskini wake wa kiroho?  Papa Francisko anafafanua kuwa Jumuiya ya Kikrsito inaalikwa kuhusika katika uzoefu huu wa ushirikishwaji kwa utambuzi kwamba siyo halali  kuweka mwakilishi mwingine. Ili kuwa msaada kwa maskini, na ni vema kuishi umaskini wa kiinjili ukiwa mstari wa mbele. Hatuwezi kuhisi mambo ni sawa, ikiwa mjumbe mmoja wa familia ya binadamu haonekani  na amekuwa kivuli. Kilio cha ukimya kwa maskini wengi kinapaswa kipate watu wa Mungu walio mstari wa mbele daima na kila mahali kupaza sauti kwa niaba yao, ili kuwalinda na kuwatetea, kuwashikamanisha nao dhidi ya  ubinafsi mwingi na ahadi zisizo timizwa na ili kuwakaribisha washiriki katika maisha ya jumuiya. Ni kweli kwamba Kanisa halina suluhisho kamili la kupendekeza, Papa anaongeza,  lakini pia linatoa kwa nguvu ya neema ya Kristo, ushuhuda wake na ishara za ushirikishwaji. Na zaidi Kanisa linahisi uwajibikaji wa kuwakilisha wale ambao hawana mahitaji ya kuishi. Wakristo wanalo jukumu la kukumbusha thamani kubwa ya maisha ya pamoja na hakuna anayesahulika miongoni mwa binadamu ambao wamekiukwa mahitaji yao msingi.

Sintofahamu zinasahu kuwapa maskini ukarimu

Kuwapa maskini kwa ukarimu, unasaidia kugundua, awali ya yote anayetenda kuonesha kwa dhati kuwa  upo uwezekano wa kutenda ishara ambazo zinatoa maana ya ukarimu ya maisha, anafafanua Papa Francisko katika kifungu cha tano. Ni mikono mingapi ya ukarimu inayotolewa kila siku! Kwa bahati mbaya inatokea mara nyingi haraka na kupelekea wingi wa sintofahamu, hadi kufikia kutojua wema ambao kila siku unatendeka katika ukimya na kwa ukarimu mkuu. Hii inajitokeza kwamba inapotokea jambo fulani la kushangaza katika mchakato wa maisha yetu macho yanakuwa na uwezo wa kutambua wema wa watakatifu yaani wa mlango wa jirani “ wale wanaoishi karibu nasi na ni kioo cha uwepo wa Mungu”(Wosia Gaudete et exsultate, 7), na wakati huo huo hakuna yoyote anayezungumza. Habari mbaya ni nyingi katika kurasa za magazeti, katika tovuti, skrini za televisheni hadi kufikiria kwamba ubaya ndiyo unatawala. Lakini “Siyo hivyo”, Papa amebainisha. Kwa hakika ukatili haukosekani na vurugu, ubaguzi na ufisadi, lakini maisha yanesukana na matendo ya heshima na ukarimu ambayo si tu kwamba unalipa ubaya, bali unasukuma kwenda zaidi ya… na kuwa na ujazo wa matumaini.

Kuwapa ukarimu maskini ni ishara ya ukaribu,mshikamano na upendo

Kuwapa ukarimu maskini ni ishara, Papa katika kifungu cha sita anasema. Ishara ambayo inajaribu kukumbusha moja kwa moja ukaribu, mshikamano na upendo. Katika miezi hii, mahali ambapo Dunia nzima imekumbwa na virusi vya corona na kupelekea uchungu na vifo, kukata tamaa na mahangaiko, ni mikono ya ukarimu mingapi iliyonekana! Mikono iliyo wazi ya daktari ambaye alikuwa anaangaikia mgonjwa kwa kujaribu katafuta kila njia ya haki. Mkono wa ukarimu wa muuguzi wa kike na kiume ambaye zaidi ya masaa ya kazi waliyokuwa wakikaa kwa sababu ya kusaidia wagonjwa. Mkono wa ukarimu ulionyoshwa ukifanya kazi katika utawala  na kutafuta vifaa kwa ajili ya kusaidia maisha mengi iwezekanavyo. Mwanafamasia ambaye alikuwa akihudumia mambo mengi  ya watu katika hatari ya kuweza kuambukizwa; Padre ambaye alikuwa akibariki na moyo uliopondoka. Mwanakujitolea ambaye alikwenda kusaidia anayeishi barabarani, ni wangapi licha ya kuwa na paa lakini hawakuwa na chakula. Mkono ulionyoshwa wa ukarimu  wa mwanaume na mwanamke anayefanya kazi kwa ajili ya kutoa huduma muhimu na usalama. Papa Francisko katika kuorodhesha mikono ya ukarimu huo ameongeza ni mikono mingi sana ya ukarimu  ambayo tunaweza kufafanua hadi kufikia litania ya matendo ya wema. Mikono yote hiyo ya ukarimu imechangamotisha maambukizi na hofu japokuwa ilikuwa ni  katika kutaka kutoa msaada na faraja.

