Tafuta

Vatican News
Janga la covid-19 bado linatikisa ulimwengu! Janga la covid-19 bado linatikisa ulimwengu!  (AFP or licensors)

Papa Francisko:Ukaribu wa Papa kwa watu wanaoteseka na janga!

Mara bada ya sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Papa amesalimia mahujaji wote wa Italia na wengine ambao wameanza kipindi cha pili katika harakati za kupambana na janga la virusi vya corna, japokuwa ameonya wasishangilie ushindi badala yake kuzingatia kanuni zilizowekwa za kujikinga.Mawazo pia kwa nchi nyingine ambazo bado zinaendelea na mapambano ya covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 7 Juni 2020, Papa Francisko amewageukia wanahija wa Roma na kila mwamini, familia na jumuiya za kidini. Kwa mara nyingine tena janga la covid-19 limerudi katika mawazo ya Papa kwani amesema uwepo wao katika uwanja ni ishara ya kuanza kwa upya nchini Italia kipindi cha kushinda janga, japokuwa ametoa onyo kuwa wasiimbe ushindi kwa sababu bado inabakia ulazima wa kufuata sheria zilizowekwa. Kwa bahati mbaya, Papa Francisko amebainisha kuwa katika nchi nyingine virusi bado vinaendelea kuathiri watu wengi. Kwa kutoa mfano amesema, “siku ya  Ijumaa iliyopita katika nchi amekufa mtu mmoja kila dakika moja, hii ni  hali mbaya”. Kufuatia na hilo Papa Francisko amependa kuonyesha ukaribu wake kwa watu, wagonjwa na familia zao na wote ambao wanatoa huduma ya kuwatunza na kuwasadia.

Zaidi ya waathirika 400,000 wa covid-19

Ikiwa katika Nchi nyingi za Ulaya maambukizi yameanza kupungua, Bara la Amerika ya Kusini kuinyume chake idadi ya waathirika inazidi kupanda kwa kasi, kwa mujibu wa takwimu za wiki ya mwisho, idadi ya kati ya maambukizi mapya ya covid-19  imebainisha zaidi ya 100,000 kwa siku. Takwimu hizi zinathibitishwa ni jinsi gani janga bado halijamalizika! Maambukizi ulimwenguni kwa sasa  ni milioni 6.9, waathirika ni zaidi ya 400,000 na Marekani  ambao wanalipa gharama kubwa zaidi kwa vifo zaidi ya 109,000. Baada ya Uingereza kwa  vifo  zaidi ya 40,000, kuna sasa nchi ya  Brazil ambayo tarehe 6 Juni 2020 imeonesha kuongezea kwa  asilimia 904, na kufika vifo vya watu  35,930. Katika bara la Amerika ya Kusini wasiwasi mkubwa ni  katika nchi ya Peru, ikipambana na upungufu mkubwa wa oksijeni. Kadhalika maambukizi yanaendelea katika Nchi za Mashariki na Afrika.

Janga la Covid -19 katika nchi za Amerika ya Kusini

Kufuatia na janga la virusi vya corona au covid-19, Kanisa la Chuquibambilla limeanza kugawa barakoa katika maeneo yaliyo hatari ya maambukizi. Hili ni eneo ambalo ni maskini sana nchini Peru, na shukrani kwa Shirika la Wamisionari wa Yesu Neno na dhabihu ambapo wamepata kutengeneza barakoa 2400 na kuwagaiwia wakazi wa maeneo hayo. Askofu  Edison Farfán OSA, wa kwa kushirikiana na Caritas ya Chuquibambilla na Parokia ya San Salvador de Antabamba,wamejikita katika shughuli katika  jumuiya mbalimbali za wakulima katika vijiji na miji ya wilaya za Antabamba, Cotabambas na  Grau, Katika Mkowa  wa Apurímac, ili waweze kupata hata msaada wa kiroho kwa upande wa Mapadre. Wamefanya kazi hili angalau vikapu 1, 200 vilivyojaa kila aina ya mahitaji viweze kusambazwa kwa familia zilizo athirika sana huko Chuquibambilla, kwa namna ya pekee katika wilaya ya Antabamba. Na hatimaye wameweka mpango wa kila parokia mahalia ili wasaidie watu walioambukiza na Covid-19.

Nchini Bolivia msaada kutoka Caritas kwa wafungwa wa Chonchocoro

Chakula na vifaa vya madawa vimetolewa na Caritas nchini Bolivia kwa wafungwa 490 katika Magereza ya  Mtakatifu Pedro de Chonchocoro”, katika wakati huu wa janga la virusi vya corona. Jengo hilo lipo kwenye Plateau ya juu, zaidi ya mita 4 elfu juu ya usawa wa bahar. Nyumba ya gereza imezungukwa na nchi kavu, isiyo na maji ya kunywa ikiwa siyo tu yale ambayo hupatikana kutoka kisima kimoja na inazungukwa hewa ya baridi sana. Kwa njia hiyo, anasema Marcela Rabaza katibu mtendaji wa Caritas, kwamba “kuona misaada ya kibinadamu ikiwasili katika sehemu kama hiyo imezua hisia na shukrani miongoni mwa wafungwa”. Kwa hakika waliweza kupokea msaada huo na kutiwa moyo, tumaini na mwamko wa kutosahaulika  na kwamba janga Covid-19 haliikuwakilisha kwao kama kikwazo cha kuweza kukutana nao.

Hata hivyo Caritas nchini Bolivia mwanzoni mwa Mei waliweza pia kuwafikia Gereza jingine la Villamontes, mahali ambamo wanaishi wafungwa 74 miongoni mwao kuna wazee na walemavu. Kituo hicho kilikabidhiwa vyakula, vifaa vya usafi na vifaa vya kusafisha, pamoja na vitu vingine kwa ajili ya  utunzaji na uzuiaji wa Covid-19. Itakumbukwa kwamba michango hiyo ilifanywa shukrani  kwa ufadhili kutoka Cafod,ambalo ni  shirika la maendeleo la nje Katoliki la baraza la Maaskofu wa Uingereza na Wales.

07 June 2020, 13:19