Tafuta

Vatican News
2020-06-21 Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili ya wakimbizi 2020-06-21 Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili ya wakimbizi  

Papa Francisko:Wito wa kuzuia hatari zinazowakabiri wakimbizi kukosa ulinzi na usalama!

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana mawazo yake na sala ni kwa ajili ya wakimbizi wanaolazimika kutafuta mahali pa usalama kutokana na majanga katika fursa ya kukumbuka siku ya wakimbizi duniani iliyofanyika tarehe 20 Juni 2020.Amewatakia heri nyingi mababa wote katika siku yao iliyoadhimishwa katika mataifa mengi ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Jana Umoja wa Mataifa umeadhimisha Siku ya Wakimbizi Ulimwenguni. Mgogoro uliosababishwa na virusi vya corona umeweka mwanga kuhusu mahitaji ya kuhakikisha ulazima wa ulinzi kwa watu wakimbizi, kuwahakikishia hadhi yao na usalama. Ni maneno ya Papa Francisko mara baada ya tafakari ya Neno la Mungu na sala ya Malaika wa Bwana Jumapili, tarehe 21 Juni 2020 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican Katika kukumbuka Fursa ya Siku ya Wakimbizi duniani iliyofanyika tarehe 20 Juni 2020, Papa Francisko ametoa mwaliko wa kuungana na sala zake ili kupyaisha jitihada kwa ajili ya wote katika kusaidia ulinzi wa kila mtu, kwa namna ya pekee wale ambao wanalazimika kukimbia hali ngumu ya hatari kwa maisha yao au familia zao.

Papa akumbuka harakati za usafi wa mazingira

Mantiki nyingine ambayo janga la corona limetufanya tutafakari ni kuhusu uhusiano wa binadamu na mazingira, anasema Papa Francisko. Kuwekwa karantini, kumepunguza uchafuzi wa mazingira na kufanya tugundue uzuri wa maeneo mengi mazuri bila kuwa na foleni na kelele. Kwa sasa ambapo zimeanza shughuli kwa upya, ni lazima kuwa wahusika zaidi wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, Papa Francisko amehimiza. Katika muktadha wa mazingira Papa Francisko anawapongeza kuanzishwa kwa harakati za mambo mengi ambayo kila kona ulimwengu wanakijita nayo na yanazaliwa  mengine kuanzia chini kwa maana ya kwenda katika mwelekeo huo. Kwa mfano, Papa Francisko amebainisha kuhusu jijini Roma ambapo Jumapili wamejikita kufanya  usafi wa mto wa Tevere. Lakini pia amekumbuka hata katika sehemu nyingi! Mambo yote hayo amesema yanaweza kusaidia raia kuwa na utambuzi zaidi wa wema huo msingi wa pamoja.

Heri kwa mababa wote ulimwenguni

Papa Francisko amekumbuka kuwa kama nchini Argentina nchi yake na kama ilivyo katika nchi nuingine wameadhimisha siku ya baba: “ Ninawakikishia ukaribu na sala kwa baba wote , sisi sote tunatambua kwamba kuwa baba siyo kazi rahisi, kwa maana hiyo tusali kwa ajili yao. Ninakumbuka kwa namna ya pekee hata baba zetu ambao wanaendelea kutulinda wakiwa mbinguni.

Mtakatifu Aloysius  Gonzaga kijana aiyekufa akihudumia wagonjwa

Katika salam zake kwa mahujaji waliofika kutoka sehemu mbali mbali za Italia, Papa ametoa wazo lake kwa namna ya pekee kuhusu vijana kwa kuwakabidhi katika maombezi ya Mtakatifu Aloysius Gonzaga. Ni kijana aliyekuwa amejazwa na upendo wa Mungu na kwa ajili ya jirani. Alifariki akiwa kijana sana jijini Roma kutokana na kupata maambukizi wakati wa kusaidia wagonjwa wa mlipuko wa janga la virusi. Papa Francisko amewasalimia watu wa Roma na mahujaji kutoka pande zote za Italia na zaidi hata katika Nchi nyingine, maana katika uwanja wa Mtakatifu Petro zilionekana hata bendera nyingine. Kwa kuhitimisha wametakia Kwa wote mlo mwema lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

22 June 2020, 08:21