Janga hili lilifika kwa ghafla lakini hakuna zana za huruma zilizo za ghafla

Janga  hili lilifika kwa ghafla na likakuta hatuna maandalizi, kwa kutuacha kuwa na ukosefu wa mwelekeo na ukosefu wa nguvu ya kutojua la kufanya, Papa Francisko katika kipengele cha saba anabainisha. Mkono ulionyoshwa wa ukarimu kwa maskini licha ya hayo haukufika kwa ghafla. Huo zaidi ulikuwa unatoa ushuhuda wa jinsi gani ya kujiandaa kutambua maskini ili kumsaidia katika wakati wake wa mahitaji. Papa Francisko aidha amesema, hakuna zana za huruma zinazokuja kwa ghafla. Ni lazima kufanya mazoezi ya kila siku ambayo yanaanzia na utambuzi wa kile ambacho tunahitaji kusaidia kwanza.  Katika kipindi hiki tunachoishi kimewekwa mgogoro mkubwa wa ukosefu wa uhakika. Tunahisi kuwa maskini na wadhaifu zaidi kwa sababu tumefanya uzoefu wa maana ya vikwazo na vizuizi vya uhuru. Ukosefu wa kazi, wa upendo wa jamaa zetu, kama vile ilivyo hata mahusiano ya kawaida binafsi ambayo kwa mara noja yalikatika katika upeo na ambamo hatukuwa tumezoea. Utajiri wetu kiroho na kimwili viliwekwa katika mjadala na kugundua hofu zetu. Kwa kufungwa katika ukimywa nyumbani mwetu, tumegundua umuhimu wa kuwa rahisi na kubaki macho wazi katika mambo yaliyo ya msingi tu. Tumekomaa juu ya mahitaji mapya ya udugu  wenye uwezo wa kusaidiana na kusifiana.

Hiki ni kipindi muafaka cha kihisi kwa upya kwamba tunahitaji mmoja na mwingine Papa Francisko anashahuri na ambapo tunalo jukumu kwa ajili ya wengine na kwa ajili ya ulimwengu (…). Kwa muda mrefu tayari maadili yalikuwa yamepungua na kuanza kuchezea maadili, wema, imani na ukarimu (…) Uharibifu wa kila msingi wa maisha ya kijamii, unaishia katika kugombana mmoja dhidi ya mwingine katika hali ya kutetea kila mmoja mafao yake  mwenyewe na kusababisha kuzuka kwa mitindo mipya ya vurugu na ukatili aidha kuzuia maendelea ya utamaduni wa kweli wa kutunza mazingira ( Wosia Laudato si’, 229). Kwa hayo yote kipeo kikubwa cha uchumi, kifedha na kisiasa, Papa Francisko anasema hakitaisha hadi tukapotambua kuwajibika kila mmoja kumsaidia mwingine na kila mtu.

Kuwapa ukarimu maskini ni uwajibikaji na chachu ya kubeba mzigo wa wengine

Kuwapa ukarimu maskini ni mwaliko wa uwajibikaji na  kama jitihada za moja kwa moja  kwa yule anayehisi ushiriki wa hatima hiyo, ndiyo Papa Francisko anaanza katika kifungu cha nane. Ni chachu ya kujitwisha mzigo wa wadhaifu kama anavyokumbusha Mtakatifu Paulo “tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.”(Gal 5,13-14; 6,2). Mtume anafundisha kuwa uhuru tuliopewa kutokana na  kifo na ufufuko wa Yesu Kristo ni kwa ajili ya yetu, kuwa na uwajibikaji kwa ajili ya wengine hasa walio wadhaifu zaidi. Siyo ushauri wa kuchagua bali ni hali halisi ya dhati ya imani ambayo tunakiri. Kitabu cha Sira kinarudi kuwa msaada wetu kwani Papa Francisko anasisitiza kinashauri matendo ya dhati ya kusaidia walio wadhaifu zaidi na kinatumia baadhi ya picha. Awali ya yote kinazingatia udhaifu wa walio na huzuni “Usiwape kisogo wanao omboleza (Sir 7,34). Kipindi cha janga kimelazimisha kwa nguvu zote kubaki na upweke na kutuzuia kutofariji na kukaa karibu na marafiki na jamaa wenye huzuni kutokana na kuondokewa na wapendwa wao. Bado mwandishi wa hekima anasema “Usiache kuwatembelea wagonjwa( Sir 7,35). Tumefanya uzoefu wa kakaa karibu na anayeteseka na wakati huo huo kuwa na dhamiri ya udhaifu wa kuishi kwetu. Kwa hakika Neno la Mungu halituachi tuwe na utulivu kamwe na zaidi linendelea kuwa chachu ya kuweza kutenda  yaliyo wema.

