Tafuta

Vatican News
2020.06.07 Angelus: Sala ya Malaika wa Bwana 2020.06.07 Angelus: Sala ya Malaika wa Bwana   (Vatican Media)

Papa Francisko:Utatu Mtakatifu ni upendo unaokomboa ulimwengu!

Mama Kanisa akiwa anaadhimisha siku kuu ya Utatu Mtakatifu,Papa Francisko wakati wa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana amejikita kufafanua Injili ya Yohane na kwamba anaonesha kwetu fumbo la upendo wa Mungu.Kazi ya kwanza ya maisha ya Mkristo ni kumtafuta Mungu ambaye ni upendo katika Mwana na katika Roho Mtakatifu na ambaye anaunganisha upendo huo kwetu sisi wanadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika Injili ya leo kwenye siku kuu ya Utatu Mtakatifu (Yh 3,16-18), Mtume Yohane anatumia lugha rahisi kuonesha fumbo la upendo wa Mungu kwa ajili ya ulimwengu, aliouumba. Katika kuelezea mazungumzo ya Nikodemu na Yesu anamwakilisha Yule ambaye analeta utimilifu wa mpango wa wokovu wa Baba kwa ajili ya ulimwengu, ni ishala ya wokovu wetu. Mungu aliumba dunia nzuri, lakini baadaye dhambi imeoneshwa na ubaya na ufisadi, sisi sote wanaume na wanawake wote tu wadhambi; na zaidi Mungu anaweza kuingilia kati na kuhukumu ulimwengu, ili kuharibu ubaya na kutoa adhabu kwa wadhambi. Kinyume chake Yeye anapenda ulimwengu licha ya dhambi zake; Mungu anampenda kila mmoja hata anapokosea na kuwa mbali na Yeye. Mungu baba anapenda kiasi kwamba ili kuweza kuuokoa, anatoa kilicho chake chenye thamani, yaani Mwanaye wa pekee, anayetoa maisha kwa ajili ya watu, anafufuka, anarudi kwa baba na pamoja na Yeye wanatuma Roho Mtakatifu.

Utatu Makatifu ni Upendo, upo kwa ajili ya huduma ya ulimwengu wote

Ni tafakari ya Papa Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 7 Juni 2020, ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Utatu Mtakatifu yaani Mungu  Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu, siku siku kuu ambayo inafanyika wiki moja baada ya sikukuu ya kushuka kwa Roho Mtakatifu. Katika kuendelea na tafakari Papa amesema Utatu Makatifu kwa maana hiyo ni Upendo, upo kwa ajili ya huduma yote ya ulimwengu, ambao anataka kuukomboa na kuumba kwa upya. Kwa kufikiria leo hii  kuwa Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, tufikirie upendo wa Mungu! Na vema kuwa sisi tunahisi kupendwa. “Mungu ananipenda” na ndiyo hisia ambayo lazima kuwa nayo kwa siku ya leo.

Sisi ni watoto katika Mwana kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Sisi ni urithi wa Mungu

Papa Francisko akiendelea na tafakari yake kwa waamini  waliokusanyika katika uwanja wa Matakatifu, Petro mara baada ya karantini katika kipindi cha janga, anasema: “Wakati Yesu anapothibitisha kuwa Baba alimtoa Mwanaye wa pekee, mara moja tunaijiwa na wazo la Ibrahim kwa kumtoa sadaka mwanaye Isaka kama inavyosimuliwa katika kitabu cha Mwanzo (rej. Mw 22,1-14). Tazama! hiki ni kipimo bila kipimo “cha upendo wa Mungu”, anafafanua Papa. Kwa njia hiyo amewaalika kutafakari jinsi ambavyo Mungu alijionesha kwa Musa kama mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli  na mwaminifu. Katika kukutana  na Mungu umlitia moyo Musa ambaye kama Kitabu cha Kutoka kinavyosimulia hakupata hofu ya kuwalekea kati ya watu na Bwana kwa kusema “, nakuomba, Bwana, uende kati yetu maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako. (Kut 34,9).” Ndiyo alivyo fanya Mungu kwa kumtuma Mwanaye. Sisi ni watoto katika Mwana kwa nguvu ya Roho Mtakatifu! Sisi ni urithi wa Mungu! Amesisitiza Papa

Tuache tushangazwe kwa upya na uzuri wa Mungu

Papa Francisko amesema “siku kuu ya leo inatualika kujiachia kwa upya tushangazwe na uzuri wa Mungu; uzuri wa wema na ukweli usioisha. Lakini hata uzuri wema na ukweli unyenyekevu, wa karibu ambao umefanyika mwili na kuingia katika maisha yetu, katika historia yetu, historia yangu na ya kila mmoja wetu ili kila mwanaume na mwanamke aweze kukutana naye na kuwa maisha ya milele. Hii ndiyo imani ya kumkaribisha Mungu upendo ambaye anajitoa katika Kristo na ambaye anafanya tusukumwe na Roho Mtakatifu; kujiachiaa tukutana na Yeye na kumwamini  katika Yeye. Haya ndiyo maisha ya Kikirsto: kupenda , kukutana na Mungu, na kumtafuta Mungu: na Yeye anatutafuta akiwa wa kwanza, Yeye ndiye anatangulia kukutana na sisi akiwa wa kwanza! Papa amesisitiza. Bikira Maria aliye ndani ya Utatu Mtakatifu atusaidie kukaribisha kwa moyo ulio wazi upendo wa Mungu na kutujaza furaha na maana ya safari yetu katika ulimwengu huu kwa kutazamia daima hatima ya ambayo ni Mbinguni.

07 June 2020, 13:13