Vatican News
Jumapili 14 Juni Papa ataadhimisha Misa  katika Sikukuu ya Mwili na Damu ya Yesu Jumapili 14 Juni Papa ataadhimisha Misa katika Sikukuu ya Mwili na Damu ya Yesu   (Vatican Media)

Papa Francisko:Tunaalikwa kutafuta hata tabernakulo za mateso,maskini na wenye upweke!

Wakati wa salam kwa lugha ya kiitaliano,Papa Francisko amekumbusha Siku kuu ya Mwili na damu ya Yesu inayoadhimishwa Alhamisi 11 Juni.Licha ya Taberkulo ya Kanisani tunayopaswa kumtafuta Yesu,zipo tabernakulo nyingine za mateso,maskini na walio na upweke.Amekumbusha mwezi Juni uliotolewa kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.Katika Moyo wa mwokozi uliochomwa mkuki panabubujika kisima cha faraja zote na bahari ya huruma ya Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mara baada ya katekesi, siku ya Jumatano tarehe 10 Juni 2020, Papa Francisko amewasalimia watu wote na zaidi, katika lugha ya kitaliano, amewakumbusha kuwa  siku ya Alhamisi 11 Juni, ni si Siku kuu ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo. Mwaka huu haiwezekani kusheherekea kama kawaida kwa  maandamano ya umma, lakini pamoja na hayo tunaweza kusheherekea  katika maisha ya Ekaristi,amesisitiza.

Papa Francisko amesema Ostia iliyobarikiwa inafumbata na ni Yesu mwenyewe. Sisi sote tunaalikwa kumtafuta mbele ya Taberkulo Kanisani, lakini hata katika tabernakulo nyìngine ambazo ni za mwisho, kama vile za mateso, watu walio peke yao na maskini. Aidha mawazo ya Papa Francisko pia yamewaendea kwa namna ya pekee wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Wote amewashauri kupata nguvu za lazima kutoka katika Ekaristi ili kuishi kwa nguvu ya ukristo katika wakati mgumu sana.

Katika salam kwa watu wote wa lugha ya kipoland,  Papa Francisko amewakumbusha kuwa mwezi Juni umetolewa kwa ajili ya Moyo Mtakatifu wa Yesu na ambao kwa namna ya pekee amesema unasikika sana katika utamaduni wao. Moyo wa Mungu uliojaa amani na upendo na kwa maana hiyo ameongeza kusema, tunaweza kumwelekea wasiwasi wote wa mioyo yetu na upendo wetu usio mkamilifu. Katika Moyo wa mwokozi  uliochomwa mkuki panabubujika, kwa ajili ya ubinadamu wote,kisima cha faraja zote na bahari ya huruma ya Mungu.Yesu mpole na mnyenyekevu tufanye mioyo yetu ifanane na ya kwako! amewabariki.

10 June 2020, 14:17