Wape ukarimu maskini katika kupinga tabia za wazembe na ulimbikizaji wa mali

Wape ukarimu  maskini kwa kupinga tabia za wale hasa wanaobaki wameweka mikono yao mifukoni na wahaondoki mahali walipo kwenda kwa maskini anabainisha Papa Francisko katika kifungu cha tisa, na kwamba mara nyingi hao ndiyo wanaochangia umaskini huo. Sintofahamu na shuku ndiyo chakula chao kila siku. Mambo hayo ni kinyume na yule ambaye daima ana  mikono ya ukarimu iliyoelezwa! Kuna walio na mikono  ya ukarimu kwa  haraka katika compyuta ili kupeleka kiasi cha fedha kutoka sehemu moja kwenda  nyingine ulimwenguni, huku wakilimbikiza kutoka utajiri wa sehemu zilizo finyu na  shida ya umati au kutofaulu kwa mataifa yote. Kuna wengine wanatoa  mikono yao kwa kukusanya fedha nyingi kutokana na kuuza silaha ambazo zinaishia katika mikono mingine hata kwa watoto kuwatumia kupanda vifo na umaskini. Kuna mikono mingine iliyonyoshwa kwenye vivuli, huku ikibadilisha dozi ya vifo kwa ajili ya kujitajirisha na kuishi kwa raha bila kujali shida za wengine.  Kuna mikono mingine iliyonyoshwa ambayo inabadilishana faida zisizo halali za haraka na ufisadi. Kuna hata mikono mingine ambayo umenyoshwa kwa ubinafsi kwani inaweka sheria ambazo kwao haziwasaidii.

Katika mtazamo wote huo waliobaguliwa wanabaki wakisubiri. Ili kuweza kusaidia mtindo mmoja wa maisha ambao haubagui wengine au kuweza kuwa na shauku ya mawazo haya ya kibinafsi, wameunda utandawazi wa sintofahamu. Hii hata bila kujali tumegeuka kuwa wasio na uwezo wa kushikwa na huruma mbele ya kilio cha uchungu wa wengine , hawalii mbele ya majanga ya wengine na wala kujishughulisha kuwatunza, utafikiri wao siyo wahusika na wala hayawagusi (Wosia Evangelii gaudium, 54). Kwa njia hiyo Papa Francisko anabainisha kwamba hatutakuwa na furaha kama mikono inayopanda vifo  haitageuka kuwa chombo cha haki na amani kwa ulimwengu mzima.

Katika matendo yako yote kumbuka mwisho wako

Katika matendo yako yote kumbuka mwisho wako (Sir 7,36) ndiyo kifungu cha kumi kinachohitisha ujumbe wa Papa Francisko wa siku ya Maskini duniani 2020. Papa anaeleza kuwa ni kielelezo ambacho  Sira anahitimisha tafakari yake. Kifungu hiki kinatafsiri mbili. Ya kwanza ni ile ambayo sisi tunahitaji kuzingatia daima hasa mwisho wa maisha yetu. Kukumbuka hatima yetu inaweza kuwa msaada wa kutusaidia katika maisha ya kuwa na uangalifu kwa wale ambao ni maskini zaidi na hawakupata fursa kama sisi wenyewe. Ipo tafsiri ya pili ambayo zaidi ya mwisho lengo lake  ni kumwelekea kila mmoja anachotarajia, Papa Francisko anafafanua. Mwisho wa maisha yetu unataka uwe na mpango wa kutimiza na safari ya kutimiza bila kuchoka na kwa maana hiyo mwisho wa kila matendo yetu. Haiwezekani kuwa tofauti na upendo. Ndiyo lengo ambalo sisi tunatembea ndani mwake na ambalo hakuna jambo lolote lituondolee  mtazamo huo. Upendo huo ni ushirikishwaji, kujitoa na huduma japokuwa  unaanzia kwa kugundua sisi wenyewe tukiwa wa kwanza kupendwa na kuamshwa kwa upya katika upendo. Mwisho huo unafanana kama vila mtoto anapokutanisha macho yake na mama yake, anahisi kupendwa kwa kuwa yeye anaishi. Hata tabasamu kwa maskini ni kisima cha upendo na kumruhusu aishi kwa furaha. Kuwapa ukarimu maskini kwa njia hiyo unatajitajirisha na tabasamu ya yule ambaye haleti usumbufu kwa uwepo wake, au msaada ambao anatoa japokuwa unafurahisha tu kwa kuishi mtindo wa wafuasi wa Kristo,

Katika safari yetu ya kukutana na maskini kila siku  anatusindikiza Mama wa Mungu ambaye zaidi ya kila kitu ni Mama wa Maskini. Bikira Maria anajua kwa karibu ana matatizo na mateso ya wale ambao wamebaguliwa, kwa sababu yeye mwenyewe alionja katika hali kujifungua Mtoto wa Mungu katika holi la wanyama. Kwa sababu ya hatari ya Erode, akiwa na Yosefu mchumba wake na mtoto Yesu walikimbilia katika nchi nyingine na ni hali ya ukimbizi ambayo ilikumba hata Familia Takatifu. Mama Maria wa maskini anaweza kupokea sala za watoto wake wapendwa na wale ambao wanahudumia kwa jina la Kristo, na wanageuka kuwa na mikono ya ukarimu, mikono ya ushirikishwaji na udugu uliopatikana.

13 June 2020, 11:30